Afisa uhamiaji Mwanza anusurika kuuawa kwa risasi na polisi

AFISA wa Uhamiaji ofisi ya Mkoa wa Mwanza Albert Buchafwe amenusurika kuuawa kwa risasi baada ya kushambuliwa na Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Polisi Nyakato, Abubakar Zebo kwa madai kuwa walikuwa wakishambulia jambazi. Tukio hilo ambalo limethibitishwa na kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow linadaiwa kutokea majira ya saa 4: 13 usiku wakati afisa huyo wa uhamiaji akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake ambapo alikutana na gari dogo aina ya Suzuki lililomuashia taa likimuashiria kusimama.

Akielezea mkasa kamili Buchafwe alisema kwamba baada ya kuwashiwa alipochunguza kwa makini gari hilo aliweza kulibaini kuwa ni lile linalotumika na afisa huyo wa Polisi, hivyo alisimama na kujitambulisha kwake akiwa ndani ya gari lakini aliamuriwa kuzima taa za gari lake na kutoka ndani yake.

"Nilitii nikazima taa, lakini nilisita kutoka katika gari langu, nilijitambulisha kwamba mimi ni afisa Uhamiaji na kumtaja jina afisa huyo, ambaye aliendelea kunilazimisha kushuka ndani ya gari huku nikiona akijiweka sawa ikiwa ni pamoja na kuandaa Bastora yake tayari kwa kushambulia," alieleza. Alisema wakati bado akijitambulisha alishuka askari aliyekuwa na sale katika gari hilo la afisa huyo wa polisi akiwa na silaha ya SGM hali ambayo ilimlazimu kugeuza gari haraka na kukimbia huku gari lake likishambuliwa nyuma kwa risasi.

"Gari langu limeshambuliwa kwa risasi zaidi ya tano, moja imetoboa upande wa mbele karibu na Taili ya kulia, risasi tatu zimetoboa nyuma ya gari na moja ubavuni mwa gari upande wa nyuma, lakini sikuweza kupata madhara hali ambayo ilinilazimu kukimbia hadi ofisini kwangu na kutoa taarifa kwa bosi wangu wa mkoa usiku huo," alizidi kufafanua.

Buchafwe alisema amepatwa na mashaka na tukio hilo kutokana na asakri huyo aliyehusika kuwa na mahusiano ya karibu na mkewe ambaye wamekuwa na ugomvi naye pamoja na kesi ya kutalikiana mahakamani na kusema kwamba huenda ahalikuwa la bahati mbaya.

"Nina kesi na mke wangu mahakamani, na afisia huyu wa polisi amekuwa na mahusiano ya karibu na mke wangu huyu ambaye tunashitakiana mahakamani, inanishangaza kwamba mtu ambaye ananifahamu licha ya kujitambulisha bado alikuwa akishilikilia msimamo wa kunitaka kushuka, nadhani hapa kuna jambo zaidi ya hali ilivyo," alieleza.

Aidha akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza alikiri kuwapo kwake na kudai kwamba anayo hakika kwamba tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya kwani jeshi lake lilipata taarifa za Kiinterejensia za kuwapo kwa majambazi wakidaiwa kutumia gari sawa na ambalo afisa huyo wa uhamiaji alikuwa nalo.

"Hili ni tukio la bahati mbaya, jeshi laetu lilipata taarifa za Kiinterejensia juu ya kuwapo kwa majambazi na kuamua kuweka mtego, sasa afisa huyu alifika muda na wakati ambao askari wetu walikuwa eneo hilo na kuingia katika mtego wetu, alikuja na gari ambalo ni sawa na lile ambalo tulielezwa kuwa lingetumika, lakini bahati nzuri mauaji hayakutokea," alifafanua kamanda huyo.

Kamanda Barlow amedai kwamba kutokana na tukio hilo amepanga kukutana na afisa huyo wa uhamiaji na kuzungumza naye akiwa na askari wake kutafuta suluhu ya jambo hilo ambalo aliekeza kwamba yeye anaamini limetokana na bahati mbaya.
 
wauaji wakubwa haooo....bahati mbaya hata baada ya mtu kujitambulisha jamaa alitaka amuue alafu mke abaki na mali zote za mshkaji then wanakula raha.....!
 
Uzembe wa namna hii haukubaliki na hasa kufanywa na watu tunaoamini ni walinzi wetu! Hakuna cha suluhu hapo bali hatua za kinidhamu lazima zichukuliwe!
 
Huyu Mke wa jamaa ajiangalie vizuri. Akishafunga Ndoa na huyu POLISI, basi na yeye ATAULIWA.

