Vhagar
JF-Expert Member
- Jun 8, 2015
- 20,351
- 39,577
ZITO NI MSALITI WA WATANZANIA ASIYE NA UCHUNGU NA NCHI HII ZAIDI YA TUMBO LAKE
Na
Joseph Mwakatobe
Mwanasiasa zito ambaye ni Mbunge wa kigoma mjini takribani siku3 zilizopita ametoa kauli ya kwamba RAISI MAGUFULI anaikosesha serikali 1.8 trilioni Sababu ya mchanga wa dhahabu (ambao wataalamu wanasema mchanga huwa na zaidi ya 75% ya dhahabu) uliozuiwa bandarini kontena 268
Anasema uzuiaji huo wa mchanga ambao zaidi ya 50% ni dhahabu umesababisha kufeli kwa mauziano ya kampuni ya ACCACIA kwenda kampuni nyingine na hivyo serikali kukosa 20% ya capital gain
Huu ni upuuzi na ubinafsi sawa na ufisadi kama ufisadi mwingine ni kauli ya ajabu kweli kweli tena kutoka kwa huyu anaejiita mzalendo ana uzalendo upi zaidi ya undumilakuwili na tamaa ya rushwa bila kujali maslahi ya TAIFA hili
Niweke hesabu sawasawa kuonesha upuuzi wa huyu mtu bei ya gram 1 dhahabu kwa vunja bei inasimamia (50,000/=) elfu 50 ------- kilo1 ya dhahabu sawa na gram 1000 ni (50,000,000/=) milioni 50
Tani 1 ya dhahabu sawa na kilo 1000 ni (50,000,000,000/=) inasomeka TRILIONI HAMSINI. 50% ya hiki kiwango ni TRILIONI ISHIRINI NA TANO uzito mwepesi kabisa wa kontena ninaoufahamu ni Tani 5 tu hivyo ukizidisha na TRILIONI 25 unapata TRILIONI 125 pesa taslimu za kitanzania sio dola yapo makontena mangapi...... 256 hizo hesabu utamalizia mwenyewe mtanzania .
Nachotaka kusema hapa ni nini ni kwamba tunao wanasiasa ambao wana sura mbili moja wanajionesha ni wema lakini pili na mafisadi wahujumu uchumi na wachumia tumbo ni akili za kiuwendawazimu kwa anayejitambua mwanachi wa kawaida kuacha zaidi ya TRILIONI 125 ipotee ili kulinda mkataba wa TRILIONI 1.8 Watanzania wa leo sio wajinga kama yy alivyo na kwa hili ni dalili wazi kuna jambo lipo nyuma ya pazia na kauli hii tatanishi ya zito
Baada ya kushuhudia tatizo hili MAGUFULI amechukua hatua maramoja kumtengua katibu Mkuu wa wizara ya nishati na madini kwa suala hili napendekeza hatua zaidi zichukuliwe dhidi yake kwa uhujumu uchumi baada ya kupata thamani halisi pamoja na madini mengineyo yaliyoambatana na mchanga huo wa dhahabu
Lakini zito huyu huyu anaacha kupiga kelele kwanini ACCACIA hawauzi hisa zao DSE wanauza LONDON STOCK EXCHANGE kwa bei ya 25,000/= sawa na pound 10 kwa hisa moja hivyo kufanya umiliki wake usiwe wa watanzania bali waingereza wakiendelea kukaidi agizo la kuuuza hisa zao DSE na Jana katika akaunti yao ya twitter ACCACIA wanasema wanapoteza dollar milioni 1 sawa na TRILIONI 2.2 pesa za kitanzania kila siku sababu ya mchanga uliozuiwa bandarini hivyo wanajipanga kiwanda cha kuchuja na kuyeyusha mchanga hapa nchini
Nimalizie kwa kusema ile Kauli ya MAGUFULI alipofanya ziara ya kushtukiza aliposema kwamba "MALI ILIYOPO HUMU UNAWEZA KULIA MACHOZI" kwakweli imenigusa sana sana kama mzalendo wa nchi hii tunaye RAISI ambaye anaipenda nchi hii kwa moyo wake wote japo Wapo ambao hawamuelewi bado ila ni mzalendo mwenye uchungu na nchi kwasababu amezaliwa Tanzania amekulia Tanzania na atafia Tanzania na napata ukakasi kwanini Wapo wanasiasa ambao hawana chembe ya huruma kwa rasilimali za nchi hii ambazo zingetufaa sisi na vizazi vijavyo wanaona sawa vipotee tu
Joseph Mwakatobe
Mwananchi wa kawaida