Mkuu hivi vinamaliza vijana hatari mtu anakunywa asbh analewa siku nzimaVipi na hizi pombe za vilailoni ama viroba maana ndo vinaharibu watu kabisa na mtu unakuta ameviweka mfukoni kama 10 hivi we utashangaa jamaa anazidi kulewa tu na Bar hajaenda...Watazibiti vp?
Tatizo ni kutambua ni saa zipi ndiyo saa za kazi? Wengine wanafanya kazi kwa shift (Polisi, hospitalini,viwandani, mahotelini, walinzi, nk.). Na wengine wanafanya siku mbili au tatu mfululizo halafu wanakuwa off kwa siku nzima inayofuata. Hivyo, kama wewe unamaliza kazi saa 11 jioni mwingine ndiyo anaanza kuelekea kazini. Sasa kwa nini huyo mtu asistarehe saa 5 asubuhi wakati yuko off? Miaka ya 70 gazeti la Daily News lilianza kupiga picha watu mtaani "wakati wa kazi" na kuwatangaza hao kama wazururaji. Haikupita hata wiki moja wakaacha kwani walijitokeza watu waliotaka kulipeleka gazeti mahakamni kwa kuwaita wazururaji wakati walikuwa livu. Sasa utampangia mtu saa ya kustarehe wakati yuko livu?