Absalom Kibanda akamatwa!

Jeshi la polisi linamshikilia mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, A. Kibanda kwa tuhuma za uchochezi. Kibanda anashikiliwa kwenye makao makuu ya polisi jijini Dar es Salaam.

===============

UPDATES

Habari zilizonaswa sasa hivi kutoka makao makuu ya polisi Dar zinasema Mhariri wa Tz Daima Absalom Kibanda ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa na polisi kwa zaidi ya masaa matatu kwa tuhuma za uchochezi. Amedhaminiwa na Mhariri wa Mwanahalisi Saed Kubenea kwa dhamana ya Sh 5,000,000/-. Kibanda anatakiwa kuripoti polisi hqtrs Jumatatu asubuhi.

Hawa watoto wa kufikia wa Lowassa bwana,lakini naona first born kaenda kumdhamini mdogo wake,kweli wanapendana sana siku hizi za karibuni
 
John Heche

tunalaani kitendo cha polisi kumkamata mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania daima, kitendo hiki ni dola kujaribu kutumia polisi kutishia waandishi ili waogope kusema maovu ya serikali ya ccm.

Na wewe umejiunga lini na jeshi la lowassa?mwenyekiti wako anazo taarifa hizi lakini?au unacheza ngoma usiyoijua?
 
Kama nilivyoeleza hapa: JOHN MNYIKA: Mwigamba apata dhamana; tuepuke dola ya kipolisi taratibu watawala wetu wanatupeleka kuwa na dola ya kipolisi. Mwaka 2008 walivamiwa Kubenea, Ndimara na Ofisi ya Mwanahalisi nilisema kwamba lile lilikuwa na shambulio dhidi ya uhuru wa kikatiba na haki za msingi wa kutoa na kupata habari. Matukio ya kukamatwa kwa Mwigamba na sasa Kibanda kutokana na makala ni kamata kamata ya vyombo vya dola dhidi ya uhuru wa kutoa maoni na kuwasiliana.

Ni dalili mbaya wakati huu ambapo kuna sheria mbovu kama ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 yenye kifungu chenye kutoa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 7 au faini ya hadi milioni 15 kwa makosa ya kukusanya maoni au kutoa elimu juu ya mabadiliko ya katiba kinyume cha sheria husika.

Kama kuandika makala tu kuhusu polisi kwa masuala ambayo hayana mwelekeo wa uchochezi au uhaini kama inavyodaiwa tayari vyombo vya dola vimeanza kamata kamata hatma ya mchakato wa katiba na masuala mengine ya kitaifa iko mashakani. Awali ilikuwa ni wananchi wa kawaida, wanasiasa wakiwemo wabunge, sasa wanahabari na hali hii itaendelea kwa wengine katika jamii kama tusipoungana pamoja kuidhibiti.

JJ

Unatafuta pa kutokea baada ya kutuingiza choo cha stendi mlipoenda kunywa chai ikulu sio?!!hapa hutoki kamanda!
 
Unatafuta pa kutokea baada ya kutuingiza choo cha stendi mlipoenda kunywa chai ikulu sio?!!hapa hutoki kamanda!
Unajuwa mtu mzima kuropokaropoka ni upunguwani? Yaani wewe ndio una akili kuliko sisi wote? unasema kutuingiza choo cha kike ni wewe na nani unaemuwakilisha hapo mpaka unatumia neno we badala ya i?
 
Kwa kufuata taaluma na maadili ya uandishi katika vyombo vya habari mhariri ametoka nje ya uringo wake kwa kuruhusu makala au barua kama hii ichapishwe kwenye gazeti lake. Mhariri ana mamlaka ya kukubali au kukataa makala au habari ambayo kwa haki alizo nazo pamoja na busara yake kulinda chombo chake cha habari.

Mhariri alikuwa na haki ya kuihariri kama kuna kitu ambacho kinaonyesha kuhamasihsa kinyume cha sheria. Na kama mleta mada alikataa angeweza kuiweka kapuini, ila kwa uamuzi wake wa kuichapa alijua nini kitatokea na ndicho kilichotokea.

Kwa habari hii kama ilivyotokea kwenye gazeti lake vigumu kumtetea, kwani siku zote kutanguliza busara ni kinga kwa kazi na wajibu.

Hana muda wa kusoma yuko busy na fred lowassa........!

Unajuwa mtu mzima kuropokaropoka ni upunguwani? Yaani wewe ndio una akili kuliko sisi wote? unasema kutuingiza choo cha kike ni wewe na nani unaemuwakilisha hapo mpaka unatumia neno we badala ya i?

