Absalom Kibanda akamatwa!

Nani kamchochea nini? Hawajui kuwa serikali ndiyo inachichmbia kaburi? Hivi hawaoni mifano akida Mubaraka walivyonyanyasa vyombo vya habari na matokeo yake? Serikali pumbavu sana hii.
 
Mwenye details aweke basi, .....haitoshi kusema kuwa Kibanda kakamatwa!!
In fact si kwamba amekamatwa. Aliitwa kwenda kuhojiwa kutokana na makala iliyoandikwa na Mwigamba ambaye ana kesi ya uchochezi. Mpaka sasa hivi mahojiano yanaendelea, labda yatakapomalizika ndo wanaweza kumweka chini ya ulinzi.
 
wanajamii naendelea kufuatilia huu mtanange wa nami zaidi kati ya wabunge hawa vijana..lakini naona kama mda wa kupiga kura umeongezwa kimyakimya,je hiyo ni njama ya kumbeba mtu au ni mpango binafisi wa mwenye blog(mjengwa)

mjengwa ni kweli umeongeza mda wa kupiga kura!!?

nawakilisha......:lol:
 
Haja kamatwa ila ameitwa kulisaidia Jeshi la polisi acheni uchochezi nyie mnajua maana ya kukamatwa!!!!!

anaitwa kulisaidia?????????? yaani yeye ana ujuzi zaidi ya hao Polisi hadi awasaidie au?????????? wanampotezea muda wa kufanya kazi zake ............yaani .............. kwa .......... hao polisi wenyewe ..........majority wako hoi bin taaban ..............wamelundikwa pale wanapoishi miaka nenda rudi .... no change of houses .... no change of life style............ halafu wamekata tamaa hadi wanashindwa kufanya usafi wa mabanda yao ya bati ............ ila wala hawaelewi ........ SIKU WAKIFUNGUKA MACHO NA MASIKIO ...........NDIO WATAONA NA KUELEWA
MWANDISHI WA WATU AJIPE MOYO TU ......HILO NALO LITAPITA :disapointed:
 
Yote hii ni kuthibitisha kuwa JK na CCM yake wameshindwa kutawala Tanzania na kunatakiwa serikali mbadala.

Ni dhahiri kuwa Chama cha Magamba-CCM kimeshachanganyikiwa mpaka sasa hawajui nani hasa ni mbaya wao!Inasikitisha kuona kwamba kwa sasa ni kamatakamata ya yeyote ambaye anajaribu kukosoa sera za Wanamagamba. Kama serikali imefikia hatua ya kuamua kuwashtaki wanafunzi wa Vyuo Vikuu,kuwafukuza na kuwanyima udahili katika chuo chochote Tanzania basi tunakoelekea ni kubaya.
 
Haja kamatwa ila ameitwa kulisaidia Jeshi la polisi acheni uchochezi nyie mnajua maana ya kukamatwa!!!!!

anaitwa kulisaidia?????????? yaani yeye ana ujuzi zaidi ya hao Polisi hadi awasaidie au?????????? wanampotezea muda wa kufanya kazi zake ............yaani .............. kwa .......... hao polisi wenyewe ..........majority wako hoi bin taaban ..............wamelundikwa pale wanapoishi miaka nenda rudi .... no change of houses .... no change of life style............ halafu wamekata tamaa hadi wanashindwa kufanya usafi wa mabanda yao ya bati ............ ila wala hawaelewi ........ SIKU WAKIFUNGUKA MACHO NA MASIKIO ...........NDIO WATAONA NA KUELEWA
MWANDISHI WA WATU AJIPE MOYO TU ......HILO NALO LITAPITA :disapointed:

How can u change the form four failures?
 
"Katika mazingira haya
ndimo tunakuta: kamata
mbowe, kamata Slaa.
Kamata Zitto. Bambika
mashitaka. Weka rumande.
Peleka mahakamani… Fungulia mashitaka… kama
jana, kama leo, kama kesho,
kila siku."

Mnayakumbukwa hayo maneno yaliandikwa na mwandishi gani wa mwanahalisi?
Je kinatofauti gani na hali inayoendelea leo nchini kwetu?

nakumbuka ni andishi la Ndimara.
 
Tumepewa uhuru wa kujieleza. Ila usivuke mipaka.

