Kwa kuwa tumeamua kupambana dhidi ya rushwa, hongo, ufisadi, uzembe na uvivu;
Kwa kuwa tumeamua kuhakikisha kuwa mali asili ya Nchi yetu Tanzania ni mali ya wananchi wote na kwamba lazima itumike kutokomeza umasikini nchini kwetu na kuleta maendeleo sawia na endelevu ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa;
Kwa kuwa tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na lililo juu ya misingi ya haki kwa watu wake wote;
Kwa kuwa tumeamua kushiriki katika ujenzi wa Umoja wa Afrika ili kuwaenzi waasisi wa ukombozi wa Mwafrika na kujenga kontinenti lenye sauti yenye nguvu na ushawishi katika jamii ya mataifa ulimwenguni;
Kwa kuwa tumeamua kupigania demokrasia, uhuru wa mawazo, umoja, utu, uadilifu, uwajibikaji, uzalendo kwa Taifa na Amani;
Kwa kuwa kwa nia moja tumeamua kujenga chama cha mrengo wa kushoto chenye kufuata misingi ya Demokrasia ya Kijamii (Social Democracy),
Demokrasia ya Rasilimali na misingi asili iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) kama Azimio la Arusha ; na
Kwa wajibu tulio nao wa kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia na utamaduni wa mfumo wa vyama vingi Tanzania;
Hivyo basi..........."
Yes, Chama kinachoasisiwa kwa muundo wa kuwarubuni viongozi wa vyama vya upinzani ni cha kuogopa kama UKOMA.Kwa kuwa tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na lililo juu ya misingi ya haki kwa watu wake wote;.
Upo sahihi anapaswa kuachia nafasi zake kwa kuwa zimetokana na CHADEMA kwa kuwa tayari hapo amekiri kuanzisha ACT.Kwa kuwa kwa nia moja tumeamua kujenga chama cha mrengo wa kushoto chenye kufuata misingi ya Demokrasia ya Kijamii (Social Democracy), Demokrasia ya Rasilimali na misingi asili iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) kama Azimio la Arusha ;
zitto atawachezea sana watanzania wengi hasa wale wavivu wa kufikiri, zitto atawatumia sana vijana wengi hasa wale wasaka tonge na wale wasomi walio weka akili zao mifukoni na kuamuwa kutumika kama dekio
Huyu dogo asiwaumize vichwa kwani kishachanganyikiwa na ndo maana anajidai hatagombea Ubunge kwani ameshanusa upepo na kujua hatima mbaya kwake
Tushatafakari na tushajua uwezo wake.... wewe baki na chama chako
Zito akiondoka atakitikisa chama lakini hataweza kufikia lengo la kuua harakati hizi kamwe! Ataingia kwenye historia ya Mrema na atakwisha kisiasa taratibu.
Katika hali ya Kimungu (yaani perfection) tunasema mtu akifanya mambo mia moja kati yake 95 mabaya alafu 5 mazuri basi tuangalie mazuri na tusahau mabaya ili kumpa moyo lakini katika hali halisi ya kidunia inakuwa kinyume, hata akifanya mazuri 95 bado tutaangalia mabaya 5!mmmmmmmmmm, usianze kuwa na mashaka na vijana wengi, huo ndiyo ukweli kwamba vijana wanamtaka kijana kama ZITTO na si vinginevyo, wewe kama unajijua ni mzee shauri yako manake uzee siyo lazima umri, unaweza kuzeeka hata kwa fikira. Lazima kijana yoyote mpenda maendeleo amuunge mkono ZITTO KABWE.
CHADEMA ni lazima mjiandae kisaikolojia, huyu kijana ni tishio kwa msatakabali wa chama chenu ambacho mwanzoni mlijivua nguvu ya vijana, nguvu ambayo hapana shaka sasa inayumba yumba ikisubiri kuona ZITTO KABWE anaweka wapi mizizi.