Chikawe Jr
Member
- Jun 6, 2017
- 23
- 85
Na
Juma George
Tanzania ni mali yetu, kuipenda na kuijenga ni wajibu wa kila mmoja wetu. Huu ndio ulikuwa msimamo wa wazee wetu walioipigania na kuikomboa nchi hii kutoka katika mikono dhaIimu ya Mkoloni.
Kauli mbiu hii ilishika kasi hasa baada ya mapinduzi ya utawala wa Kikoloni mwaka 1961 na 1964, na kila Mtanzania alijua tafsiri ya kuipenda nchi yake na kuijenga. Katika hili sitosahau dhana ya SIASA ZA UJAMAA NA KUJITEGEMEA. Wazee hawa walikuwa na busara pevu sana, hata kuona kuwa UHURU wa KWELI ni pale tu tutakapoweza kujitegemea. LAKINI leo nasikitia ninapowaona vijana kama wakina ZITTO ZUBERI KABWE ambao hawaoni busara za wazee hawa kuwa ni za kuzingatiwa na zaidi sana wameshika kasi kudharau na kutumikia Mabepari. Wakati wengine tukichukua fito na kuijenga nchi yetu iliyobomolewa vibaya na UKOLONI MAMBOLEO wao hawajaacha kuwa Vibaraka wa Mkoloni na kubomoa pale tunapojenga, tena bila woga hivi ni nani ALIYEWALOGA?
Mara kadhaa Zitto Zuberi Kabwe amekuwa mstari wa mbele kuwa kinyume na Nchi yake na kusema mambo ya hovyo wazi wazi bila kujali Utaifa. Katika maandiko yake amekuwa akisema Vibaya Serikali na kuwaaminisha watanzania kuwa ndio namna ya kukosoa wakati sio kweli.Huu sio ukosoaji na kwa nchi kama Marekani au Urusi au China watu kama hawa huitwa wasaliti wa nchi.
Mwanasiasa bora ni yule anayekuja na Mbadala wa njia ya kutatua tatizo na si kuendelea kuongeza tatizo. Katika utumishi wake kama Mbunge, Zitto Zuberi Kabwe anajua fika kwamba maendeleo ya nchi yoyote hayatokani na misaada isipokuwa KODI ZA WANANCHI na MIKOPO kutoka kwa nchi marafiki. Hata marekani, Urusi, Ujerumani n.k wanakopa lakini hilo haliwafanyi kuachana na mipango ya kujijengea uwezo wa kukopesha wengine kwa kuwa kukopesha ni kuwekeza. Haya yamekuwa yakifanyika na SERIKALI YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI hapa kwetu kwa dhamira hiyo hiyo ya kutaka kujitegemea KIUCHUMI, KISIASA NA KIJAMII.
Tumeona jitihada hizo za kujikomboa kutoka utegemezi kwa kuongeza mkazo katika kukusanya KODI, Kuweka sheria nzuri zinazolinda Rasilimali zetu, Kupunguzia makali ya gharama za elimu watanzania kwa kutoa elimu bure pamoja na mambo mengi makubwa.
Cha kushangaza ni kwamba wakati wengine wanajenga wanasiasa kama wakina ZITTO wamejipa kazi ya kupiga kelele na kuichafua nchi kitaifa na Kimataifa. Zitto Zuberi Kabwe anajua kuwa ni asilimia 30 tu ya walipa Kodi wote ndio hulipa Kodi, na hata hivyo hawalipi Kodi stahiki. Hii ni ishara kuwa Asilimia 70 ya wanaotakiwa kulipa kodi hawalipi kodi zao kabisa, lakini huwezi kusikia ZITTO KABWE analisemea hilo au hata kuhamasisha wananchi KUDAI RISITI wakati wa KUNUNUA bidhaa au Mfanyabiashara kutoa RISITI ANAPOUZA BIDHAA. Uchu wa madaraka na dhamira ya kuiondoa CCM kama wanavyotumwa na mataifa ya magharibi ndio muhimu sana kwao kuliko misingi ya nchi au maendeleo ya watanzania. Kwa kauli zao za uongo na za hovyo zimeendelea kuharibu mitazamo ya wananchi wetu na kuchochea tatizo la wananchi kutopenda kulipa kodi Nchini. Mambo haya hayakubaliki.
Mara zote serikali imeonyesha ugumu uliopo wa kuipata Kodi ambayo wananchi wanachangia kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa ajili ya maendeleo yao. Ikumbukwe kodi hii inapitia katika mikono ya wafanyabiashara ambao wanapaswa kuiwasilisha Kodi hiyo serikalini lakini waliowengi wao hawafanyi hivyo.
Tulitegemea watu wenye ushawishi katika jamii kama wakina ZITTO KABWE kuwa mstari wa mbele kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi lakini hawafanyi hivyo na wakati mwingine wanaenda mbali zaidi kupotosha na kuibomoa jamii yetu katika misingi yake ya UMOJA, UZALENDO na UTU na kujenga Chuki, Utengano na Usaliti.
Tunajua uko tayari hata kuuza nchi ili tu utimize malengo yako binafsi. Huu ni usaliti na sisi wazalendo tunakushauri achana na hiyo biashara kwa sababu haitakulipa. Hakuna siasa zisizo na mipaka na wewe unajua, na msingi wa siasa ni kuleta maendeleo kwa wananchi na sio kuifarakanisha Dola na wananchi wake. Ni busara ya kisiasa kukaa chini na kuangalia mapungufu ya mwenzako na kuwa na Mkakati wa ushawishi lakini sio kupotosha watu au usaliti. Hii nchi ni muhimu kuliko Siasa na Wanasiasa kama wewe na kamwe hatuwezi kuwaacha mtufikishe pabaya kwa maslahi yenu wanasiasa wachache mnaotumiwa na Watu wa magharibi.
Watanzania wanauchungu mkubwa wa kuibiwa Rasilimali zao na hawako tayari kuona mtu anawayumbisha na kuwatoa katika agenda za msingi za maendeleo. Kuna watu wana uchungu na hii nchi kuliko wanasiasa, ni vema mkatulia mkasubiri 2019 na 2020 maana mtakuwa na uwanja mpana wa kuendesha siasa na sio sasa.
Narudia kusema NCHI NI MUHIMU KULIKO MWANASIASA MAARUFU. Rais kwa kuzingatia umuhimu wa kujenga Nchi ameteuwa watu kutoka katika chama chako ulitakiwa kuona ni kwa namna gani ameona UMUHIMU wa kujenga nchi na watu wote bila kuangalia UVYAMA.
HII NCHI YETU SOTE, WANASIASA HAMNA HATI MILIKI MSITUSUMBUE, Mwacheni RAIS MAGUFULI tuliyempa dhamana ya KUTUONGOZA atimize MAJUKUMU YAKE.
TANZANIA KWANZA
UZALENDO WA KWELI.
Chikawe Jr.