Elimu ndogo wewe!!Right to expression/speak is human right and human right can't be taken nor granted by anyone except God!Ts God gifted!
Wenye elimu ndogo utaskia Rais Kikwete ametoa uhuru mwingi sana hadi watu wanamsema,who is he??Vinyago tuvichonge sisi wenyewe alafu vitutishe!!

Haki za binadamu huwa zinabakwa tu,
 
Hii lazima tutashinda tu!!! serikali Dhalimu hutisha wananchi kwa kutumia jeshi but soon and very soon we wiil be free from them!!!
 
polisi walianza na huyu==>>>

MWANDISHI wa safu ya
‘Kalamu ya Mwigamba (36)’
inayochapishwa kila
Jumatano na gazeti la
Tanzania Daima, Samson
Mwigamba (36), jana alifikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam, kwa kosa la
kuwashawishi askari na
maofisa wa majeshi ya hapa
nchini kuacha kuitii serikali iliyopo madarakani kwa sasa.

Mwigamba ambaye ni
Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Mkoa wa Arusha
alifikishwa mahakamani hapo
jana saa tatu asubuhi chini ya ulinzi mkali wa makachero wa
Jeshi la Polisi na kisha
kuifadhiwa katika mahabusu
ya mahakama hiyo, kabla ya
kupandishwa kizimbani na
kusomewa shitaka hilo la jinai namba 289, la mwaka huu. Mbele ya Hakimu Mkazi,
Waliarwande Lema, Wakili
Mwandamizi wa Serikali
Elizabeth Kaganda, alidai
mshitakiwa huyo anakabiliwa
na kosa la kuwashawishi askari na maofisa wa Jeshi la
Polisi, Magereza na Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) kutoendelea
kuitii serikali iliyopo
madarakani kwa sasa ambayo inaongozwa na Rais Jakaya
Kikwete, kinyume na kifungu
cha 46(b),55(10(a) na 35 cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu
kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002. Wakili Kaganda alidai
Novemba 30 mwaka huu,
gazeti la Tanzania Daima la
siku hiyo toleo Na. 2553
lilichapisha waraka uliokuwa
na kichwa cha habari kisemacho “Waraka Maalumu
kwa askari wote” ambao
uliandikwa na mshitakiwa
huyo kupitia safu yake
ijulikanayo kwa jina la
‘Kalamu ya Mwigamba’.

Hata hivyo mshitakiwa huyo
ambaye alikuwa amevalia
magwanda ya chama hicho
alikana kosa hilo na wakili
Kaganda alidai upande wa
Jamhuri hauna pingamizi la mshitakiwa kupewa dhamana
kwasababu kosa linalomkabili
lina dhamana kwa mujibu wa
sheria na kuongeza kuwa
upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika. Kwa upande wake, Hakimu
Waliarwande Lema alikubali
mshitakiwa apate dhamana
kwa sharti la kuwa na
wadhamini wawili wa
kuaminika ambao kila mmoja atatakiwa asaini ‘bondi’ ya sh
5,000,000, na kati yao
awasilishe hati ya mali
isiyoamishika yenye thamani
ya sh 5,000,000. Hakimu Lema alisema sharti
jingine ni kwamba
mshitakiwa huyo atatakiwa
kila mwisho wa mwezi aripoti
katika kituo Kikuu cha Polisi
na asalimishe hati yake ya kusafiria mahakamani hapo. Hata hivyo, Wakili wa
mshitakiwa Edson Mbogoro
alieleza kuwa wapo
wadhamini wawili ambao ni
madiwani wa wilaya ya Ilala
ambao wamekuja na barua zinazowatambulisha,
isipokuwa hawakuwa na hati
ya mali isiyohamishika na
kuiomba mahakama impatie
dhamana mteja wake.

Hakimu alikataa ombi hilo na
kuamuru mshitakiwa
apelekwe gerezani hadi
Desemba 20 mwaka huu, kesi
itakapokuja kwa ajili ya
kutajwa. Hii ni mara ya pili kwa serikali
kumfungulia kesi ya jinai
Mwigamba tangu mwaka huu
ulipoanza. Mwigamba pia ni miongoni
mwa viongozi na wanachama
wengine wa CHADEMA
wanaokabiliwa na kesi ya
mkusanyiko na maandamano
haramu ya Januari 5, mwaka huu, katika Jiji la Arusha na
kesi hiyo ipo katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Arusha na
imefikia hatua ya kuanza
kusikilizwa.
 
Back
Top Bottom