SI KWELI Zitto awashukia wanaharakati walioko ughaibuni

SI KWELI Zitto awashukia wanaharakati walioko ughaibuni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Zitto Sept 17.jpg
 
Tunachokijua
Zitto Kabwe ni mgombea wa ubunge jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo na pia ni kiongozi mstaafu wa Chama cha hicho pia amewahi kuwa mbunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania katika vipindi tofauti.

Madai

Septemba 17, 2025 kupitia kurasa za mitandao ya kijamii kumekuwa na grafiki yenye utambulisho wa chombo cha habari cha Nipashe ikiwa imeambata na inayoonekana kuwa ni screenshot kutoka katika ukurasa wa X wa mgombea ubunge jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe akieleza kuwa kelele za wanaharakati waliopo nje ya nchi hazina tija.

Uhalisia wa madai hayo
Baada ya ufuatiliaji wa kina uliofanywa na JamiiCheck juu ya taarifa iliyowaasilishwa na mdau akitaka kupata uhalisia wake imebaini kuwa si ya kweli.

Ufuatiliaji kwa njia ya maneno muhimu umebaini kuwa taarifa hiyo haijachapishwa na Nipashe wala chanzo chochote kingine cha kuaminika.

Screenshot inayoonekana kuwa ni ya Zitto Kabwe ni ya kughushi kwani ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umejirirdhisha kuwa, Zitto hajachapisha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa X.

Aidha grafiki inayoonekana kuwa ni ya Nipashe ni ya kughushi huku ikiwa na mapungufu kadhaa ikiwemo kutumia aina tofauti ya mwandiko pamoja na mpangilio ukilinganisha na grafiki halisi za chanzo hicho.
Back
Top Bottom