Habarini wakuu, langu moja tu naomba kama kuna mwenye ujuzi wa utaratibu gani unaofuatwa kisheria wakati wa kununua kiwanja/nyumba hasa ktk maeneo tata kama dar es salaam,
na JE ni sahihi kuishia serikali za mitaa pekee kuandikishiana na muuzaji?
naomba nifaham kuna ndg yangu ana shida ya kufaham kabla hajafanya manunuzi
nafanya assumption ni uwanja/nyumba kwa matumizi ya residential au apartments au biashara ndogo, pia na assume matumizi ya huu mchakato labda mil 5-mil 50.
ingekua ni investments kubwa kama kiwanja masaki/posta ningeshauri otherwise.
anyway nakushauri vitu vitatu vya kuzingatia
1. legal part-unahitaji mwanasheria akupe taratibu nzima ya namna ya kununua kiwanja uhakiki kiko sawa, aina ya mikatabu ya kununua, namna ya kulipana na vitu kama hivyo. nafkiri wanasheria watakuja kushauri vizuri hapa.
2. technical part
a/ status ya kiwanja/nyumba: unahitaji kuhakikisha umiliki uko clean na kiwanja kiko sawa. how inategemea kama kimepimwa na kina hati basi ni kuhakiki hati wizarani (wanasheria pia hufanya hili) kama hakina hati basi utahitaji land surveyor akupe muongozo namna ya kufaham kama kiko surveyed/not and to what level, kiko within town plan maps or not, kina intended land use, real points za site zinafanana na mchoro na vitu kama hivyo.
land surveyor watakupa muongozo hapo.
kwenye hii sehemu pia unahitaji kufanya utafiti binafsi, ndo nafasi yako kua mzee wa kaunda suit, dadisi majirani, kwa mangi, dalali wawili watatu, mjukuu wa mmiliki nk.
b/ potential ya hicho kiwanja/nyumba:
watu wengi sana hili hua hawafanyi sbb ya kutokujua au wengine kuto ona umuhimu. land as land is a good thing but not useful kama haijapewa thamani yake halisi either kwa mjengo, kilimo au matumizi mengine yoyote. kama una nia ya kujenga mtafute "architect" akupe ushauri kuhusu hilo eneo au nyumba. kama utapata mtu sahihi basi atakushauri vizuri kuhusu advantages na limitations ya eneo lako, sio unanunua uwanja mil 5 kisa nafuu, ila kwenye ujenzi wa nyumba una acha mil 40 kwenye msingi sbb ya slope kali. au ndo scenario kama mafuriko na vitu kede kede. mtafute mtalaamu husika akushauri, please use a recomended architect/ mtaalam wa kilimo kama ni pa kulima.
katika proper investments basi valuers hua ndo wanahusika maeneo kama haya pamoja na economists pamoja na wengineo nk.
kua makini na
-madalali/wa katikati
-usiwe na papara esp kwenye kutoa pesa
-watalaamu nao wasijekukuyumbisha use recomended people.
-usiamini kwenye bahati, viwanja/nyumba viko vingi.