Zito,Mkumbo na Wenzake kufanya mkutano na waandishi wik ijayo

Status
Not open for further replies.
Tunawashukuru watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha harakati za mabadiliko. Haya ni mawimbi katika harakati za mabadiliko na ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika mfumo wa demokrasia hapa nchini kwetu. Ninashauri tuwe na subira katika kutoa hitimisho na hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa tumekwisha kupata upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni subira nasi tuseme ndipo mpitishe hukumu. Mungu akijalia tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na tutaeleza upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu. Kwa sasa tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara katika kuhakikisha kwamba siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu katika harakati takatifu za mabadiliko hapa nchini.

well defined
 
Poleni sana kina Zito,

Do not argue with an idiot. He will drag you down to his level and beat you with experience.Lema.
 
Mkumbo hawezi kuwa mpinzani wa chama tawala hata siku moja, kwani historia inaonyesha wazi kuwa ni pandikizi la CCM. Tangu akiwa kiongozi wa wanafunzi UDSM ndiyo style yake, yakuwaonyesha yuko na nyinyi lakini kumbe yuko na wale zaidi. Tangu amejiunga CHADEMA mimi sikuamini yuko pamoja nao. Kifupi kwa mtazamo wangu hakuna mpinzani kati ya Zitto na Mkumbo. Hao wote na mapandikizi. Sielewi CHADEMA walishindwa vipi kuwatambua, wakati mwingine naanza kuamini hata CHADEMA siyo chama cha upinzani.

mkuu umemalizia vyema comment yako hata cc tulijuwa zamani kua chadema ni tawi la ccm.
 
Tunawashukuru watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha harakati za mabadiliko. Haya ni mawimbi katika harakati za mabadiliko na ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika mfumo wa demokrasia hapa nchini kwetu. Ninashauri tuwe na subira katika kutoa hitimisho na hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa tumekwisha kupata upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni subira nasi tuseme ndipo mpitishe hukumu. Mungu akijalia tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na tutaeleza upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu. Kwa sasa tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara katika kuhakikisha kwamba siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu katika harakati takatifu za mabadiliko hapa nchini.
Naamini katika hiki ulichokisema na pia naamini haya ni mawimbi yakisiasa Dr.Kitila Mkumbo maana kumbuka usemi fulani usemao huwezi kung'oa mbuyu au mti mkubwa bila wewe mwenyewe kutikisika..Pia huwezi kung'o mbuyu bila kuua majani na miti midogo iliyoota chini yake juu yake...Always intentions to bring changes reprises by different genre and goes with different names like treason, instigation and a like but if you can withstand such situations without exacerbating you will prove your creamy political..Be wise stay there in CDM and your colleagues ZZK and SM...People are with you all in your good political party CDM.
 
Mkumbo nawashauri mje na stahiri hii: Tajeni mikakati yote na mbinu ambazo CCM wamezifanya kupitia kwenu na watajeni wote waliokuwa wanahusika. Na kwa ushahidi imara mkitaja majina ya waliyokuwa wanawatumia toka CCM. Kwa kufanya hivyo mtakuwa mmerudisha heshima yenu (kutubu) lakini mtakuwa mmeisulubu sana CCM.
 
kama wanataka kukiri na kuwaomba watz msamaha utajuaje

tuwe wapole tusiwahukumu kwanza

Wakiwaangukia Watanzania na kutubu dhambi zao hapo watakuw a wameng'alisha nyota yao.na tutawasamehe. Kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa.
 
Kwani unaogopa nini? Mwache tu aseme.

Anataka kuongea nini alichoshindwa kukisema ndani ya kikao? nashauri akileta longolongo afukuzwe kabisa.kama alishindwa kujitetea ndani ya kikao anataka kujitetea kwa waandishi wa habari ili wamsaidie nini?
 
Mwambie akajitete kwenye Chama Chake huko siyo JamiiForumn.

Nakubaliana na wewe, wamepewa 14 good dyz za kusubmit utetezi wao kwenye vikao halali vya chama. Kuanza kuitisha press conference na kutoa matamko, ni UTOVU WA NIDHAMU na kudhihilisha kushindwa kujitetea ndani ya vikao halali na kuanza kutafuta huruma ya wananchi. Kitila fuata utaratibu wa Chama, ikitokea umeonyeshwa mlango wa kutokea ndipo itisha press conference utapike yaliyokukwama kooni.
 
Yan napata picha ya siasa mufilisi ndan ya chadema ambayo iliaminiwa na wananchi,walaka unaodaiwa wa zitto na wenzake ni dhaili kisemacho ndan ya chadema na uamhuz wa kamati kuu uoneshi mantik katika ukweli wa vifungu vya sheria katika katiba ya chadema chama chenye maamuz ya nguvu ya mtawala si chama cha harakati wananchi tumejua kila kitu!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Taarifa za wenyeviti 18 na wanachama zaidi kutimuka,huu ndio mwisho wa chadema,wasomi wengi wamelaani kukandamizwa kwa demokrasia,

wakiwepo basi hawakustahili CDM...kwani wale madiwani kawasaidia nini, vipi wengin ambao wamechoka sana....?hao 18 km walikuwa kizani bora wabaki humo humo..kwani watajipeleka ktk njaa bila sababu.
 
Akajibu shutuma za kamati kuu na sio kujibaraguza na kutafuta sympathy ya wananchi.

Hawajui tu hao..wanafikiri wakienda kwa media ndio itasaidia. Wajibu shutuma hizo kama walivyotakiwa na kikao halali. Wataongea na media sawa,then what ?..ndio itasaidia nini?
 
Wewe vipi? Sii umeambiwa katika kikao wamekiri kuufahamu mpango huo wa uhaini. Wanachosubiriwa ni kujieleza kwa nini hatua kali za kinidhamu juu yao zisichukuliwe ikiwa ni pamoja na kufukuzwa uanachama. Hiyo ni lugha ya kiofisi elewa wewe!
Na Chadema bado haijawafukuza Chamani ila imewavua uongozi,jambo ambalo ni la kawaida kabisa katika taasisi yeyote. Wanaweza wasifukuzwe uanachama kutokana na kile watakachojibu ndani ya 14 days na wakabaki wanachama hai na wenye nafasi ya kugombea uongozi siku za usoni.
Tatizo hapa ni kuwa maamuzi ya Chadema kwa wanachama wake imekuwa mjadala ndani ya CCM mpaka Naibu Katibu mkuu Taifa wa CCM leo kajitosa. Na kuonyesha kachanganyikiwa eti leo anamsifu Kitila kuwa ni kiongozi mahiri. INACHEKESHA SANA

Mimi ningewashauri mambo mawili: 1. Wawaambie mashabiki wao wa CCM kuwa wanawaponza. Kwa maneno ya akina Mwigulu watu wataamini kweli wahaini
2. Wasiongee na vyombo vya habari hadi watoe maelezo kadiri walivyoelekezwa na chama na chama wakajibu barua zao. Kuongea na vyombo vya habari SI suluhisho kwa tatizo Lao. Kama wataongea itaonesha kiburi Chao na hata haitawasaidia Sana hata kwa wananchi. Na wananchi hawawezi kubadili maamuzi ya kikao halali cha chama.
 
Nukuu ya Kitila Mkumbo Katika Mabadiliko group..

.....|•••••|••••|

Tunawashukuru watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha harakati za mabadiliko.

Haya ni mawimbi katika harakati za mabadiliko na ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika mfumo wa demokrasia hapa nchini kwetu.

Ninashauri tuwe na subira katika kutoa hitimisho na hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa tumekwisha kupata upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni subira nasi tuseme ndipo mpitishe hukumu. Mungu akijalia tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na tutaeleza upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu.

Kwa sasa tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara katika kuhakikisha kwamba siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu katika harakati takatifu za mabadiliko hapa nchini.

Kitila
Anzisheni chama chenu,tuachieni chadema yetu!
Tamaa ya pesa imewaponza!
 
Watanzania makini tunaojua nini kinaendelea nyuma ya pazia,tuna hamu Kubwa yakuwasikia .
 
tatizo la kitilya ni jina alilopewa la MKUMBO anafuata mkumbo hvyo tusimlaumu waliompa jina ndo yamkini hawakujua neno linaumba kwenye masalia alivyotajagwa nikajua pamoja na elimu jina limeponja kichwa
yaani uwezo wako wa kufiri kweli umekomea hapo? Huna hoja ya zaidi ya kuanza kuyuhumu jina. Demikrasia tz bado kwa kweli!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom