Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,513
113,644
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nikipata fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa"

Hili ni maslahi ya taifa ya pongezi kwa TRC nimeona mzigo wa mabehewa mapya ya kisasa ya reli ya kisasa ya SGR ukipokelewa bandarini, DSM, hivyo hatua ya kwanza ni kutoa pongezi kwa TRL kwa kazi hii kubwa, ngumu nzuri yenye maslahi makubwa kwa taifa.

Kwa vile kabla ya kupokelewa kwa mabehewa haya, huko nyuma TRC, walitoa taarifa kwa umma kuhusu vichwa na mabehewa ya reli ya SGR, taarifa hiyo iliandamana ni picha za vichwa na mabehewa ya treni hizo, yakionyesha ni vichwa na mabehewa mchongoko!, lakini baada ya picha za mabehewa haya kuwasili na kuonyesha ni tofauti na zile za kwenye picha za mwanzo, mabehewa haya ni box body na sio mchongoko, hali iliyopelekea ujio wa mabehewa haya mapya, kupokelewa kwa mixed feelings, TRC Serikali na baadhi ya watu wakisema ni mabehewa mapya, huku wananchi na mitandaoni wakipiga kelele ni mabehewa used, mitumba, chakavu ya muundo wa kizamani, yaliyo karabatiwa na kutiwa nakshi nakshi tuu!.

Waziri Mkuu. Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa, alipotembelea nchini Korea Kusini kukagua kazi ya uundaji mabehewa yetu kampuni ya Sung Shin Rolling Stock Technology Company (SSRST) na hiki ndicho Waziri Mkuu alichokisema


Hii maana yake, mabehewa haya ni mapya kabisa kutoka kiwandani.

Kwa sisi baadhi yenu, tulioishi nchi za wenzetu, tumepanda treni hizi za kisasa za kasi zinazoendeshwa kwa umeme, ziko za aina mbalimbali, kuna zile za kasi, bullet trains, ambazo zinakwenda hadi kasi ya speed 360kmh kwa saa!, na kuna hizi za kawaida kama SGR yetu, yenyewe speed yake ni hadi 160 kph kwa saa.

Vichwa na Mabehewa ya treni hizi pia yana tofautiana ki usasa, mitindo na muonekano, ila mabehewa ya abiria ya wenzetu tuliyo yapanda, sio kama haya tunayo letewa sisi!, hivyo kwanza natoa hongera sana TRC kwa mabehewa haya mapya kuwasili nchini, hii ni hatua kubwa muhimu.

Kwa vile reli yetu ya SGR ni reli mpya na ya kisasa, je vichwa, mabehewa haya tulioletewa ni mabehewa mapya ya kisasa? Kwa jicho langu tuu la kawaida, naona kama behewa hilo ni na mtindo wa yale mabehewa ya kizamani, ila pia mabehewa kuonekana kwa mtindo wa mabehewa ya kizamani, sio issue, inawezekana ni muonekano tuu, sio lazima yawe ni mabehewa ya zamani, used, inawezekana kabisa, haya ni mabehewa mapya kabisa, ila yameundwa kwa mtindo wa kizamani, hivyo mabehewa haya ni mapya, sio mitumba, sio used, sio mabehewa chakavu ni mabehewa new brand!.

Ila hata kama yangekuwa ni mabehewa yaliyotumika, kumaanisha ni used, Watanzania tuelezwe tuu ukweli, Watanzania ni watumiaji wazuri wa vifaa used, na hakuna ubaya wowote kutumia vitu vilivyotumika yaani used au mitumba, Ila kitu muhimu ni kwa ubora, uimara na umadhubuti wa vifaa hivyo, kuna vifaa used ni bora, imara na madhubuti kuliko vifaa vipya!. Kama mabehewa haya ni used, Watanzania tuelezwe tu ukweli kuwa mabehewa haya ni used, na sio TRC na viongozi wetu watueleze tumenunua mabehewa mapya ya kisasa, kumbe ni mabehewa mitumba used yaliyo karabatiwa, kupakwa rangi na kufanyiwa nakshi nakshi tu!.

Mwanzo tuliahidiwa hiviPicha namba 1
Tumeletewa haya mabox Picha namba 2
Ni huzuni

View attachment 2424970View attachment 2424971
Madai ya Vichwa na Mabehewa Yetu Kupigwa Mnada!
Mabehewa 30 na vichwa 2 vya treni za SGR mali ya TRL vinapigwa mnada 25/11/2022, nchini Germany kufuatia mgogoro wa TRC na EUROWAGON Railways Limited (Turkey), iliyopewa kazi ya kukarabati na kutia nakshi. TRC wamelipa Sh. 23 bilioni (35% ya kazi).

Inadaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalçın Aydemir amesema wataanza na mnada wa mabehewa 17 ya awali katika mnada huo (hadi sasa wateja wawili wamepatikana kutoka Serbia), na mabehewa 13 na vichwa 2 vya treni za mwendokasi vitasubiri hadi mteja apatikane na kisha watavipiga mnada.

Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kampuni ya EUROWAGON ya kutoka Turkey ziliingia makubaliano Oktoba 2020 kwa ajili ya ujenzi (ukarabati na utiaji nakshi) wa vichwa viwili vya treni ya umeme na mabehewa 30 ya abiria ambao ulitegemewa kukamilika ifikapo Novemba 2021.

TRC ilisitisha mkataba huo Februari 25, 2022 kwa madai kwamba EUROWAGON wamechelewesha kazi na mazungumzo hayajawahi kuendelea. Kampuni ya RINA ilipewa kazi ya kuthibitisha kazi ya ukarabati na utiaji nakshi mabehewa hayo na kuthibitisha kwamba kazi hiyo imekamilika kwa 50%.

Hivyo EUROWAGON Railways Limited wanataka malipo ya Sh. 10 bilioni, ambayo ni 15% ya kazi iliyothibishwa na RINA kwamba kazi ya ukarabati na utiaji nakshi ilifanyika kwa 50% na malipo ya Sh. 23 bilioni ni kwa ajili ya 35% ya kazi hiyo. Malipo haya yalifanyika Desemba 14, 2020.

Baada ya kuvunja mkataba huo Februari 25, 2022 na EUROWAGON, TRL wakaingia mkataba na kampuni nyingine kwa ajili ya ukarabati wa mabehewa na kutia nakshi. Kampuni hizo ni Zeller KG Engineer (Austria), Baltic Port Service GmbH na Lueckemeir Transport Logistics GmbH (Germany)

EUROWAGON kupitia Mwanasheria Duygu Seda, wakamuandikia barua Mkurugenzi wa TRL kwamba Tanzania Railways Corporation (TRC) wamevunja mkataba kwa njia ambazo siyo halali. TRC walivunja mkataba kwa kigezo cha EUROWAGON kushindwa kuwasilisha Dhamana ya Utendaji (performance Bond)

Mwanasheria wa EUROWAGON, Duygu Seda katika barua hiyo kwa Mkurugenzi wa TRC amemueleza kwamba kutokana na sheria za EU, Germany, Turkey na Austria na makubaliano kati ya EU na Turkey, TRL hawaruhusiwi kufika yalipo mabehewa na vichwa vya SGR wala kusafirisha isipokuwa EUROWAGON.

TRC hawakununua vichwa na mabehewa mapya kwa ajili ya SGR, isipokuwa, EUROWAGON waliopewa zabuni walinunua vichwa 2 na mabehewa 30 kutoka kampuni ya Reli inayomilikiwa na serikali ya Germany, DB Regio, ili kuvikarabati na kuvitia nakshi nakshi, kisha vilisajiliwa kuwa mali ya TRC.

Mkurugenzi Mtendaji wa EUROWAGON, Yalcin Aydemir anasema kwamba TRC walimpa kazi bila dhamana ya Utendaji (Bank/performance guarantee) lakini ghafla TRC wakabadili gia angani na kuidai. Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa anasema EUROWAGON wanatapatapa tu hawana hoja.

TRC June 17, 2022 ilisema imesitisha mkataba na kampuni ya EUROWAGON, iliyokuwa ikitengeneza mabehewa hayo baada ya kushindwa kukamilisha ukarabati vichwa 2 na mabehewa 30 ya abiria, kwa ajili ya majaribio hayo, ni kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk.

Vifaa hivyo kutoka EUROWAGON vilitakiwa kukamilika Novemba, 2021, TRC ilisitisha mkataba na kuwataarifu kwa barua Februari 25, 2022 na kuendelea na kazi ya kukamilisha ukarabati unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka 2022,” alisema mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk

Kwa mujibu wa Tanzania Railways Corporation, taarifa waliyoeleza kwa waandishi wa habari June 15, 2022, walisema Mkataba kati yao na EUROWAGON unaipa TRC haki ya kuchukua jukumu la kukamilisha ukarabati iwapo mzabuni atashindwa kuzingatia masharti ya mkataba.

View attachment 2424063

1. Nimemtafuta Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk, kwanza amethibitisha mabehewa haya ni mapya na sio mitumba, pili mabehewa yaliwasili nchini, ni mabehewa ya mkataba mpya wa mabehewa na Kampuni za Zeller KG Engineer (Austria), Baltic Port Service GmbH na Lueckemeir Transport Logistics GmbH (Germany) na sio yale mabehewa 30 na vichwa 2 vya mkataba uliovunjwa wa EUROWAGON ambao nao waliingia sub contract na walinunua vichwa 2 na mabehewa 30 kutoka kampuni ya Reli inayomilikiwa na serikali ya Germany, DB Regio, ili kuvikarabati na kuvitia nakshi nakshi, kisha vilisajiliwa kuwa mali ya TRC. Mkataba wa EUROWAGON ulivunjwa June 22 vile vichwa na mabehewa tayari yalikuwa ni mali na TRC, Hivyo kitendo cha mzigo kuwasili nchini ni ndani ya miezi 5 tuu!, mzigo wa mabehewa umetua nchini!, hii maana yake ni ama haya ni mabehewa mapya kabisa ya dukani, yaliyokuwa yakisubiri mnunuzi, baada ya kununuliwa kiwandani kabisa South Korea's Sung Shin Rolling Stock Technology Company (SSRST) na yametiwa nakshi nakshi na kuletwa nchini!, ama haya ni yale yale mabehewa mitumba ya EUROWAGON, hivyo hoja za jee mabehewa haya ni mapya ama used, bado zina mantiki!.

2. Ukiyaangalia kwa ndani, mabehewa yaliyowasili jana, yana madirisha pande zote, hivyo huu unaweza kuwa ni uthibitisho mabehewa haya ni mapya, ila yale mabehewa aliyoyakagua Waziri Mkuu kule kiwandani Korea, yana madirisha upande mmoja tuu, hiki ni kuashiria kuwa originally haya ni mabehewa ya underground trains na sio ya terrestrial train!. Sisi SGR yetu ni terrestrial, moja ya faida na raha za kusafiri kwa mabasi na treni ni pamoja na kuenjoy kitu kinachoitwa scenery enjoyment, madirisha makubwa ya abiria kuona nje mazingira.

3. Ule mkataba uliovunjwa, ulikuwa sio mkataba wa kuunda mabehewa, ule ni mkataba wa ukarabati na kutiwa nakshi nakshi kwa vichwa na mabehewa!, na sio kuundwa kwa vichwa na mabehewa mapya!, lakini Waziri Mkuu amezungumzia ujenzi wa mabehewa na sio ukarabati na nakshi nakishi, hivyo mabehewa yaliyowasili ni mabehewa mapya!, kwa nini Watanzania hatuelezwi ukweli tangu mwanzo, hivyo kutoa fursa kwa watu kudhania tumenunua mitumba?.

4. Japo ule mkataba wa EUROWAGON uliovunjwa ulikuwa ni vichwa na mabehewa used, by the time mkataba unavunjwa, hao EUROWAGONS waliisha lipwa malipo ya awali na kuvununua hivyo vichwa na mabehewa 30, ambayo tayari ni mali ya TRC, Watanzania tuna haki ya kuelezwa, hivyo vichwa na mabehewa ya EUROWAGONS, vilinunuliwa wapi, viliundwa lini, wapi?, vimetumika wapi na kwa muda gani kabla TRC hatujauziwa?

5. Watanzania tuelezwe gharama halisi za manunuzi, ukarabati, naksh naksh na usafirishaji mpaka yamepokelewa ili tufanyiwe a comparative analysis, kama tungenunua vichwa vipya na mabehewa mapya, tungetumia gharama kiasi gani, compared na kununua vichwa na mabehewa used ili tujue tumeokoa fedha kiasi gani kwa kununua used?

6. Japo gharama za kununua vitu vipya ni juu ila gharama za maintenance ni ndogo, unaweza kununua kitu used kwa bei poa kumbe ni kitu chakavu sana choka mbaya, hivyo gharama ya maintenance ikawa juu kuliko hata ungenunua kipya!.

7. Sii wengi wanajua kazi ya CAG wakidhani ni kutoa tuu zile ripoti za ukaguzi wa hesabu za serikali, CAG ni Mdhibiti na Mkaguzi, udhibiti unafanywa kabla ya manunuzi, je, kulifanyika tathmini yoyote rail worthiness report ya hivyo vichwa na mabehewa hayo used kabla hayajanunuliwa? Kama haikufanyika, then tusisubiri hadi mradi ukamilike ndipo CAG aikague SGR, baada ya kuanza hizi kelele kelele za mpya vs used, atufanyie a value for money audit, hiki kipande cha Dar- Moro, ili kama tumepigwa, tusiendelee kupigwa mpaka mwisho, tena usikute ni kweli tumeuziwa vichwa na mabehewa used kwa bei ya mapya!, watu wakajivunia viji 10% vyao vya maana tu!, hili litabainika kwenye ripoti ya CAG!.

8. Ukiingia mkataba wa manunuzi, kwa matengenezo, mzigo ukanunuliwa, delivery ndio ikachelewa, huwezi kuvunja mkataba huo ukabaki salama, hivyo kesi ikifunguliwa, Tanzania tunashindwa hata kabla kesi haijaanza!

9. Tulivunja mkataba wa Dowans, wanasheria wetu wakatuhakikishia hatutashitakiwa!, tukashitakiwa!, wanasheria wetu wakatuhakikishia tutashinda!, tukashindwa na tukadaiwa tozo ya Dowans, wanasheria wetu wakatuhakikishia hatutalipa na hawatatufanya lolote!, tena kuna wakajiapisha "over my dead body", hatulipi!
ukweli ni kwa tumelipa every cent kisiri siri bila Watanzania kuelezwa, bila Bunge kujulishwa na kuidhinisha, bila CAG kudhibiti na kukagua!. Kwanini hatuambiwi ukweli?

10 Tulipo vunja mkataba wa Dowans, Zitto akashauri tuitaifishe ile mitambo, waheshimiwa Wabunge wetu wakagoma kuwa Tanzania hatununui mitambo chakavu, mitambo mitumba, na kweli kwa wakati huo hatukuwa na sheria ya kununua mitambo chakavu.

11 Tulivunja mkataba ule wa Dowans kwasababu ya gharama kubwa cha capacity charges na umeme wenyewe!, Mitambo ile Dowans ikanunuliwa na Simbion, tukaingia nao mkataba ule ule wa Dowans!, kwa capacity charge ile ile!, watu wale wale walio ikataa dowams, ndio hao hao danced to the tune na Hilary Clinton kuzindua Simbion!, kwa mkataba ule ule tuliovunja!, kwa gharama zile zile!, na capacity charge ile ile!, na tukawalipa!.

12. JPM alipoingia tukavunja tena na mkataba wa Simbion, tukashitakiwa, tukashindwa, tukadaiwa, JPM akagoma kulipa!, ila baada tuu ya JPM kuitwa kule alipoitwa huku nyuma, sisi hao hao, sio tuu tumelipa!, bali pia tumeinunua ile mitambo ya Simbion kwa bei ya ajabu!, sasa mitambo ile tuliosema ni chakavu, mtumba, na serikali yetu hatununui, mitambo chakavu, sasa ndio tumeinunua!, sasa mitambo ile ya Simbion ni mitambo yetu, ni mali yetu! na malipo yote yaliisha fanyika chap chap fasta fasta!, bila bajeti yake kuombwa popote!, bila Bunge letu kuijadili, kuipitisha na kuidhinisha, bila CAG kuidhinisha malipo hayo!, na haya yote yamefanyika bila sisi Watanzania kuambiwa!, kwanini vitu vikubwa kama hivi hatuambiwi?.

13. Kwa vile mambo kama haya kwenye manunuzi makubwa yaliwahi kutokea kule nyuma kwenye ununuzi wa Rada mtumba toka BAE, watu wakaweka cha juu kikubwa tuu, tukalipa fasta!, Mama Mzalendo wa kizungu, Linda Chalkel akabaini, akatupigania tukarudishiwa chenji ya Rada!.

14. Ununuzi wa ndege ya rais Gulf Stream bei ikapaishwa zaidi mara mbili!, Mzee John Memosa Cheyo akaonyesha bei halisi ya kiwandani! watu wakatia pamba masikioni tukalipa fasta!. Kuna vifaa fulani chakavu vya taasisi fulani nyeti tumeuziwa hapa!, tangu vimenunuliwa havijawahi kutumika mpaka leo!. Hivi naomba nisivizungumzie wala msiniulizie!, maana hata sisi waandishi wa habari haturuhusiwi kuzungumzia mambo ya taasisi fulani fulani nyeti ila fedha zilizotumika sio fedha za taasisi nyeti, ni fedha za Watanzania, kuzungumzia vifaa vya nyeti sio sawa, hivyo hatuvizungumzii, lakini kwa vile tulilipia kwa fedha za Watanzania, hakuna mipaka yoyote ya kuzungumzia matumizi ya fedha za umma!, Watanzania wana haki ya kujua matumizi yote ya kodi zao!.

15. Tukanunua meli fulani moja mtumba iliyochoka, dholfu bin taaban, MV Bagamoyo, ikafanya safari moja tuu ya Dar - Bagamoyo, mahali pa safari ya dakika 30, ilitumia masaa 3!. Hii meli sasa imewekwa kwenye kundi la vifaa vya taasisi nyeti, hairuhusiwi kuzungumziwa hivyo isizungumzwe!, ila fedha zake ni fedha za Watanzania, Watanzania wana haki kujua!.

Hitimisho
Namalizia kwa msisitizo, hakuna ubaya kutumia vitu used!, tena vingine ni vizuri, imara, bora, madhubuti kuliko hata vipya!, na Watanzania walio wengi, kutokana na low purchasing power due to umasikini uliotopea, wengi wetu affordability yetu ni mitumba kuanzia magari, nguo hadi mitambo, hivyo tumezoea, tunachohitaji ni kuambiwa ukweli tuu!,
tutaelewa tuu kuliko... kwenye hili tusubirie ripoti ya CAG ya mwaka 2024!.

Wasalaam.
Paskali.
NB. Makala hizi ni free kutumiwa na gazeti, jarida, mtandao wowote, hazina copyright, ila source na mwandishi wawe attributed.
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo baada ya kampuni ya wahindi kupewa TRC kuiendesha mara waliomba mabehewa makuukuu ya TRC wayanunue kama chuma chakavu. Suala hili lilizua mjadala wa kitaifa, ila likazimwa kiaina.

Sasa hofu yangu isije kuwa ni mabehewa yaleyale yaliyosukumwa kama chuma chakavu tumerudishiwa. Daaaa!
 
Tusilaumu.
Ndugu zangu, watani zangu wasukuma wao kwenye ujanja wa vitu hua hawapo kabisa.
Yaani mkurugenzi wa sehemu akiwa msukuma mtegemee kuletewa vitu vya kishamba hadi mkome.
Angalia wanavovaa kwanza ukikuta msukuma kapiga code za maana za kueleweka basi jiulize mara mbilimbili.
Mabehewa waliyotuagizia wasukuma yametia fora.
IMG_0956.jpg
 
Kwa sisi baadhi yenu, tulioishi nchi za wenzetu, tumepanda treni hizi za kisasa za kasi zinazoendeshwa kwa umeme, bulet trains, ambazo zinakwenda hadi kasi ya speed 160kmh kwa saa!, ila mabehewa ya abiria ya wenzetu tuliyo yapanda, sio kama haya tunayo letewa sisi!, hivyo kwanza natoa hongera sana TRL kwa mabehewa haya.
Ebu tupieni picha basi za hayo mabehewa (mabehewa siyo vichwa) ya huko ughaibuni ili tulinganishe na haya yetu. Naona mnasema maneno na kulalamika tu bila kutuonyesha hayo ya huko! Tuwekeeni tulinganishe.
 
Mambo ya Muhimili uliojichimbia chini sana🤣🤣
Lakini tuulize vizuri, inawezekana ni mabehewa ya reli ya TAZARA!!
maana ata ripoti ya Precision Air ya jqna wamesema siyo halisi ilihali vyombo vya habari vimeripoti!!?
 
SGR ni daraja la kati la Treni ziendazo kasi!
Fastest train inakwenda 360KMH.
Nadhani iko elimu zaidi ya kutambua hizi technologies..
Na zile Behewa ziko ktka madaraja mbalimbali...
Nakumbuka PM alisema zile behewa ni Daraja la 3...
Halafu singe piece cabin haliwezi kutoa taswira ya muonekano wa Train nzima pamoja na Kichwa chake....
Picha zitatutoa Roho...
 
Umejaribu kumuuliza rolu modo wako kuhusu no 12?
Kwa yanayoendelea sasa nna uhakika wa 99.999% Chuma hakikulala kwa mapenzi ya yake...ht km ni kugawana mirathi sio kwa style hii..and the bad thing ht tuliokua tunawategemea walisemee hii wame mute, wanalamba tu asali kiroho mbaya.
 
Back
Top Bottom