Zitto Kabwe kakumbwa na nini?

Zitto Kabwe kakumbwa na nini?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,172
Reaction score
162,619
Zitto Kabwe ni mmoja wa wanasiasa ambao wako active sana kwenye matumizi ya mitandao na ni mara chache sana kuona siku inapita haja-post chochote mtandaoni hasa twitter na Instagram.

Cha kushangaza ni kuwa, tangu tarehe 08/07/2018 kapotea kabisa mtandaoni ingawa yametokea matukio ambayo kwa kawaida yake sidhani kama angeacha kuyaongelea kama lile la mapokezi ya Dreamliner na hili la leo la Twaweza kutakiwa kujieleza.

Zitto na chama chake wanajitahidi sana kutumia mitandao ya kijamii kufanya siasa na pengine kwa sasa ndio wanaongoza katika matumizi ya mitandao kufanya shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Wanasiasa wengine wanaweza kumaliza hata wiki hawaonekani mtandaoni jambo ambalo mimi binafsi naliona sio zuri sana kwao hasa katika nyakati hizi ambazo uhuru wao wa kufanya siasa za majukwaani umeminywa hivyo nilitarajia wangeongeza juhudi za kutumia mitandao kuwasiliana na wapiga kura wao, kujadili issues, kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu vyama vyao, n.k.

Wakati wengine wanatumia sana matangazo ya live ya tv kufanya siasa, Zitto na chama chake wanatumia sana mitandao ikiwemo JF kuendesha shughuli zao ila kwa siku tatu na sasa yakiwa yamebaki masaa machache ingie siku ya nne, Zitto kapotea kabisa hewani tofauti na kawaida yake.

Swali ni je, kabadili style ya kufanya siasa na kutumia mitandao au kuna jambo limemsibu?

Wapinzani, kwa sasa mnapaswa sana kuongeza nguvu ya matumizi ya mitandao kuliko wakati wowote ule ili muweze kukabiliana na hali hii ya sasa.
 
Muulize ado shaibu ndio polepole wao atakupa jibu mujarab
 
Anawasiliana na Lissu /dereva wa lissu kutafuta vielelezo....BY Musiba
 
Labda anaumwa, kwani yeye ni mashine? Mbona wewe ulipotea kabisa kwa karibia wiki moja baada ya maandamano ya dada yako Mange kubuma?
 
Mkuu hujui kwamba yupo busy kuandaa mazingira ya kuunganisha chama chake na CHADEMA?
 
yuko chimbo anapakua madude ya "dream liner", kila kitu kitawekwa wazi akirudi, anzeni kujipanga soon lumumba mtaanza kucheza ngoma ya zito
 
Back
Top Bottom