Ah.. Sijui wenzangu...ila kwa sisi tuliowahi kutumia usafiri huu tuli-enjoy sana!!

hivi kwa sasa nikitaka inakuwaje???hop sijachelewa sana...na huu uzee!..lo!

Poa tu ila sijui kama ina viwango kama kipindi kile! Miaka ya karibuni mara ajali,mara migomo,mara nini.. Sijui kama ina viwango tena ..
 
Dah ilikuwa raha sana sana, Reli ya kati nilishawahi panda na Tazara, mpaka pale Salanda aisee raha kweli na Dodoma unapita mida ya mchana mchana unachapa usingizi weeee mpaka unachoka mwenyewe!

Kiukweli, wanasiasa ndo wameharibu ladha zote za usafiri wa reli kwa lengo la kuhakikisha tumbo lao lina shibe ya kutosha!

LIMENIUMA SANA!

Yaani panakuwa kama kwenu vile.. Mara miswaki,mnapiga stori na mtu usiyemjua,mara giza linaingia,mara unaenda kula(akina mama lazima wabebe vyakula visivyoharibika kama chapati,maandazi),mara kulala.. Mara kesho tena.. Acha tu..
 
King'ombe namkumbuka..

Aisey Gamba, uliwaza nini kutukumbusha hii maneno ? Inasisimua kiaina yake!
Unamkumbuka yule Mz. Kipofu wa kigogo, alikua anatembea sana na Train akipuliza filimbi ?
Unamlipa sh 50 (sungura) au sh 1 ya (mwenge) au sent 20 ya (mbuni) kisha unachagua wimbo.
 
nilivyoona thread tu nikajua utakuwa unazungumzia treni........

Acha nikasomee fani ya sheikh yahaya...
 
Aisey Gamba, uliwaza nini kutukumbusha hii maneno ? Inasisimua kiaina yake!
Unamkumbuka yule Mz. Kipofu wa kigogo, alikua anatembea sana na Train akipuliza filimbi ?
Unamlipa sh 50 (sungura) au sh 1 ya (mwenge) au sent 20 ya (mbuni) kisha unachagua wimbo.

Aisee we ni kiboko..
Nimekukubali Judgement.. Yule mzee bana alikuwa na ustadi wa aina yake.. Hela unayompa ndogo sana ukilinganisha na uwezo wa kuiga nyimbo kwa filimbi..

Na dili zake kwenye treni!
 
Aisee we ni kiboko..
Nimekukubali Judgement.. Yule mzee bana alikuwa na ustadi wa aina yake.. Hela unayompa ndogo sana ukilinganisha na uwezo wa kuiga nyimbo kwa filimbi..

Na dili zake kwenye treni!

Basi mie nilikuwa nikimuotea yule Babu sikubali anipite bila kunipigia wimbo wa Tabora Jazz , hasa Dada Asha nilikua naupenda sana .
 
Yaani panakuwa kama kwenu vile.. Mara miswaki,mnapiga stori na mtu usiyemjua,mara giza linaingia,mara unaenda kula(akina mama lazima wabebe vyakula visivyoharibika kama chapati,maandazi),mara kulala.. Mara kesho tena.. Acha tu..

daraja la kwanza na la pili sikuwahi kuonja raha yake zaidi ya kusimuliwa kama hivi, btw hivi reli ya kati ndo imetelekezwa? Ooo poor we Tanzanians!
 
Dah, umenikumbusha mbali sana.

Ukikaa 3rd class ukinyanyua mguu, kuurudisha chini utajibeba.
Salanda, kuku alikuwa na paja kubwa kama la paa
Buffet, ndo kulikuwa wanakaa wajanja na wenye pesa, kibinti kikijipisha pitisha pale ama zake ama za mapedeshee wa kwenye treni.

..kama nakuona vile .. ukiwa 3rd class, form one na sumatra lako kichwani na warrant yako mfukoni ...chini umepiga bugaluu na raizon ngazi mbili ..juu slim fit
 
daraja la kwanza na la pili sikuwahi kuonja raha yake zaidi ya kusimuliwa kama hivi, btw hivi reli ya kati ndo imetelekezwa? Ooo poor we Tanzanians!

Mi daraja la kwanza,sikuwahi...

Daraja la pili,kuna ....seating,na ...sleeping.

Sijui gharama za uendeshaji wa shirika la umma kama lile.. Halihitajiki kupata faida maana linatoa huduma.. Sema ajali ndiyo mbaya kwani behewa moja nasikia si chini ya Mil. 500...!
 
Tutapanda za umeme ma dia...hizi za kihindi usizitamani kabisa!

Keshachelewa da' Canta,kweli mfanyie tu mpango wa kuionja ya umeme.... Hizi za Kihindi kweli hazina viwango stahiki siku hizi..
 
Back
Top Bottom