Mkuu wala Akili haitachoka na wala usitegemee hilo kwa sababu mimi naamini Tanzania bora ni ile itakayo weza kuimarisha muungano. Tena ikiwezekana hadi EAC iwe nchi moja kama zilivyo USA au Canada. Tuwe na serikali moja kubwa na nyinginezo ndogo na hakuna mambo yasokuwa ya Muungano. Nguvu ya nchi hizo imetokana na muungano wao ambao kwa ukubwa tu sisi EAC tujumuishe wote pamoja ni sawa na states mbili tu za Marekani au Canada.Mzee Mkandara akili inachoka
Mwandishi wa hii thread ataenda motoni kwa ajili ya uongo wake. ni aibu kuzusha maneno kama haya kwa mtu mzima mwenye ufahamu. lowassa inawezekana hatumpend lakini kiukweli amepata mapokezi makubwa sana mpaka kero kwa watu wengine. huwezi mlinganisha na zitto hata kidogo na hivi sasa ndo naambiwa na huyu mtu kuwa zitto alikuwepo tbr. habar ya mjini tabora ni lowassa kila kona. sisi wengne wa vyama hivi najua tunakuwa tunaumia ila kuna hali inabidi tukubali tu ukweli. jamaa ana watu, ana watu weng sana lowassa kama anawanunua basi ana utajiri kupita wa bill gates. atakuwa nawalipa sh ngap hawa watu zaid ya elfu kumi? jaman kuna mambo tunatakiwa tu tukubali ukweli. jamaa wanampenda .... sijui why.
Mkuu hivi Chadema wako wapi maana naona mada zote humu zinahusu uchaguzi wa CCM inakuwaje? Yaani inafika hadi mnaanza kuamini kuwa Zitto anaifunika CCM!
Niko ndani ya mji wa tabora,nimeshuhudia ushawishi wa mwanasiasa maarufu sana hapa tanzania ndani ya mji wa tabora ndugu zitto zuberi kabwe,hapa mjini tabora bendera za act wazalendo chama ambacho zitto anakiongoza zimetapakaa mji mzima na vijiwe vyote ndani ya tabora ni mijadala kuhusu tukio la kesho kuzindua azimio la tabora,vijana na akina mama wanaonekana kuvutiwa na siasa anazofanya kijana machachali Zitto kabwe,,
Baadhi ya viongozi wa ACT wanaonekana mitaani wakiuza kadi za chama hiki kwa hamasa kubwa sana,hata lowassa alipofika hapa kutafuta wadhamini hakupata mapokeo kama haya aliyoyapata ndugi zitto kabwe.
Kesho jioni kutafanyika mkutano mkubwa wa hadhara wa kuzindua azimio la tabora kitu ambacho kinasubiriwa kwa hamu sana na wananchi wa tabora,hongera mdugu Zitto Kabwe
Taratibu anarejea.....time will tell
Kuna watu hawataki kusikia ukweli kuhusu zitto,hasa chadema,ila zitto ni zaidi ya umjuavyo,ni mwanasiasa makini na anayejiamini,tunaanza nziara kesho,mnyika tangulia kama kawaida yako