Zitto usidhulumu pesa ya kununulia sanda siku ya msiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto usidhulumu pesa ya kununulia sanda siku ya msiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wasegesege, Dec 13, 2009.

 1. W

  Wasegesege Senior Member

  #1
  Dec 13, 2009
  Joined: Oct 22, 2009
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli, Adanganyika bado tupo GIZANI. Kabwe alisema tangu mwaka 2007 kwamba hataendelea na shughuli za Kisiasa itakapofika mwaka 2010, na muda huo bado siku chache. au hukuweza kumsikia? Lakini wewe uliyeandika Makala hii ni Mwanachama wa CHADEMA ungepaswa kuwa nje ya CHAAAAAAAAA DEMA!! ungeweza kuandika makala nzuri zaidi ya hii. Unatakiwa uwe unajua namna ya kuanisha mada zako ziende sambamba na wakati uliopita, uliopo na unaokuja, lakini bila kusahau kauli ya mlengwa anayesemwa.

  Tatizo letu tunapenda Mtu badala ya Chama, hili ndiyo tatizo. Na tunasahau kwamba, vyama vyote ni zao la CCM (kwa maana kwamba Viongozi wa Vyama hivyo ama walikuwa wanawania Uongozi katika Chaguzi mbalimbali ndani ya CCM wakakosa ama walikosa kitu fulani wakaamua kuhama).

  Mfumo wa Vyama vyote vya Siasa vya Tanzania ni kama Mfumo wa CCM, tofauti ni majina tu. Hakuna Kiongozi hata mmoja wa Chama chochote cha Siasa anasema atakuwa Madarakani kwa maslahi ya Watanzania. HAIJAWAHI KUTOKEA na itachukua miaka 100 mbele kutokea kwa sababu mpaka sasa hakuna dalili zozote.

  Angalia namna ya Utawala na Uendeshaji wake wa Vyama vya Siasa ambavyo vimekamata Halmashauri. Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri hajafanya lolote la kuongeza mapato kwenye Halmashauri hizo.

  Vyama vinasubili tu ruzuku kutoka Serikali Kuu (Hela ya Wavuja jasho na wanuka Chumvi)

  Mie sijakuelewa unapomsema Zitto Kabwe.

  Hebu Punguza Ghadhabu, punguza Hasira, shusha pumzi uwe Mtoto wa Kike au wa Kiume. Kaa chini vitazame vyama vya Siasa Kuanzia na Chama chako Cha CHADEMA.

  Angalia wakati wa Uchaguzi wa ndani wa Chama?

  Ona yaliyokuwa yanatokea.

  Wanasiasa wote wa Tanzania ni WANAFIKI. Anakukumbatia kwamba yameisha na anacheka machoni lakini moyoni VITA VINAENDELEA.

  Roma wanamsemo wao mzuri sana. Unasema hivi:

  MBWA AKIMUONA MTU ANAKULA CHAKULA CHA BWANA HUWA ANABWEKA SANA TENA KWA UKALI ILI BWANA ASIKIE.

  LAKINI MBWA HUYO HUYO AKILA YEYE CHAKULA CHA BWANA HUWA MKALI PALE ANAPOFUKUZWA ILI ASIENDELEE KULA.

  Ona hili Mboe ni M/Kiti wa CHHAAAAAAAAA DEMA, na ndiye anayeongoza Vikao vya kuwawajibisha wanaokiuka taratibu za matumizi ya fedha za Chama, LAKINI YEYE NI MTIA SAINI. Inachekesha- sasa kukiwa na matumizi mabaya nani anakuwa mwenyekiti wa kumkemea mwenyekiti.

  WEWE MWANDISHI MWACHE KWABE ASOME APATE ELIMU YAKE AENDE KWENYE SUALA LINGINE.
   
Loading...