Afande Sele amchana Kikwete kavukavu!

Mimi ni mmoja wa watu wanaodharau wanamuziki wa bongofleva hasa pale wanapomkatikia kiuno Mkwere hasa kwenye matukio ya uchaguzi. Naona mambo yanaanza kubadilika. Alianza Sugu na Mkoloni. Safari hii Selemani Msindi, narudia tena SULEMAN amenukuliwa akisema yafuatayo dhidi ya Kikwete:

Anajenga makundi ya chuki na uhasama katika kila sekta kuanzia kwenye chama chake, serikali yake na sasa kwenye sanaa na haswa mziki wetu ambao ndio amekuwa akijinadi kuusaidia kumbe katika hii awamu yake ndio mziki umepotea mwelekeo. Sasa kama anasema studio aliwapa waliomuomba mbona mimi na watu wengine wenye misimamo tulikuwepo siku ile alipoahidi studio hatujui lolote na hatujaonyeshwa hiyo studio?" [/SIZE][/FONT][/I]

Source: BONGO STAR LINK

"Ah, huyu JK kwa tamko lake hili kuhusu studio aliyowapa THT na Ruge anaonyesha jinsi gani asivyo kiongozi makini na kwa mtazamo halisi anaonyesha ni jinsi gani hakustahili kuwa mkuu wa nchi.

Masikini Sele! Anakumbuka shuka wakati ndio kumekucha? Pole sana. Mliyemsifia ndiye huyo ndugu yangu. Anajua hana kipindi kingine baada ya hapa na kwa hivyo anaonyesha makucha yake kweupeeee! Mwanaume anapotafuta mchumba humchunguza sana anayemuwania pasipo muwaniwa mwenyewe kujua kama anachambuliwa. Lakini akishajionyesha na kuchunguzwa yeye ndipo huficha makucha yake yasionwe. Ngoja muanze kuishi pamoja, kila kucha na urefu wake utalijua! Kwa sababu hata konda huwajali abiria walioko nje ya bus lake na sio walioko ndani ya bus tayari. Ukibisha omba msaada kushushwa kona ilee! Utaambulia matusi na dharau "Hii sio baiskeli bwana, sishushi pale" Lakini akimwona abiria anakuja kwenye kona utasikia konda anaita "Kichwa babu punguza mwendo; Ukakwenda? Mpe mchuma juu kwa juu"
 
Labda mngemsikiliza tena maana mmekazania hapo kwenye mzalendo kama jakaya. kwingine kamchana pia

Last edited by a moderator:
Kwa nini watu wengi tunasilika ya kuto-akcnowledge failures zetu - na mara nying tunasukumia wengine. Dhambi ya Adamu na Eve inatuumiza sana. Ni nyoka ndiye kanidanganya (Eve) ; ni huyu mwanamke ndiye kanipa tunda(Adam).

Sasa JK kashindwa uongozi- anasema eti sababu yeye ni mslimu ( wakati tunda la ufisadi amekula yeye kwa roho yake nyeupe). Tubu ni njia salama sana na kuacha kutenda maovu tena
Banned
 
Mzalendo kama Jakaya hadi anaondoka Ikulu hajasomesha mtoto Ulaya",nakumbuka kibao chake msanii huyu cha kumpamba JK na leo hii anakuja kulalamika baada ya kutoswa![/QUOTE]

Ni kama mambo ya bendi tu unatoa buku ten, unatajwa jina mwanzo-mwisho!
 
Tangu alipotoroka Monduli jeshini......jk bado hajabadilika.....fitina na uchonganishi viko pale pale.....
 
Mimi ni mmoja wa watu wanaodharau wanamuziki wa bongofleva hasa pale wanapomkatikia kiuno Mkwere hasa kwenye matukio ya uchaguzi. Naona mambo yanaanza kubadilika. Alianza Sugu na Mkoloni. Safari hii Selemani Msindi, narudia tena SULEMAN amenukuliwa akisema yafuatayo dhidi ya Kikwete:

"Ah, huyu JK kwa tamko lake hili kuhusu studio aliyowapa THT na Ruge anaonyesha jinsi gani asivyo kiongozi makini na kwa mtazamo halisi anaonyesha ni jinsi gani hakustahili kuwa mkuu wa nchi.

Anajenga makundi ya chuki na uhasama katika kila sekta kuanzia kwenye chama chake, serikali yake na sasa kwenye sanaa na haswa mziki wetu ambao ndio amekuwa akijinadi kuusaidia kumbe katika hii awamu yake ndio mziki umepotea mwelekeo. Sasa kama anasema studio aliwapa waliomuomba mbona mimi na watu wengine wenye misimamo tulikuwepo siku ile alipoahidi studio hatujui lolote na hatujaonyeshwa hiyo studio?"

Source: BONGO STAR LINK

Yeyote wa kumsikiliza JK au kumpenda, iwe kutoka ktk ulingo wa Siasa, Sanaa, Dini...Elimu au tasnia yoyote, huyo ni hamnazo au anahitaji huduma ya haraka ya KIKOMBE KWA BABU -wa Loliondo maana JK hana neno lolote linalotoa dira na mwelekeo katika hizo nyanja zilizotajwa juu sembuse na sembuse na kupambana na ufisadi ambayo ndio kwaanza imemuwia kama kazi toka sayari nyingine....hawezi kuleta jema, ni mgawanyaji na mtengeneza makundi, ya dini, siasa na ktk nyanja nyingine....ni shida tupu!

