ZTE Nubia Red Magic 8S Pro+: 24GB RAM?

Reuben Challe

JF-Expert Member
Dec 10, 2021
2,761
5,048

Kama ulidhani kuwa Samsung Galaxy S23 Ultra na Xiaomi 13 Ultra ndio simu bora za Android mwaka 2023 basi hujaiona simu mpya inayotarajiwa kuachiwa kesho July 11 kutoka kwa kampuni ya Kichina ya ZTE.
Nubia Red Magic 8S Pro+ simu inayotarajiwa kuja na Qualcomm Snapdragon 8+ Gen 2 na hadi 24GB RAM


Actually, hii simu haiwezi kuwa na kamera kali kama Samsung Galaxy S23 Ultra au Xiaomi 13 Ultra ila itakuja na kamera ambayo ni fair kwa bei yake. Hata hivyo, hii ni gaming smartphone kwa hiyo focus yake haipo kwenye kamera.

Hizo picha mbili hapo juu ni matarajio ya mwonekano wa nje wa simu hiyo. Ila kuanzia hapa chini na kuendelea hizi ni picha za ZTE Nubia Red Magic 8 Pro ambayo ilishatoka tangu muda tu.


ZTE Nubia Red Magic series zimebase kwenye gaming performance,nice design,long battery life na matured software ambayo imejazwa gaming features kibao. Sasa ngoja nianze kuiongelea ZTE Red Magic 8S Pro+


ZTE Red Magic 8S Pro+ ni 5G phone na inatarajiwa kuja na display ya AMOLED yenye uwezo wa kudisplay rangi bilioni 1. Itakuja na refresh rate ya 120Hz ambayo inatarajiwa kuwa na 1300 nits peak brightness
. Screen itakuwa protected na Gorilla Glass 5.


Hata hivyo kama ilivyo flagship nyingi za mwaka huu, Nubia Red Magic 8S Pro+ haitakuja na Memory Card slot.
Jambo la kufurahisha ni kwamba inakuja na starting RAM ya 16GB na RAM ya juu zaidi ni 24GB RAM, Yes 24GB RAM wala sijakosea,Bila kusahau itakuja na chipset ya Qualcomm Snapdragon 8+ Gen 2
Simu za Nubia zinakuja na separate chipset inayoitwa Red Core ambayo kazi yake ni kusaidia vitu kama audio na haptic feedback processing na Ku control RGB lighting kwa hiyo inaipunguzia mzigo Snapdragon 8+ Gen 2 ambayo ndio main chipset.


Version ya 16GB RAM inakuja na storage options za 256GB, 512GB na 1TB. Version ya 24GB RAM inakuja na 1TB pekee, Zote zina UFS 4.0.


Tukija kwenye kamera, licha ya kuwa gaming smartphone lakini bado suala la kamera ZTE hawajaliacha nyuma. Itakuja na 50MP main camera, 8MP ultrawide camera na 2MP macro. Ingawa taarifa hizi si za uhakika asilimia 100. Inakuja na features kama LED flash, HDR na Panorama
Kamera ya nyuma inaweza kurekodi video za 8K@30fps, 4K@30/60fps na 1080p@30/60/120/240fps.

Kamera ya mbele itakuja na 16MP ambayo inarekodi video za 1080p@30/60fps
Ninafurahi kuona ZTE anatumia underdisplay selfie camera kwa hiyo hakutakuwa na kidoti chochote kwenye screen yako mfano angalia hapa chini
Inakuja na USB Type C 3.2 kwa Chinese version na USB Type C 3.1 kwa international version. Utapata stereo speakers kama kawaida, chipset ya Qualcomm Snapdragon 8+ Gen 2 (4nm) na GPU ya Adreno 740

Mwisho kabisa inakuja na Android 13 na skin ya Red Magic OS 8

Tofauti na ilivyo kwa software za simu nyingi za China, Red Magic OS ni very clean kama Stock Android tu inakuja na bloatware chache sana.
Ni kweli, Red Magic OS iko very clean kama Stock Android lakini haifanani na Stock Android hata kidogo. Red Magic OS inakuja na additional features nyingi sana kama style nyingi za Always on Display, Entertainment toolbox, uwezo wa kuweka picha, GIFs au hata video kwenye homescreen, dark theme, icons za kipekee na customisation kwenye interface yote ni mind blowing. There's too much customisation here
Unaweza kucustomize karibia kila kitu kwenye UI mfano kwenye Always on Display unaweza kuchagua style unayoitaka na unaweza kubadilisha mwonekano wa saa kwenye Always on Display kadri utakavyo. Kuna design nyingi za mwonekano wa saa ambazo unaweza kuchagua na bado unaweza kuweka hadi GIFs pia kwenye Always on Display.
Application ya Settings ina options nyingi sana unazoweza ku customize katika njia unayoitaka wewe. Unaweza kupunguza size ya icons halafu ukazibana apps unazotaka wewe zikae kwenye small interactive window. Hicho ki-window nacho unaweza kukiongeza ukubwa au kukipunguza kiwe kidogo.
Bado features kama Split screen zipo pia kwenye Red Magic OS.
Fingerprint scanner pia inaweza kutumika kupima mapigo yako ya moyo.
Pia Red Magic OS inakuja na features nyingi za gaming mfano Game space, Game Shorthand,Plugins na feature ya Red Magic Studio inayokuwezesha kucheza magemu ya kwenye simu yako kwenye PC, monitor au screen nyingine kubwa. Angalia hapa chini
Kama wewe ni mpenzi wa gaming basi hii simu itakufaa. Nimesahau kutaja battery capacity huko juu.
ZTE Nubia Red Magic 8S Pro+ inatarajiwa kuja na 5000mAh na 165W fast charger ambayo itaweza kuchaji simu hiyo kutoka asilimia 0 hadi 100 ndani ya dakika 14 tu

Gaming phones have come a long way



Specifications



ZTE Nubia Red Magic 8S Pro+ Quick Specifications

*DISPLAY
6.8 inch OLED 120Hz refresh rate
1300nits peak
1116ร—2480pixels
400ppi density

*Cameras
Rear- 50MP+8MP+2MP, 8K recording
Front- 16MP underdisplay, 1080p recording

*Performance
16GB/24GB RAM
Qualcomm Snapdragon 8+ Gen 2 (4nm)
Overlocked GPU

*Battery
5000mAh
Li Po
165W fast charging

Bei yake inatarajiwa kuwa Euro 700
Kama wewe ni gamer hii simu itakufaa sana. Kwenye gaming phones Mchina apewe maua yake



NB: Specifications hizi sio za uhakika wa asilimia 100. Simu ikiwa released nitakuja ku edit tena huu uzi
 

Attachments

  • gsmarena_009%20(1).jpg
    43.7 KB · Views: 10
Duh
Bonge la simu aisee, inakaa laini ngapi
 
Hiyo ambayo ilishatoka muda wanaiachia kwa milioni ngapi?
ZTE Nubia Red Magic 8 Pro tayari ipo ila bei yake ni around milioni 2 kwa version ya 16GB RAM 512GB ROM
Inakuja na 6.8inches na 6000mAh battery
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