ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 620
- 1,543
Serikali Ichukue Hatua Haraka Kuwaokoka Wananchi Wanaokabiliwa na Njaa Nchini
Leo (Machi 01, 2017) Shirika la utafiti la Twaweza limteoa matokeo ya utafiti kuhusu hali ya chakula nchini katika Ripoti iliyopewa jina la "Uchungu wa Njaa: Upungufu wa chakula Tanzania".
Pamoja na mambo mengine, matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kile ambacho kwa muda mrefu chama chetu cha ACT Wazalendo kimekuwa kikisema kuhusu hali ya chakula nchini.
Utafiti husika umeonyesha zaidi ya robo tatu (75%) ya watanzania hawana chakula cha kutosha majumbani mwao, na kwamba theluthi mbili (69%) ya kaya zote nchini zinakabiliwa na njaa, na kuwa theluthi moja ya kaya zote nchini (35%) zinalala na njaa kwa sababu ya kukosa chakula, hasa katika kipindi cha kati ya Septemba 2016 na Februari 2017.
Utafiti umeonyesha pia bei ya mahindi, ambacho ndicho chakula kikuu cha watanzania walio wengi, imepanda mara mbili, ikizidisha maumivu kwa wananchi wengi masikini wa Taifa letu.
Kimsingi matokeo ya utafiti huu ni tangazo la kitafiti kuhusu uwepo wa JANGA LA NJAA nchini.
Ni jukumu la msingi la serikali kuhakikisha usalama wa nchi na wananchi kwa ujumla. Jambo la chakula ni jambo la usalama wa nchi. Kwa serikali kukataa kujihusisha na kukalia kimya janga la njaa nchini ni kukwepa jukumu lake la msingi katika kuhakikisha usalama wa nchi na raia wake.
Tunaendelea kutoa wito kwa Serikali kutangaza rasmi uwepo wa janga la njaa nchini na kuchukua hatua stahiki katika kuwapatia chakula cha dharura wananchi wote wanaokabiliwa na njaa.
Aidha, tunatoa wito kwa watanzania wenye uwezo na nafasi, pamoja na mashirika mbalimbali ya ndani ya kimataifa kujitoa kuwasaidia wananchi wenzetu wanaokabiliwa na tatizo la njaa hapa nchini.
Chama chetu, ACT Wazalendo kitashiriki kikamilifu katika kuwasaidia wananchi wanaoabiliwa na njaa. Aidha, katika Bunge lijalo tutapeleka hoja maalumu ya kuibana serikali itenge bajeti ya kutosha kununua chakula cha akiba ya Taifa kwani hali ya chakula haitarajiwi kuboreka katika mwaka huu kutokana na hali ya ukame na mvua hafifu inazoendelea.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT –Wazalendo
Jumatano, Machi 01, 2017
Dar es salaam