Elections 2015 Zitto, mtumishi wa Mungu wa karne hii

EXPULSION

JF-Expert Member
Apr 1, 2015
386
280
Zitto ndio tumaini jipya la kuwakomboa watanzania wanaosumbuliwa na matatizao lukuki ya hii nchi.Zito kama kiongozi amejipanga kuwakomboa watanzania kutokana na umasikini, ujinga na maradhi.

Zito ni kijana wetu shupavu, anayeumia kwa kuona watanzania wa sasa hawana dira ya taifa ya kizalendo.Amejipanga kuwaelimisha watanzania watambue ni wapi walipokosea na kujirekebisha kufikia Tanzania tunayoitaka. Anafahamu ni nini kifanyike, mahali gani na kwa wakati upi.

Ana maono ya kiuongozi na nia ya dhati kuwatumia watanzania kwa haki na usawa. Anapenda kufanya kazi kwa pamoja, majadiliano na kwa kufanya tathmini ya jambo kwa wakati muafaka. Ni mtu mwenye kufikiria kizazi cha sasa na miaka mia mbeleni, kwa kuangalia changamoto za sasa na kufanyia forecast ya miaka mia na kuchukua hatua kwa muda muafaka.

Dhumuni la hii topic ni kuwapa wasifu wa ndani wa kijana wetu, mtumishi wetu na tushirikiane naye kuweka misingi thabiti ya kuijenga Tanzania tunayoitaka kwa miaka mia ijayo

Nawasilisha
 
ZITO ni tumaini lako wewe usiyejitambua usitulishe maneno,atakukomboa wewe na familia yako nasi watanzania.
 
Najua siku zote nabii hakubaliki kwao kwa asilimia zote.Sio lazima umkubali mtumishi wetu wa karne hii.
 
aaaa wapi zito ni mdomo dom tu ndo unampa hata kula naskia alikataa zile hela za kiinua mgongo kazifuta mlango wa nyuma..
 
Najua siku zote nabii hakubaliki kwao kwa asilimia zote.Sio lazima umkubali mtumishi wetu wa karne hii.
Mnamtumia zito kama buzi la kisiasa mkizan mtapata viti vingi vya ubunge mkashibia huko wakati mwenzenu alitimuliwa na vijanga vyake. Angekuwa kaonewa kufukuzwa angetoa ushahidi usiokuwa na mashaka kuwa kaonewa
 
Zitto ni kibaraka wa CCM
1430050154766.jpg
 
Nijuacho mimi Zitto kabwe ni mwanasiasa sio mtumishi wa Mungu. Hii tabia ya kumwita Mtumishi wa Mungu tuiangalie inaleta mapigo kwa nchi, maana tunawapa watu hadhi ya upakwa mafuta wakati hawana tena wengine ni washirikina/ wachawi/ waganga wa kienyeji wa kufa mtu, tunawapa na kuwavisha majoho ya UCHAJI mbele za MUNGU WA KWELI. Ni hatari sana katika ulimwengu wa Roho kuendekeza ujinga huu. tuwe waangalifu katika post zetu
 
...acha kufananisha vilaza na watumishi Wa Mungu, labda huyo mtumishi wako ni Yuda Escariot mkuu Wa wasaliti....
 
Zitto ni mtumish mwaminifu,hata chadema walimtukuza kwa kumwita --------,ni mtumishi wa watu wake, mingu msaidie
 
Back
Top Bottom