Mmesahau kuwa Ruge anamiliki studio iliyokuwa inampigia debe? Akina Kibonde si wapo pale? na wa-chokoraa wengine wamejaa kama kampani ya Ruge?...JK amewafavour kundi lake...analijua yeye!
 
kiukweli afande sele ni mwenye hekima kama alivokuwa mfalme suleimani, ila kwa siku hizi naona amekuwa akitumia sana bangi hivi amekuwa akiongea pumba... Ila akiwa kama ujatumia na akili zake za ukweli zipo basi afande sele uwa anaongea hekima na busara kama hizo.

Cha muhimu kama kuna mtu wakumpa ushauri mzito basi tuakuwa na mtu mzuri zaidi apa tanzania...
 
ha ha ha ha................. umenikumbusha hili mkuu na sitaki kuamini kuwa huu ndo wakati muafaka wa Afande kuamka na kuona kwamba yule aliyemsifia hakustahili kuwa rais wa nchi!!! N way hujachelewa mkuu karibu vitani

Wakati hajaonyesha haya ya sasa. Wakati watoto wake walikuwa wanasoma St. Patrick Trust ya Arusha, sasa ameshawavusha ng'ambo. Wakati huo alikuwa ndiyo ameanza watu walimwona mkombozi!!! sasa watu wanaona na kujiuliza ilkuwa kiini macho? Walimpamba na kumpa nafasi ya kutekeleza lakini haijawezekana! Sasa inabidi waseme wenyewe!! Hakuna mtu aliyemwambia aahidi hata kama haitatekelezeka!!!
 
funguka kaka Afande kwani huyu mtu sio wa kumtarajia hata kidogo hata hao waliopewa wenyewe watakuja kujuta siku moja......
 
Mwenye macho haambiwi tazama, afande SELE umenena hata sisi tunalalamika kila leo kuwa huyu mkuu wa nchi ni mtu wa makundi na chuki, leo tena kamtuma sheikh mkuu kuwachonganisha watanzania kwa kutumia kichaka cha udini.TUMEKWISHA

Hiyo studio ya kisasa JK aliowaahidi wanabongo flavor haijakamilika?
 
uzuri wa mungu hapendi wanafki, malipo ni hapa hapa. kwanza mimi hawa nataka waishi kwa kutegemea maconcert tu lakini sio kuuza cd zao, kwa jinsi walivyo wapuuzi mimi nadowload manyimbo yao ya kipuuzi na nazigawa bure kabisa, mbwa hawa.

Saigon, Sikufahamu hunifahamu lakini ukweli tuuseme: hivi kuleza maoni yako bila kutoa matusi haiwezekani? Hivi unapata raha gani unapomtukana mtu aliyetumia haki yake ya kutumia jamvi hili kutoa maoni yake? Labda humtukani aliyeleta mada, lakini unafurahishwa namna gani unapowaita hao wasanii mbwa? Mpendwa lugha za namna hiyo si nzuri!
 
Mimi ni mmoja wa watu wanaodharau wanamuziki wa bongofleva hasa pale wanapomkatikia kiuno Mkwere hasa kwenye matukio ya uchaguzi. Naona mambo yanaanza kubadilika. Alianza Sugu na Mkoloni. Safari hii Selemani Msindi, narudia tena SULEMAN amenukuliwa akisema yafuatayo dhidi ya Kikwete:

"Ah, huyu JK kwa tamko lake hili kuhusu studio aliyowapa THT na Ruge anaonyesha jinsi gani asivyo kiongozi makini na kwa mtazamo halisi anaonyesha ni jinsi gani hakustahili kuwa mkuu wa nchi.

Anajenga makundi ya chuki na uhasama katika kila sekta kuanzia kwenye chama chake, serikali yake na sasa kwenye sanaa na haswa mziki wetu ambao ndio amekuwa akijinadi kuusaidia kumbe katika hii awamu yake ndio mziki umepotea mwelekeo. Sasa kama anasema studio aliwapa waliomuomba mbona mimi na watu wengine wenye misimamo tulikuwepo siku ile alipoahidi studio hatujui lolote na hatujaonyeshwa hiyo studio?"

Source: BONGO STAR LINK

Afande Sele kweli mlevi ana acha kuongea mambo ya msingi ana zungumzia studio
 
Hivi mtu aliyechanika anawezaje kumchana alivevaa??
Huyo hata kwao morogoro hivi sasa hana thamani kutokana na vituko vyake hasa baada ya kula mjani.
Na alijidharaulisha sana pale alipomfukuza mwandani wake ambaye wengi tulifikiri kuwa ni mkewe kwa madai kuwa anatembea na marafiki zake.
Wanamorogoro hawana kichaa cha kumpatia kura zao ili awe mbunge wao.
Ushauri wangu ni kuwa aendelee kula mjani lakini ahakikishe polisi hawamkamati maana asije akajidai kuwa ni kwa sababu za kisiasa wakati sababu ni kukutwa na mjani mfukoni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom