Zitto Kabwe- TBC ni kichaka cha matatizo

Zumbe Kimweru

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2014
Posts
340
Reaction score
27
NOVEMBA 7, mwaka 2012 niliandika makala katika gazeti hili la Raia Mwema kuhusu uendeshaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali (kichwa cha habari; Maswali matatu muhimu kwa watu muhimu kitaifa).

Katika makala hayo nilieleza namna ambavyo Shirika la Magazeti ya Serikali (TSN) linapaswa kuwa Shirika la Magazeti ya Umma na kutumikia umma badala ya kuwa chombo cha propaganda cha Serikali.
Nilieleza namna ambavyo serikali imekuwa ikiingilia utendaji kazi wa shirika hili kinyume cha sheria ya kampuni, sheria ya mashirika ya umma na sheria ya msajili wa hazina ambazo zote zinaelekeza uhuru wa Bodi ya Wakurugenzi katika usimamizi wa uendeshaji wa shirika.

Ni vema niwajulishe wasomaji wangu kwamba, baada ya kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na TSN, Bodi ya Wakurugenzi imetekeleza maagizo yote ya kamati hiyo.

Bodi imefanya uamuzi kutofautisha shughuli za uhariri na shughuli za uendeshaji, imeamua kuchukua hatua kuhusu ufisadi katika ununuzi wa mtambo wa kuchapa magazeti na pia kuwezesha mtambo huo kufanya kazi kwa ufanisi, imekaimisha nafasi ya Mhariri Mtendaji kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo na imepeleka mapendekezo yake kwenye mkutano mkuu wa kampuni kuhusu suala la kuorodhesha Shirika katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Ni dhahiri iwapo masuala haya yatakuwa yametekelezwa kikamilifu TSN itakuwa Shirika la Magazeti ya Umma badala ya Shirika la Magazeti ya Serikali, linaloendeshwa kwa maslahi ya umma bila upendeleo wa kisiasa na kwa faida. Leo nahamia shirika jingine kwenye tasnia hiyo hiyo ya habari.

Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) ni moja ya mashirika nyeti sana katika nchi yetu. Hata hivyo ni Shirika linalopewa lawama nyingi sana na hasa kutoka vyama vya siasa, inaonekana kuwa TBC hupendelea zaidi habari za chama tawala na kuonekana kama mashine ya propaganda ya Serikali.

Shirika la TBC linapaswa kuwa Shirika la Utangazaji la Umma na sio Shirika la Utangazaji la Serikali. Linapaswa kuhudumia umma kwa kutoa taarifa, elimu na burudani kwa umma. Shirika linapaswa kutoa haki na fursa sawa kwa wadau wote na nyakati za chaguzi kufanya ?coverage? kwa usawa kwa vyama vyote.

Hata hivyo ni lazima Shirika liwe na bajeti ya kutosha inayogharimiwa na umma, Shirika liendeshwe kwa uhuru na bila upendeleo wowote. Bahati mbaya, TBC imekuwa chombo kinachoendeshwa kwa upendeleo mkubwa, kutoa nafasi kwa Serikali na chama tawala na hata kuhusika kusambaza propaganda mbaya dhidi ya vyama vingine vya siasa au makundi ya kijamii yanayokosoa serikali. Pamoja na kutumika huko, bado shirika hili linaendeshwa kwa ufanisi wa chini sana, bajeti ndogo na mazingira magumu sana ya kufanyia kazi.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma ilianza kazi zake mwaka 2013 kwa kutembelea TBC kwa ajili ya ukaguzi wa hesabu na utendaji wa kazi. Lililokuwa dhahiri kabisa ni kwamba shirika lina hali mbaya, majengo yake hayajakamilika tangu mwaka 1995 Rais Ali Hassan Mwinyi alipoweka jiwe la msingi kujenga jengo hilo na sehemu ya kutunza nyaraka muhimu kuna hali mbaya. Kamati ilitembelea ?archive? ya shirika na kukuta namna ambavyo kumbukumbu za historia ya nchi zinavyohifadhiwa na kwa kweli ni masikitiko makubwa.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa kwamba kumbukumbu za taifa zitapotea kutokana na utunzaji mbovu ya mikanda ya video na hata sauti.
Kamati lilishuhudia ?studio? za shirika zikiwa katika hali mbaya ambapo uwekaji wa picha kwa ajili ya matangazo ni wa zamani na ndio maana hata mara mara tunaona matangazo yakiwa yanazimika.

Morali ya wafanyakazi ipo chini kutokana na malipo duni na pia vitendea kazi vya hovyo. Mwaka wa fedha 2012/13 shirika liliomba bajeti ya shilingi bilioni kumi na mbili na milioni mia tano, serikali ikapitisha shilingi milioni mia tano tu.

