Binafsi nimekuwa mfuatiliaji wa Siasa za ZZK kwa Kipindi kirefu sana (Tangia Akiwa University of DSM kama mwanafunzi).
Kwakutumia historia ya matukio mbali mbali aliyokwisha kuyafanya, pamoja na reaction yake juu ya uamuzi wa serikali kuzuia usafirishaji wa makontena ya mchanga nimehitimisha kuwa huyu jamaa ni hatari sana kwa ustawi wa Taifa la Tanzania. Ukiorodhesha wanasiasa ambao siasa zao msingi wake ni maslahi yao binafsi, huyu jamaa atachukua nafasi ya juu kabisa. Anatumia vibaya sana imani ambayo baadhi ya watanzania walikuwa nayo kwake, anatumia vibaya sana uwezo wake wa kushawishi.
Naomba muheshimiwa Rais, aamue kabisa kuwa linapokuja suala lenye maslahi makubwa ya Taifa, ambalo umoja wa kitaifa ni msingi ktk kulifanikisha, wanasiasa kama hawa wanapoto kauli za kukatisha tamaa, wakamatwe na walazimishwe kueleza msingi wa maoni yao na ikiwezekana watakiwe kuthibitisha. Tukiacha watu wawe wanaropoka ropoka vikauli vya kukatisha tamaa na kuichonganisha serikali na wananchi, itatuwia ngumu sana kusogea mbele kama taifa. Taifa haliwezi kuenda mbele bila wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali.
Kaka yangu ZZK naomba ujifunze kitu kupitia hii sagga, unajivua nguo mbele ya kadamnasi, hila zako zinaendelea kubainika.