Zitto ataka stars ivunjwe, poulsen atimuliwe..

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
ZITTO ATAKA STARS IVUNJWE, POULSEN ATIMULIWE





KIWANGO kilichoonyeshwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, katika mechi dhidi ya Msumbiji, kimesababisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kutamka kuwa amekerwa na kiwango hicho na kulitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanya maamuzi magumu ya kuvunja timu hiyo.

Stars inayonolewa na Jan Poulsen ambayo juzi ilivaana na Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuambulia sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2013), ilishindwa kuwafurahisha mashabiki baada ya kutoonyesha uwezo mzuri.

Akizungumza muda mfupi baada ya mechi hiyo, Zitto alisema kuwa kuna haja ya TFF kufanya maamuzi ya kukibadili kikosi hicho ambapo kwanza wanapaswa kusitisha mkataba wa Poulsen ambaye ameonekana kushindwa kusonga mbele.
Aliongeza kuwa mbali na kuondolewa kwa Poulsen, pia timu inatakiwa kuvunjwa na kuitengeneza upya kwa kutafuta vijana wadogo kwa kuwa wachezaji waliopo wameshindwa kuonyesha uwezo wa juu.​

"Nimechukizwa sana leo (juzi) na kiwango kilichoonyeshwa na timu yetu, nadhani kuna jambo linahitajika kufanyika haraka na kwa kuanzia TFF waangalie ni namna gani wanaweza kumtimua huyu Poulsen, ni dhahiri ameshindwa kuibadilisha timu," alisema Zitto na kuongeza:

"Pia waivunje hii timu kwa sababu wachezaji wengi wameshindwa kubadilika hali inayowafanya kila siku kuwa na matatizo yaleyale. Kwa hali hii kila siku timu itazidi kutengeneza mashabiki wa kuichukia kuliko wa kuipenda."
 
tanzania tuwekeze ktk riadha italipa!kuna wamasai,wambulu na asili ya ethiopia huenda ikatuokoa
 
Kaka hapo umegusa hisia zangu kwani tangu nimesikia kocha yule wazambia aliomba kazi hapa kwetu na hakuchaguliwa naomba kuongeza, hata TFF nayo ijivue gamba baada ya kufurumusha kocha na timu.
 
zito acha kuongea hivyo naomba ungesema hivi tuandae vijana,tuwe na akademi kila mkoa,tuwapeleke makocha wazalendo wakasome.
 
tanzania tuwekeze ktk riadha italipa!kuna wamasai,wambulu na asili ya ethiopia huenda ikatuokoa

Mkuu, kila siku mimi hua nasema tuachane kabisa na ishu ya mpira, tuwekeze kwenye riadha tuachane na soka maana hakuna tunachoambulia zaidi ya presha na hasara na matusi juu dhidi ya Wachezaji na TFF
 
Kwani kocha wa timu ya taifa ndo anakazi ya kufundisha wachezaji jinsi ya kucheza au ni club zao?! Hata aletwe Ferguson timu itakuwa mbovu tu manake mfumo wa ligi wenyewe mbovu?!
 
kama kauli hii imetoka kwa zitto basi ufahamu wake wa soka ni wa kutilia mashaka!na nimeshangaa pia wachangiaji mmeshindwa kuliona hili!ukweli ni kwamba hakuna kitu kinachoitwa "kuvunjwa timu ya taifa"!timu ya taifa hakuna mchezaji wa kudumu aliyesajiliwa useme eti unavunja timu ya taifa!kocha anaweza kuchagua leo wachezaji wengine na kesho tofauti kabisa na wale wa leo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom