Ah.. Sijui wenzangu...ila kwa sisi tuliowahi kutumia usafiri huu tuli-enjoy sana!!

gambachovu

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
1,854
292
Usafiri wa treni...

Ah... Tuliowahi tukumbushane,mabehewa marefu kama nyoka,hekaheka za ma-TT, mambo ya "buffet car",enhe...

Tukumbushane jamani..
 
Ni usafiri mzuri.Kwa wale wa reli ya kati wanakumbuka pale Singida sehemu inaitwa Salenda(sijui ndo matmshi yake sahihi),kuna nyama za kutosha pale.
 
panaitwa Salanda mkuu.. Pale ni balaa kwa nyama za mishkaki na kukaanga.. Vipi matairi yake yanavyonguruma,na honi yake..
 
Dah, umenikumbusha mbali sana.

Ukikaa 3rd class ukinyanyua mguu, kuurudisha chini utajibeba.
Salanda, kuku alikuwa na paja kubwa kama la paa
Buffet, ndo kulikuwa wanakaa wajanja na wenye pesa, kibinti kikijipisha pitisha pale ama zake ama za mapedeshee wa kwenye treni.
 
Umenirudisha mbali mkuu, nilikua nasoma Shy, tukifunga Shule nyumbani Dar, ilikua kizazaa iko trip tulikaa chooni tena kwa kusimama frm Shy to Tbr (Mboka)
gogo likifika Mboka saa 12 asubuhi hamuondoki hadi gogo la Mpanda lifike,
na wakati ule ilikua haikawii kusikia ya kutoka Mpanda sijui reli imefanyaje!
Gari ya kutoka Mwz unakuta inashinda Tbr station hadi jioni, na Tbr ndy palikua pakiongoza kwa wizi,
nakumbuka foleni ya kununua Chai Tbr.
Nakumbuka Ma-TT walivyokua wakiamsha watu "abiria amkeni Tbr hapa muangalie wezi"
nakumbuka unawezakua umelala chumbani, bila kuangalia nje ukisikia tu, treni imesimama ukajua uko station gani kw kusikia tu kelele za wafanyabiashara nje !
"hayaa hayaa vitunguu"
unajua hapa kama sio Kimamba basi Kidete. N.k
 
Nakumbuka nililala dom siku 3 nikisubir treni ije tuunge hadi mwanza. Tulinyeshewa mvua, tukapigwa baridi steshen huku steshen masta akitangaza, "gar la abiria toka pwani kuelekea bara liko njian, tunawaomba abiria kua wavumilivu". Halaf nilikua nimekata daraja la kajamba nani, wewee! Nilifika mwanza hoooi bin taaban kwa uchovu.
 
Buffet Konnie palikuwa poa sana.. Na kuna wajanja waiokuwa na tiketi wanaongea na TT wanampa mshiko,wanakaa buffet..
Kuku wa Salanda kuna wakati tulikuwa tunawaogopa kama kuku wa Uwanja wa fisi..
3rd class noma!
Watu mnabanana kama mochware ya Muhimbili zamani...
 
Umenirudisha mbali mkuu, nilikua nasoma Shy, tukifunga Shule nyumbani Dar, ilikua kizazaa iko trip tulikaa chooni tena kwa kusimama frm Shy to Tbr (Mboka)
gogo likifika Mboka saa 12 asubuhi hamuondoki hadi gogo la Mpanda lifike,
na wakati ule ilikua haikawii kusikia ya kutoka Mpanda sijui reli imefanyaje!
Gari ya kutoka Mwz unakuta inashinda Tbr station hadi jioni, na Tbr ndy palikua pakiongoza kwa wizi,
nakumbuka foleni ya kununua Chai Tbr.
Nakumbuka Ma-TT walivyokua wakiamsha watu "abiria amkeni Tbr hapa muangalie wezi"
nakumbuka unawezakua umelala chumbani, bila kuangalia nje ukisikia tu, treni imesimama ukajua uko station gani kw kusikia tu kelele za wafanyabiashara nje !
"hayaa hayaa vitunguu"
unajua hapa kama sio Kimamba basi Kidete. N.k

Tabora kama unatokea Dar unaingia usiku vile? Dodoma saa nne asubuhi..

Na lile la Mpanda kweli lilikuwa haliaminiki..bovubovu,na kipondi kile tulikuwa tunaambiwa nchi yetu changa tunaamini,wala hatuhojisana wala kuilaumu serikali

Ma TT wanakagua tiketi usiku kwani ni vigumu kuwatoroka..
Ma TT wengine walikuwa wakorofi hadi wanajulikana.. "Leo yuko TT fulani..."
 
Nakumbuka nililala dom siku 3 nikisubir treni ije tuunge hadi mwanza. Tulinyeshewa mvua, tukapigwa baridi steshen huku steshen masta akitangaza, "gar la abiria toka pwani kuelekea bara liko njian, tunawaomba abiria kua wavumilivu". Halaf nilikua nimekata daraja la kajamba nani, wewee! Nilifika mwanza hoooi bin taaban kwa uchovu.

Yaani we acha tu..

Ila sisahau kwa wale waliowahi kulala Second,na First vyumba vile ni vizuri na unaenjoy mle ndani,na safari haichoshi

Panakuwa kama kwenu...mara mkakae mahali mpige stori,mara muagane kwenda kupumzika,mara kwenda chooni,mara kuagana na kwenda kulala,mara asubuhi miswaki,dah mambo mengi kwa kweli..
 
Nataman siku nikibahatika kupanda tren sijawahi tangu kuzaliwa lol!

La siku hizi wala hautaenjoy.. Enzi zile kabla ya ajali za mara kwa mara,ndiyo ilikuwa raha tupu! Kuna waliobefriend kupitia treni,yaani ilikuwa raha sana tu kiufupi Cantalisia!
 
Umenirudisha mbali mkuu, nilikua nasoma Shy, tukifunga Shule nyumbani Dar, ilikua kizazaa iko trip tulikaa chooni tena kwa kusimama frm Shy to Tbr (Mboka)
gogo likifika Mboka saa 12 asubuhi hamuondoki hadi gogo la Mpanda lifike,
na wakati ule ilikua haikawii kusikia ya kutoka Mpanda sijui reli imefanyaje!
Gari ya kutoka Mwz unakuta inashinda Tbr station hadi jioni, na Tbr ndy palikua pakiongoza kwa wizi,
nakumbuka foleni ya kununua Chai Tbr.
Nakumbuka Ma-TT walivyokua wakiamsha watu "abiria amkeni Tbr hapa muangalie wezi"
nakumbuka unawezakua umelala chumbani, bila kuangalia nje ukisikia tu, treni imesimama ukajua uko station gani kw kusikia tu kelele za wafanyabiashara nje !
"hayaa hayaa vitunguu"
unajua hapa kama sio Kimamba basi Kidete. N.k

tena kuna wadada wauza chai walikuwa wanasema aa chai ya maziwa ya rangi aaaa chai..
 
Tabora kama unatokea Dar unaingia usiku vile? Dodoma saa nne asubuhi..

Na lile la Mpanda kweli lilikuwa haliaminiki..bovubovu,na kipondi kile tulikuwa tunaambiwa nchi yetu changa tunaamini,wala hatuhojisana wala kuilaumu serikali

Ma TT wanakagua tiketi usiku kwani ni vigumu kuwatoroka..
Ma TT wengine walikuwa wakorofi hadi wanajulikana.. "Leo yuko TT fulani..."

Baadhi ya MaTT maarufu nawakumbuka
Lumami RIP (ambae badae alikua mw/kiti Simba s.c) Teko RIP
King'ombe RIP
Kilinda yuko hai
 
tena kuna wadada wauza chai walikuwa wanasema aa chai ya maziwa ya rangi aaaa chai..

Na kweli ujasiriamali wa kipindi kile jamani,we acha tu!

I miss kile chombo kwa sana..

Mnakutana hadi watu mliopoteana muda mrefu,mnaungana hata na kufahamiana na watu wapya,it was fun pia..
 
Kamanda miye umekumbusha machungu na raha, machungu ni msiba wa baba yangu mdogo ambaye alikuw akifanya kazi stesheni Tabora, nilikuwa sipandi kajamba nani, nimeshuka sana daraja la pili, nilikuwa sijui kabisa adha za daraja la tatu wakati nikitoka Dar kwenda shule ya Uyui pale Tabora, raha nakumbuka nilipata mademu wawili mmoja wa Kigoma alikuwa akiitwa Kidifa.... sijui yuko wapi na mwingine Mchaga alikuwa akiitwa Haika.... hata huyu sijui yuko wapi. Treni ulikuwa bonge la usafari jamani.
 
Nakumbuka mkifika Korogwe mnabadilisha mabehewa yale ya kwenda tanga na ya kuelekea Moshi yanaunganishwa na kuendelea na safari!!
 
Back
Top Bottom