G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Zipo ishara za wazi sana kuwa Rais Magufuli anaenda kushughulikiwa vilivyo na jumuiya za kimataifa na litakalotokea mpaka watanzania wenyewe watashangaa.
Nimemsoma Dr. Christopher pahala (Huyu ni mbobezi wa mambo ya uchaguzi Afrika) anasema wazi kuwa ipo hofu Tanzania kuwa kama Zimbabwe baada ya huu uchaguzi mkuu ujao. Hili hata mimi sina shaka nalo kabisa. Tumejijengea heshima ya hovyo mbele ya mataifa wenzetu ambayo hapo kabla walituona kama mfano halisi wa ukuaji wa demokrasia.
Rais Magufuli aliahidi kuwa uchaguzi mkuu utakuwa huru na wa haki baada ya kujiaminisha kuwa wapinzani walishajifia na hakuna mtanzania atakayewaunga mkono. Alijiamini kuwa ameleta maendeleo sanaaa hivyo atakubalika kirahisi yeye pamoja na wagombea wenzake wa CCM.
Kwanza kushindwa kuujua ukweli huko ardhini ni udhaifu mkubwa sana kwa kiongozi anayejidai kujiamini. Amelazimika kuikana ahadi yake ya uchaguzi kuwa huru na wa haki. Amelazimika tena hadharani na ameenda mbali zaidi hata kuonekana kituko mbele ya jamii.
Tuseme ukweli, kama siyo uthubutu binafsi wa Tundu Lissu na Maalim Seif basi yaliyotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa yangekuwa yaleyale ya uchaguzi mkuu. Hawa watu wamepigana kweli kweli na nadiriki kusema kuwa wamevishinda vita.
Aidha kuna haja ya kumshukuru sana Tundu Lissu kwani kwenye huu uchaguzi "ame act" kama kiongozi mkuu wa watanzania. Amezijua shida za watanzania kwa muda mfupi kuliko Rais waliyekuwa naye kwa miaka mitano. Amefanya tuone kumbe Rais alikuwa hafanyi chochote kile kwa ustawi wa maendeleo ya watanzania. Alijielekeza kwenye mambo yake binafsi anayoyajua yeye.
RAI YANGU: Magufuli be careful and watch iti! Hizo nguvu unazodhani unazo, huna! Na zaidi watakaoumia ni watanzania na nikueleze wazi kuwa kwa yanayoendelea huko mikoani mpaka sasa unaonekana huna ukaribu na watanzania wengi. Huo ndiyo ukweli wenyewe na ukitaka umeze au uteme ila utabaki kuwa hivyo.