Bwana matola ni wazi kwamba umekurupuka kunijibu kwa jazba nadhani inatokana na kumpenda kupita kiasi bwana mnyika hivyo hupendi kuona 'akigongwa',ukweli ni kwamba ungetulia kusoma kwa makini huo mstari wangu mmoja tu ungeelewa sikutumia neno la kumdhalilisha mwanamke(choo cha kike)...soma tena!

Kuhusu mimi pekee kuwa na akili kupita nyie wote pia si kweli,wapo wengi wenye akili wasiotawaliwa na mapenzi kupita kiasi labda kwa kiwango cha kukufikia wewe,nao ni hawa hapa chini!

1: Shukia: "Mnyika ndo katuuza. Katika makubaliano aliyotia saini pale Ikulu wakati anapiga ile 'tea', hakuna hata moja lilosema kuwa mmekubaliana rais asisaini muswada kuwa sheria kabla ya marekebisho.

Ni afadhali muheshimiwa Mnyika akae kimya na atuombe radhi kwa kutokutafakari makubalianao kabla ya kusaini. Ni sawa kabisa na wale wanaoingia mikataba mibovu.
"

2:Waberoya: "Mnyika naona unaona maoni ya watu wengi hapo juu, hata kitaani ni hivyo hivyo

All I can say to you guys please STICKY to your decision, chadema ijulikane ina mlengo gani, mlengo wa kulia, kushoto au kati, amueni kuwa radicals na dunia ijue hivyo...au muwe kondoo na dunia itawajua hivyo. Mmekuwa mnabadilika badilika sana.....

Hata iwe vipi hamtakuwa na uwezo wa kumfurahisha kila mtu.....ila amueni muwe vipi na mtavuta wengine kwa vile mtakavyokuwa!!

Leo mtakasirika, kesho mtamchekea yule yule aliyewakasirisha jana, kitu gani huwa kinatokea??...hatujui

Lingine, jamani ikiwezekana hiyo ruzuku ichukue nafasi ya posho zenu za bungeni...susieni vikao vya bunge na DUNIA ijue hivyo CCM wanajua kuwa huwa mnatisha leo....mnakuja kesho! this aint good not neither for your supporters nor for your members.

3:Manyanza: "hapa John Mnyika ulichofanya hakuna tofauti na NAPE NNAUYE, na wewe tumekuona Vuvuzela tu. Kwanini mlienda Ikulu kabla ya kutafakari? Halafu Ukaitisha press Conferess aibu. Yaani bora hata ya NCCR ambao hawataki hata kuonana na M.KWERE...

4:Mpiga kelele: "Mimi ningemuelewa Mh.Mnyika kama angeanza kwa kusema kuwa kile kipande cha karatasi kilichopatikana kwenye vyombo vya habari kikiwa na makubaliano mawili, ambacho alikisaini ikulu kilikuwa cha kughushi(yaani yeye kama Mh. Mnyika hajawahi kusaini kitu kama hicho). Kwa maelezo anayotoa sasa ni vigumu kunishawishi kuwa anaamini anachokizungumza."

5:KIMBUNGA:Hivi katika makubaliano aliyosaini Mnyika kulikuwa na kipengele kwamba Rais asisaini mswada? Au ile haikuwa sahihi ya Mnyika? Mnyika rejea hati uliyosaini wewe na Nchimbi na kama ni ya kughushi utuambie ila kama ni yako kwako wewe ndio inakiuka makubaliano. Vinginevyo useme ulisaini kitu ambacho hukukijua (kitu ambacho siamini). Ukiwa kama Mbunge wangu mimi binafsi nakuamini sana.

moz-screenshot-2.png

[h=2]Tuesday, November 29, 2011[/h] [h=3]Taarifa Ya Pamoja Ya Serikali Na Chadema Kwa Vyombo Vya Habari[/h]

Kwahiyo na wewe unaungana na Polisi kwamba makala ile ni ya uchochezi? umeshawahi kusoma gazeti la Al nuur wewe?

Siungani nao,ila naelewa kinachoendelea nyuma ya pazia, najua mafisadi wanamchezesha kibanda na huyo mdhamini wake ngoma yao,ndio sitamtetea hata nimkute anapigana na nyoka nitamsaidia nyoka,mi sitaki kuicheza ngoma ya kifisadi!madhara ya kuwakabidhi nchi hii mafisadi zaidi ya huyu anaeondoka madarakani ni makubwa kuliko kumuonea huruma kibanda na msaliti mwenzie huyo mmwagiwa tindikali aliekwenda kumuwekea dhamana ya mamilioni polisi!
 