Wewe mama, kimbia haraka sana maana ukishaanza kucheza na wauwaji, na wewe watakuuwa tu.

Kama kuna ndugu au jamaa wa huyu mama, mwambieni heri abaki na mumewe kuliko huyo Polisi.
 
Sasa kidoogo naanza kuwaelewa CHADEMA
Huu ni upumbavu wa hali ya juu unaofanywa na polisi

Hivi nikikamatwa na polisi haki zangu ni zipi?? Naomba kujua
 
Kweli Tz ni zaidi ya maajabu kila kukicha haviishi vioja
yaani hapa ni kwere
 
Wataua raia kwa maksudi kwa kisingizio kuwa ni majanmbazi wakidai inatokana na "intelligentsia" ya polisi. Huu ni upuuzi mtupu.
 
Hv hawa polisi akili zao zinakwenda wapi pale wanapotekeleza MAUAJI ya raia wasiokuwa na hatia.
 
ukweli maauji mengi sana ya watu wanaosemekana ni majambazi huwa nayo mashaka sana maana hawa jamaa huwa hata wa kisa cha mahawala wanaweza kusingizia ni jamabazi kweli tanzania tutashangaa mengi sana
 
Laana za namna hii watawala mtaziweka wapi!!!? Yaani mtu anatumia cheo chake kuua kwasababu ya K!!! Duh!!
 
Aidha akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza alikiri kuwapo kwake na kudai kwamba anayo hakika kwamba tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya kwani jeshi lake lilipata taarifa za Kiinterejensia za kuwapo kwa majambazi wakidaiwa kutumia gari sawa na ambalo afisa huyo wa uhamiaji alikuwa nalo.


Hivi mtu anaweza kufikia cheo cha kuwa RPC halafu malalamiko ya namna hii ya jaribio la kuua linachukulia rahisi rahisi hivi eti kwa kusema "nina hakika???" Unaweza kuwa na hakika ya taarifa hizo za kiinteligensia lakini huna hakika kuwa huwenda zilikuwa zumepikwa na huyo askari wako wa chini. Je ulijua kuwa huyo alskari alikuwa na ugomvi na afisa wa uhamiaji Buchafwe ambaye naye ni askari?

Kamanda wa Mkoa aliyeiva kazini angefanya uchunguzi (independent) kabla hata ya kufikia azimio uchwara kuwa ataongea nao utafikiri ilikuwa ni kesi ya kusutana ya wizi wa kitenge wakati kuna watu walikuwa wamefyatua risasi kuelekeza kwa mwanadamu mwenzao. Hata kama ni mtego sasa kwanini wao wasingemfuata tu mpaka mwisho wake waone ni nani maana yeye hakuwajibu kwa kuwafyatulia risasi?

Mimi Obudsman ningeanza na huyo Barlow aletwe mbele ya red Capet kwa mwendo wa ndege aulizwe maswali ya mazito tupate maelezo yake na uwezo wake wa kutatua na kupambanua mambo tuujue. Wakati huo huyo Zebo na yeyote aliye fyatua risasi wako Maabusu ya kipolisi akisubiri hukumu yake.

Hili ni jambo serious sana kwani:

1. Binadamu asiye na hatia ametaka kuuwawa kwa risasi, kisaikolojia ameumizwa sana na anaweza kushindwa kufanya kazi zake na hata kutembea hapo Mwanza akihofia hicho kikundi cha kumchukulia mkewe na pia kutaka kumtoa roho

2. Askari wa Uhamiaji anata kuuawa na askari wa Polisi na anatetewa na RPC wake. Kwahiyo Mkuu wa Uhamiaji Mkoa na Maafisa wote wa Uhamiaji wanaweza kutangaza uhasama na vita kila wanapokutana je kutakalika Mwanza?

3. Kila mara tunajadili hapa mauaji ya raia na tunatoa maelezo. Je kulikuwa na ulazima gani kufyatua risasi wakati mtuhumiwa hajasababisha hatari yeyote? haya ni matumizi ya nguvu isiyo ya lazima. Amejitambulisha ni afisa wa uhamiaji, muulize kiongozi wako ni nani, tupe namba yake n.k wangeweza hata kumpigia simu bosi wa uhamiaji au kumsindikiza kwenda nyumbani kwake kuona kama si jambazi waliyemdhani.

Viongozi wazembe nchini Tanzania sasa hamuwezi kuendelea kujificha chini ya kivuli cha 'taarifa za kiiteligensia' wala "kwa mujibu wa kutoingilia shughuli za kimahakama'; tunawatafuta popote mlipo na kuwafukuza kazi na kuwafungulia mashitaka.
 
