Zitto:Bajeti ya madeni na mishahara

Huey P jr

JF-Expert Member
Apr 26, 2015
347
134
Bajeti ya kulipia Deni la Taifa 2016/17 ni tshs 8 trilioni. Ukaguzi wa Deni la Taifa ni muhimu sana kufanyika ili kubaini uhalali wa madeni mengi ambayo Tanzania inalipia hivi sasa. Katika shilingi 100 tunayokusanya kama kodi, tshs 46 tunahudumia deni la Taifa na shilingi 50 tunalipa mishahara ya wafanyakazi wa Serikali. Ina maana Serikali inabakia na tshs 4 tu za kufanya kazi katika kila shilingi 100 ambayo tunakusanya kama mapato.
Kama ilivyo wafanyakazi hewa, kuna madeni hewa. Serikali iruhusu ukaguzi maalumu wa Deni la Taifa ili kubaini uhalisia wa Deni na kuchukua hatua. Vinginevyo hatutafanikiwa kabisa katika juhudi za kuleta maendeleo ya watu wetu
 
Back
Top Bottom