Katika mazingira haya huwezi kuwa na Shirika la Utangazaji la Taifa lenye jukumu la kutoa huduma kwa taifa zenye ubora.
Masuala ya mikataba nayo kama ilivyo kwa mashirika mengine imegubika TBC. Itakumbukwa mwaka 2009 shirika liliingia makubaliano na Kampuni ya Star Communication Network Technologies Company Limited ya China kuanzisha kampuni ya Star Media (Tanzania) Limited.

Katika ubia huu Shirika la TBC lina hisa asilimia 35, Kampuni ya Star Communication asilimia 62 na Kampuni ya SDTV asilimia tatu.
Mtaji wa kampuni hii ya ubia ni dola za Marekani milioni moja na kila mbia alitarajiwa kulipia hisa zake kulingana na kiwango cha hisa wanachomiliki. Hata hivyo kamati ilikuta mazonge mengi katika mkataba huu na hasa mchango wa kila mbia katika kampuni ya ubia. Kwa mfano TBC walitoa ardhi ya kuweka mitambo na ofisi bila makubalino maalumu ya namna mbia atakuwa analipia upangaji huu. Tayari TBC na wabia wake katika Star Media wamekubaliana kuhusu malipo haya ya upangaji.

Suala lenye utata sana ni mkataba kati ya Star Media na Kituo cha Uwekezaji nchini ambapo kampuni hii ilipewa hadhi ya Mwekezaji wa kimkakati (Strategic Investor). Katika makubaliano hayo kampuni ya ubia ilitakiwa kuwekeza jumla ya dola za Marekani milioni 238 ikiwamo mtaji wa dola za Marekani milioni 34, mikopo kutoka benki dola za Marekani milioni 68 na mapato ya ndani dola za Marekani 136 milioni.
Mpaka sasa hesabu za kampuni za ubia zinaonyesha kuwa mtaji ulioandikishwa BRELA ni dola milioni moja tu ambazo hazijalipiwa na mbia yeyote na mkopo uliochukuliwa ni dola milioni 48.

Kimsingi StarMedia inaendeshwa kwa mkopo tu bila mtaji wa wanahisa na kama mkopo huu unatoka upande mmoja wa wabia na kutoka shirika dada ni dhahiri kuwa faida kubwa ya kampuni itakwenda kulipia madeni na TBC inaweza kukaa muda mrefu sana bila kupata gawio lake. Kinachoshangaza ni ile hali ya mamlaka za umma kutosimamia mikataba sawa sawa na hivyo kuweka maslahi ya nchi kwenye matatizo makubwa.

Hivi sasa nchi imeingia katika dijitali na hivyo kulazimisha wananchi kuwa na ving?amuzi kwa ajili ya kupata huduma za matangazo, kwa kuanza na televisheni na kisha radio.

Hivi sasa Watanzania 700,000 wana ving?amuzi vya StarTimes ambavyo vinalipiwa jumla ya shilingi bilioni saba kila mwezi na hivyo kufanya mapato ghafi ya kampuni hii kuwa zaidi ya shilingi bilioni 70 kwa mwaka.

Kwa uamuzi huu wa kuelekea dijitali tayari serikali imetoa fursa kubwa ya kibiashara kwa kampuni za kuuza ving?amuzi kama StarTimes na hivyo ilipaswa kuweka misingi bora ya kuhakikisha taifa linafaidika na fursa hii ya kibiashara kwa kupitia Shirika la TBC na pia Watanzania wengine binafsi wenye kampuni za aina hii.

Inatarajiwa kuwa ifikapo mwishoni mwa mwaka 2013, jumla ya Watanzania milioni 2.3 watakuwa wanamiliki ving?amuzi na hivyo kuifanya biashara hii kuwa na thamani ya zaidi shilingi bilioni 300 kwa mwaka. Ifikapo mwaka 2015 jumla ya Watanzania milioni tano watakuwa na ving?amuzi na kupaisha zaidi biashara hii.

Utaona kwamba hii ni biashara kubwa sana. StarTimes kama kampuni iliyoanza kufanya biashara hii itafaidika sana. Inapaswa kuhakikisha kwamba TBC inafaidika sawia.
Katika hali ya kushangaza sana, malipo ya leseni ya kampuni ya StarMedia yalilipiwa na TBC peke yake. Jumla ya shilingi milioni 458 zililipwa TCRA kwa ajili ya leseni hii.

StarMedia wanasema wamesamehewa tozo ya leseni. Tunaweza kuwa na vivutio vya kuleta wawekezaji, lakini unawezaje kusamehe leseni? Sasa mamlaka za leseni kama TCRA zinaendeshwa namna gani kama tunaweza kusamehe hata leseni za kufanya biashara?
Kamati ya POAC ilitoa maagizo kwamba malipo ya leseni ya StarMedia ndio utakuwa mtaji wa TBC katika kampuni ya StarMedia. Wachina nao walipie sehemu yao ya mtaji. Umuhimu wa kulipia mtaji ni mkubwa sana kwani hivi sasa biashara hii ni kubwa na yenye uendelevu. Hii sio biashara ya kuchezea hata kidogo na hivyo ni lazima TBC wasimamie mkataba wao sawa sawa na kwa ukaribu. Hii ni biashara yenye thamani ya dola nusu bilioni katika muda mfupi sana ujao.

