Uchaguzi 2020 Adam Mchomvu ampiga mtama Emmanuel Mbasha stejini kwenye tamasha la CCM uwanja wa Uhuru

Usisahau pia aliyepiga aliomba msamaha na kusema angekuwa na uwezo angewashawishi wananchi kumchangia Magufuli pesa za vacation.

Akajikalie huko yeye ampigie kampeni tu akija endelee na kazi yake.
Mkuu umechangia kama mtu aliyekimbia umande.

Umesahau kuhusu mambo ya kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Mkuu umechangia kama mtu aliyekimbia umande.

Umesahau kuhusu mambo ya kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
Sio kwamba umemuelewa Mchomvu tofauti na nilivyomwelewa mkuu?

Kwanini ufikiri sasa mimi ndiyo nilikimbia umande na sio wewe.
 
Unaweza ukamlazimisha binaadamu kumfikisha kwa nguvu unakotaka nautafanikiwa kumfikisha kimwili lakini sio kifikra,,.
 
Hiki ndicho kinachotuuma wanaccm. Kwamba aliyepiga hajavaa hata nembo ya CCM na aliyepigwa katupia full CCM.

Mbaya zaidi aliyepiga alikiri hadharani kuwa hakumpigia Rais Magufuli kura mwaka 2015. Inauma sana jamani. Yani tukifungua kila "engo" tunakutana tu na topics za mitama!

Yani tumelipa Tshs milioni 800! Mapato yote yaliyokusanywa kutoka kwa watia nia tumeenda kutupa pale taifa kisha jamaa anachukua points tatu na magoli yote 200! Hapana!
Alikuwa kavaa za chadema.
 
Mbasha hii ni laana ya kuchanganya jina la Mungu na utopolo wa ccm. Ona sasa mzigo wako Flora watu wanachapa, wewe nawe unachapwa mitama!
 
Wasanii wangapi wamechafuka kwa kuambiwa wanavuta bangi??? Bangi ni sehemu ya vifaa vya kazi vya wasanii wengi! Na wasanii na entertainers wengi wanavuta bangi na wanajulikana na hawajawahi kushuka umaarufu kisa wamefichuliwa wanavuta bangi. Hata hivyo kimjini mjini The term "bangi sana" ninavyoelewa haimaanishi mtu anavuta bangi, humaanisha MKALI sana au ANA VITUKO SANA . Huyo Mchomvu atakuwa mshamba na akili zake zina mapungufu. Mtu mzima kumpiga teke au ngumi mtu mzima mwenzako ni wazi ni mshamba na mjinga

Mimi na wewe tunaweza tukawa waelewa wa hayo maneno "Bangi Sana" vipi wale wasioelea? Wale wanaotafsiri moja kwa moja? All and all haikuwa sahihi kuongea yale maneno kwenye umati wa watu tena Tanzania nzima walikua wanaangalia.
 
tunachosahau wasanii Hawaji bure kwa mapenzi yao, wao wamekuja kikazi na kimaslahi ,Hapo waandaji wamepiga pesa na ikiwezekana PCCB itupie jicho.
Msimu wa kupiga pesa huu.2015 wapo waliojenga nyumba na hawakuwahi tarajia hivyo kipato.
baada tu yakampeni
 
Matumizi mabaya na neno mtama Mtama gani huo yani unamshtukiza mtu na mtama tena uko nyuma yake bado anapata nafasi ya kushika chini ilitakiwa wakamuokote kwenye maspika kule
 
Ni ishara ya kiroho ya kipigo kinachokuja kuipata CCM October, chadema watumie ishara ya mtama katika kampeni zao kama kibwagizo
Piga mtama! Mtama1, mtama 2, mtama 3. Wananchi mumeonaaaaa? Tena Lissu atapiga mtama kwa mguu ulio mbovu jinsi mpinzani wake alivyo dhaifu!
 
Ni ishara ya kiroho ya kipigo kinachokuja kuipata CCM October, chadema watumie ishara ya mtama katika kampeni zao kama kibwagizo
Mtama kama Tendo, au mtama kama Jimbo, au mtama kama mtama. Maana aliyesema atapiga mtama anatokea jimbo la mtama na si mkulima wa mtama.
 
Back
Top Bottom