Zitto Zubery Kabwe Anafaa Kuiongoza CHADEMA!

TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2014
Posts
4,305
Reaction score
2,564
Kwa Chama chochote cha siasa kufanikiwa kinahitaji kuwa na Viongozi wenye mapanzi ya kweli na Chama husika.Mapenzi ya kweli kwa Chama husika huja pale MwanaCHAMA anapokuwa amekitumikia Chama kwa muda mrefu sana tangu utotoni (Chipukizi) hadi utu uzima wake.Kukitumikia Chama muda mrefu hivyo kunakufanya uwe hisia za upendo juu ya Chama hicho.Kuna aina flani za hisia unazitengeneza juu ya Chama kwa vile umekuwa nacho kwa muda mrefu.Zitto alishawahi kusema kuwa hataweza kuondoka Chadema kwasababu ana mapenzi nacho ya dhati,Najua kuna baadhi ya watu walichukulia kauli ya Zitto kama mzaha flani hivi ila kwa sisi tuliosomea Organizational behavior study tumemuelewa vizuri sana.Zitto anafaa sana kukiongoza Chadema kwasababu hajawahi kuwa Mwanachama wa Chama kingine.Mbowe,Dr Slaa,Tundu Lissu na wengieo wote hawa walitokea CCM na wana unasaba na CCM kwa asilimia kubwa.MwanaCHADEMA jiulize kwanini baada ya Zitto kutimuliwa na Chadema hawa CCM hawaonekani kumchangamkia kama ilivyokuwa kwa akina Mwampemba?Kaa tafakari.
 
Lzima wewe utakuwa gamba tu,atafaaje wakati alishanunuliwa kwa hela za kufa mtu.labda kusudi iwe ccm B
 
Huu uzi hauna muda hapa....sasa hivi utafungwa...
 
Impact ya ZZK Itaendelea kuitesa cdm maishani mwao...
 


pole sana, yaelekea haukuwepo nchini baada ya ZZK kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya CDM, MIKUTANO YOTE YA ZZK ILIYOFUATA KIGOMA, TABORA NA KUKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI ILIRATIBIWA NA KUFADHILIWA NA CCM
 
Unadhan ccm ndowanakimbilia msaliti? Jipange
 

hukumbuki walivyomwandalia mkutano serena hotel???
au walivyoshirikiana naye kuhujumu ziara ya dr Slaa?
 
Alliance for Creative Traitors (ACT) ipo, kachukue kadi.
 
Reactions: G11
Baada ya kusoma uzi huu , NIMECHEKA SANA ! Asante mkuu kwa kuamua kutuvunja mbavu !
 
Kwa sababu umemsifu basi hu uzi utabak, kinyume na hapo ungekua ushaondolewa, sheria mpya za jf hauruhusiwi kumsema vibaya zitto ukifanya ivyo utapigwa tu
 
Mwenzako anajifariji kwa kuvaa ngwanda ili mjue yuko cdm akilin anajisuta kwa upuuz na ushenz wake.....

Anafaa kuwa mwenyekt wa ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…