Kwa hali ya sasa ya uendeshaji wa StarMedia, mapato mengi yatatumika kulipia mikopo, hivyo ukaguzi wa mara kwa mara ni lazima ufanyike. Nilipoangalia hesabu za kampuni hii niligundua kwamba Wachina wanatumia ?Thin capitalisation? kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya mapato katika ubia inarudi kwao China na kwa faida ya mbia mmoja. Kamati imetoa maelekezo maalumu kuhakikisha kuwa TBC na Tanzania inafaidika na ubia huu.

Shirika la TBC linapaswa kuwa Shirika la Umma lenye kufanya kazi ya umma kwa faida ya umma. Tunatarajia kwamba Shirika litakuwa na ?channels? nyingine za masuala ya Umma kama TBC Bunge itakayokuwa na majukumu maalumu ya kurusha vipindi vya Bunge, kufanya elimu ya uraia kwa wananchi na kuendesha midahalo ya wananchi.

Hivi sasa kazi ya midahalo inafanywa zaidi na vituo binafsi vya televisheni kama ITV na StarTV wakati hili ni jumuku la Shirika la Umma. Nyakati za Uchaguzi Mkuu sheria iweke wazi kwamba TBC itafanya midahalo ya wagombea urais angalau mara tatu kwa masuala tofauti tofauti ili wananchi wawe na uchaguzi wakiwa wanawajua wagombea na sera zao. Hatutaki Shirika la Utangazaji la Umma kuanza kukimbizana na kampuni binafsi katika matangazo, hivyo lazima liwe lina bajeti ya kutosha kutoka kwa umma na liwajibike kwa Umma.

Lakini Watanzania lazima tukubali kwamba Shirika la Utangazaji la Umma lazima liendeshwe na umma kama tunataka litumikie umma badala ya kuitumikia Serikali na chama tawala. Hivyo hatuna namna isipokuwa ni kutumia fursa za kuingia dijitali kwa kuwa na tozo maalumu ya kuendesha TBC ambapo inapendekezwa tozo ya shilingi 1,000 kwa kila king?amuzi kwa mwezi. Lakini mapendekezo haya lazima yaweke uwanja sawa wa biashara kwa kuzuia Shirika la Utangazaji la Umma kufanya matangazo na hivyo kushindana na kampuni binafsi za utangazaji.

Wenzetu kwenye nchi nyingine wanafanya hivi, BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza, SABC (Shirika la Utangazaji Afrika Kusini) na mengine mengi. Hata hivyo hatuna budi kufanya mabadiliko makubwa sana katika uendeshaji wa Shirika na kuweka uwajibikaji wake kwa umma kupitia Bunge badala ya hali ya sasa ambapo Serikali ndio inaelekeza kila jambo lifanywalo na TBC. Tuwe na TBC ya Umma na sio ya Serikali. Tunapaswa kuelekea huko kwa kutazama mbali.

Wenzetu kwenye nchi nyingine wanafanya hivi, BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza, SABC (Shirika la Utangazaji Afrika Kusini) na mengine mengi. Hata hivyo hatuna budi kufanya mabadiliko makubwa sana katika uendeshaji wa Shirika na kuweka uwajibikaji wake kwa umma kupitia Bunge badala ya hali ya sasa ambapo Serikali ndio inaelekeza kila jambo lifanywalo na TBC. Tuwe na TBC ya Umma na sio ya Serikali. Tunapaswa kuelekea huko kwa kutazama mbali

- See more at: Raia Mwema - TBC ?&[HASHTAG]#8364[/HASHTAG];&[HASHTAG]#732[/HASHTAG];kichaka?&[HASHTAG]#8364[/HASHTAG];&[HASHTAG]#8482[/HASHTAG]; cha matatizo

Kumbe wamiliki wa ving'amuzi washafika milioni 5?
good bussiness indeed
 
Jamaa akirudi bungeni atakuwa hana cha kuongea maana kila siku matamko. Chama kimekataliwa na Watanzania hicho
 
Amewaacha Kwenye Mataa Washirika wake Ma-"M", Na Sasa wote Wako Taabani Bin Fukara. Chama Kilikosa Mvuto Na Sasa Ni Yeye

Kujitangaza Zaidi.
 
Kuondoka kwa Tido TBC ilikuwa ni kama kulitumbukiza hilo shirika ndani ya shimo.....huyo mshana sioni anachofanya zaidi ya kuitumikia CCM.
 
MSHANA NI JIPU!/
A FAILURE DIRECTOR LIVE BY 100% TOTALL FAILURE!
ii
 
Back
Top Bottom