Aise mkuu wa uhamiaji peleka swala lako haki za binadamu ungeshuka wangekumaliza kama walivyommaliza Kombe!!
 
OMBUDSMAN Kila siku tunasema hapa jeshi la Polisi chini ya Said Mwema ni kichaka cha wahalifu, wala rushwa na wabambikiza kesi. Ona sasa jamaa angekufa tungeambiwa walidhani jambazi kumbe kuhalalisha wamuue wabakie na mkewe. Kuna mtu hapa alitilia mashaka hata majambazi watano waliouawa Arusha
 
Last edited by a moderator:
Hivi nini maana ya Intelijensia?!! kwamba unapata clue na unachunguza kwa hakika na kijiridhisha ndio unachukua hatua!! what if wangemuua?!! hawa Polisi wajinga sana na wanabebana hata kwa vitu vya wazi na kweli..shame
 
Hakuna mambo ya intelijinsia......huo ni ushuzi mtupu. Hivi Tanzania hakuna sheria ambayo inaruhusu taarifa za intelijinsia kuwekwa mbele ya mahakama kama ushahidi? Kunatakiwa kiwepo chombo cha kupitia hizi classified info kama ushahidi unatakiwa mbele ya sheria.Kila kitu ooh taarifa za intelijinsia. Yani jeshi limegeuka kuwa kikundi cha ngonjera na taarabu.

Mwakyembe aliwahi kuelezea in details maandalizi ya yeye kuuawa lakini polisi hakushughulikia taarifa zake. Leo hii watu wanaingilia ndoa za wengine, mnawatafuta kuwaua ili muendelee kutanua na wake zao. This is very shame kwa jeshi la polisi.
 
polisi wa tanzania wanachofundishwa ni kuua tu vijisababu vyao taarifa za kiinteligensia.
 
Walipanga kumuua,jamaa asikubali suluhu,inakuwaje mtu anajisalimisha then anajitambulisha bado unamng'ang'ania.jamaa achukue hatua dhidi ya wauaji hao wala haiitajiki tume ya suluhu hapo.hiyo ni miuaji tu siku hizi nikiiona hiyo mijitu natamani kuipiga mawe tu ife bora tujilinde wenyewe.NOSENSE!!!
 
Ndo maana siji kwenye hili jukwaa maana unaweza kutukana na mwishowe ukala ban
Taarifa za kiitelijensia mtu amejitambulisha kwako na amekuita na jina kwamba wewe fulani nakufaham bado unamwambia ashuke kwenye gari ili umfanye nini
Na kwa nini ajitambulishe na kukutambua na bado unajiandaa kutoa bastola yako wakati ashakuambia yeye ni nani na wewe ni nani
na yule askari mwingine alishuka lili akamfanyeje huyo afisa uhamiaji
Na je baada ya kukimbia walifanya nini kuhaklikisha kuwa sio yule jambazi waliyekuwa wanamfuatilia
Mbona hawakukimbiza gari mpaka wakahakikisha huyo waliyedhania ni jambazi mpaka wamkamate au waone ameingia wapi au baada ya kujua wamemkosahawakuwa na haja nae tena maana issue ishaingia nuksi
Na kamanda wa polisi anasupport ujinga na uhuni kama huu kumtetea polisi mwenzake
Tuliamini muda huu wakati anatoa mapovu ya ujinga wake huyo kamanda mwenzake awe mahabusu ndipo aje aongee ujinga wake huo
Je angeuwawa huyo kamanda angesema kuwa alifananishwa na jambazi au tungeambiwa story ya kutunga kwamba afisa uhamiaji alijaribu kukataa amri halali ya kukamatwa ndipo akapigwa risasi au tutaambiwa alifananishwa na jambazi lililokuwa linatafutwa
 
......."Hili ni tukio la bahati mbaya, jeshi laetu lilipata taarifa za Kiinterejensia juu ya kuwapo kwa majambazi na kuamua kuweka mtego, sasa afisa huyu alifika muda na wakati ambao askari wetu walikuwa eneo hilo na kuingia katika mtego wetu, alikuja na gari ambalo ni sawa na lile ambalo tulielezwa kuwa lingetumika, lakini bahati nzuri mauaji hayakutokea," alifafanua kamanda huyo....
PAMBAF intelijensia!! Intelijensia!! intelijensia ya kuua raia wema tu!! Plain stupidity!! mburuze huyu mpuuzi kwa pilato!! haya majambazi yanayoitwa polisi yatatumaliza. Intelijensia imeua Arusha, imeua Mwanza, imeua Iringa!!
 
Back
Top Bottom