Wakubwa naomba kueleimishwa na aina ya siasa ya bongo! Hivi kwa mtaji huu kila mtu si atakuwa mwanasiasa kama kazi ni kutoa ahadi pasipo kuwatajia source ya hizo hela zitatoka wapi? Mimi ninaamini kwa sasa hamna hela serikalini basi tunapopewa ahadi pia tuambie kitafanyika nini ili kuongeza kwa ajili ya kutimiza hizo ahadi. Mimi naona watu tunafanywa kama watoto au wajinga fulani. Basi wagombea wote wanaotoa ahadi waainishe hela zitapatikanaje kwa maana hizo ahadi hazipo kwenye bajeti! Tuelezwe vizuri kama kutakuwa source mpya za mapato. Nimechoka kusikiliza wagombea wetu. Nchi tunahijua kwa kipato chake.