Post # 167 ulichokileta hapo wewe ni ile karasi iliyochapwa kutoa taarifa kwa vyomba vya habari, naomba utuletee document ya makubaliano yao rasmi na acha kutuchezea akili watu na akili zetu timamu!
Pili kuhusu Kibanda chuki zako kwake ni za kimaslahi zaidi, nadhani nyinyi ndio wale ambao mkikosa connection za ulaji mnaanza kutokwa na mapovu.
 
Naona una matatizo ya kusoma kiswahili,labda ni mzuri zaidi kwa kusoma kiingereza!i don't know,but hiyo taarifa ndiyo rasmi ambayo kuhusiana na walichokuwa wakikizungumza na "kukubaliana",na hayo mawili ndio waliyoyazungumza na kukubaliana kwa mujibu wa signature ya mpendwa wako na bwana nchimbi,document ya makubaliano yapi unayoyajua wewe ambayo wengine hatuyajui?ntaiwapa wapi kwanza kama mpendwa wako hakuionyesha mimi nitaweza kweli,au unataka nifungwe kwa kukutwa na nyara za serikali???

Pili kuhusu kibanda ina maana yeye hatokwi na mapovu kwa kuwa ana connection sio?na wewe vipi ?uko connected na mnyika au?
 
Post # 167 ulichokileta hapo wewe ni ile karasi iliyochapwa kutoa taarifa kwa vyomba vya habari, naomba utuletee document ya makubaliano yao rasmi na acha kutuchezea akili watu na akili zetu timamu!
Pili kuhusu Kibanda chuki zako kwake ni za kimaslahi zaidi, nadhani nyinyi ndio wale ambao mkikosa connection za ulaji mnaanza kutokwa na mapovu.
Wewe acha ushabiki wa kipuuzi, ni nini usichoelewa kwenye waraka ule? Au una interests zako na mambo ya kuwapumbaza watanzania?

"Pamoja na sheria hiyo kupitishwa na Bunge"....... Bunge halipitishi sheria, linapitisha mswaada.

"kwamba yawepo mawasiliano na mashauriano ya mara kwa mara kati ya serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo".......... Wadau gani?, kwanini isiwe wabunge?...... Hebu tuambieni wadau gani ambao watawawakilisha wananchi. Hata mimi si mdau?
 
Achana nae huyu kamanda,mapenzi yake kwa mnyika yamemzidi nguvu na kupunguza uwezo wake wa kufikiri na kuchambua mambo,naona hawajui wanasiasa sawasawa,bado anaamini wana uchungu na yeye!
 
JESHI la Polisi limemkamata Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda, kwa tuhuma ya kuchapisha makala inayodaiwa kuwa ya uchochezi.

Kibanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), alijisalimisha mwenyewe jana majira ya saa nne katika ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, linaloongozwa na IGP, Said Mwema.

Mara baada ya kufika katika ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Kibanda alihojiwa na maofisa wa juu wa jeshi hilo kwa saa tatu akiwa na wakili wake, Nyaronyo Kicheere.

Akizungumza jana mara baada ya kuachiwa, Wakili wa Kibanda, Nyaronyo alisema polisi walimhoji mhariri huyo kwa tuhuma za kuruhusu kuchapishwa kwa makala wanayodai kuwa ya uchochezi.

“Kibanda amehojiwa lakini ameachiwa huru baada ya kudhaminiwa na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwanahalisi, Saed Kubenea, kwa dhamana ya sh milioni tano, na ameamriwa kurudi tena Jumatatu, Desemba 19 asubuhi. Hatujui ni kwa shughuli gani,” alisema Kicheere.

Hata hivyo, kuna hofu kwamba huenda Mhariri Mtendaji huyo akafikishwa mahakamani akiungana na Samson Mwigamba ambaye ndiye mwandishi wa safu maalumu katika gazeti la Tanzania Daima Jumatano.

Wiki iliyopita Mwigamba ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Arusha, alifikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kuandika makala ya uchochezi inayodaiwa kuwashawishi askari wote wa majeshi ya ulinzi na usalama pamoja na magereza kutoitii serikali halali iliyoko madarakani.

Mwigamba alitupwa rumande kwa siku tano baada ya kukosa dhamana kabla ya kudhaminiwa juzi Alhamisi Desemba 16.

Source: Tanzania Daima
 
baubu hiyo title imekaa ki udaku zaidi hapa sijui itakuwa hapa tz hasa kwa upande wa vyombo vya habari..
 
Back
Top Bottom