Zinduka tumlinde mtoto wa kiume dhidi ya ulawiti

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
Maisha yanakwenda kasi sana, Matukio mabaya yanachukua nafasi katika jamii, Wanajamii wamejisahau na Madhara makubwa yanaikumba jamii.

Ni miaka kadhaa sasa serikali, wadau mbalimbali wa maendeleo na wanajamii wamefanya juhudi za kutosha juu ya kumlinda mtoto wa kike dhidi ya mila potofu, mila kandamizi na vitendo vya ukatili dhidi yake. Juhudi hizi hakika zimeleta tija katika jamii yetu kwani mpaka sasa uelewa umeongezeka kwa kiasi kikubwa na mtoto wa kike amepata walinzi katika kila nyanja ya maisha yake.

Wadau hawa wamejidhatiti katika kumlinda mtoto wa kike wametoka katika maeneo/ ngazi mbalimbali kitaifa na kimataifa. Kwa hakika juhudi zao zimeonekana. Leo heshima ya mtoto wa kike imerudi kwa kasi kubwa sana. Hongereni Sana!

Wacha sasa ni wakumbushe na kuwazindua wadau wote ikiwemo serikali, Kwanini tumesahau kumlinda mtoto wa kiume? Thamani yake katika jamii ni ndogo?

Kutokana na ripoti na taarifa mbalimbali zinazotolewa na idara zetu za serikali juu ya kukithiri na kuongezeka vitendo vya ULAWITI kwa watoto wa kiume zinapaswa kutuamsha kutoka kwenye usingizi mzito uliopelekea kumsahau mtoto wa kiume katika kumlinda dhidi ya ukatili huu (Ulawiti). Ni dhahiri kuwa jitihada za kumlinda mtoto wa kiume zipo lakini hazijapewa uzito mkubwa kama vile za kumlinda mtoto wa kike.

Kwa taarifa yenu, waharibifu wameshtuka na wameona kuwa kwa sasa jamii inauelewa mkubwa juu ya haki na kumlinda mtoto wa kike wameamua kuacha kabisa na sasa wamehamia kwa mtoto wa kiume, Wanafanya wanavyotaka!

Bila shaka tunapaswa kuliangalia hili kwa jicho la tatu na kulipa uzito mkubwa na bila kufanya hivyo tutaumbuka huko mbeleni.

Tumeona wadau mbalimbali wa maendeleo walivyoweza kushirikiana na serikali katika kumlinda mtoto wa kike kwa kuanzisha miradi mbalimbali katika jamii zetu kwa kutoa elimu ya kumlinda mtoto wa kike. Juhudi zote hizi zimeleta manufaa makubwa na sasa tunayaona.

Ongezeko hili la vitendo vya ULAWITI kwa watoto wa kiume linapaswa kutuleta pamoja wadau wote wa haki za watoto kutambua umuhimu wa kulisemea hili kwa sauti ya juu huku tukipata sapoti kutoka kwa serikali yetu na viongozi wenye dhamana na masuala haya kutoka wizara yetu ya Maendeleo ya Jamii

Tujikumbushe kidogo kitakwimu ambazo zinaonyesha kwa miaka 6 nyuma kuonyesha ukubwa wa tatizo na namna linavyoongezeka kwa kasi kubwa kwa sasa.

1. Mwaka 2016 jumla ya watoto 537 walilawitiwa. Wakiume 487 na wakike 50

2. Mwaka 2017 jumla ya watoto 501 walilawitiwa. Wakiume 442 na wakike 59

3. Mwaka 2018 jumla ya watoto 1,159 walilawitiwa. Wakiume 1,026 na wakike 133

4. Mwaka 2019 jumla ya watoto 1405 walilawitiwa. Wakiume 1,193 na wakike 212

5.Mwaka 2020 jumla ya watoto 1,000 walilawitiwa. Wakiume 885 na wakike 115

6. Mwaka 2021 jumla ya watoto 1,114 walilawitiwa. Ikiwemo Wakiume na wakike.

N:B 87% ya matukio yalifanywa kwa mtoto wa kiume

Kwa takwimu hizi, tunapaswa kujiuliza tatizo la ulawiti katika jamii zetu kwa watoto wa kiume linalopungua na kuongezeka, litatuletea madhara kwa kiasi gani.

Tukumbuke ya kuwa takwimu hizi zimepatikana baada ya kesi za ulawiti kuripotiwa katika ofisi husika (Jeshi la polisi) . Tunaamini kwamba zipo kesi nyingi za ulawiti kwa watoto wa kiume na kike haziripotiwi kabisa, hivyo basi kunalifanya tatizo hili kuwa kubwa zaidi.

Nini kifanyike?

Ningependa kutoa wito wangu kwa serikali, wadau wa haki za watoto na wanajamii kwa ujumla tuamke na tuzinduke juu ya kumlinda mtoto wa kiume. Haya yafuatayo yanapaswa kutekelezwa:

A: SERIKALI
1. Uzingatiaji na utekelezaji wa sheria.

2. Kupewa nguvu kamati za ulinzi na usalama wa mtoto zilizopo katika mitaa, vijiji na kata zetu (MTAKUA)

3. Kuimarisha mifumo ya kuripoti kesi za ulawiti ili kesi nyingi ziripotiwe kwenye vyombo husika

4. Kuzuia mianya ya rushwa kuanzia kesi inaporipotiwa (Polisi, Upelelezi) na inapofikishwa Mahakamani kwajili ya taratibu za kisheria.

5. Wataalamu wa Ustawi wa jamii waajiriwe kwenye ngazi za serikali ya mitaa (Kata), mashuleni ili waweze kutoa elimu na kufatilia kwa ukaribu zaidi juu ya kumlinda mtoto wa kiume.

6. Jeshi la polisi liharakishe upelelezi kwenye kesi za ulawiti na ubakaji ili mahakama zitoe hukumu za haraka ili waharibifu wajifunze kutokana na ubaya walioufanya.

7. Kesi za watoto zipelekwe Juvenile court Ili zipewe uzito mkubwa wa usikilizwaji na utoaji wa hukumu.

B WADAU WA MAENDELEO

1. Kushirikiana na serikali katika kuibua kesi za ulawiti na kumlinda mtoto wa kiume.

2. Kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara ya ulawiti na kuwajengea uwezo katika kuibua chanagamoto hizo.

3. Kuanzisha miradi/programu juu ya kumlinda mtoto wa kiume ambayo itasaidia katika kuleta uelewa kwa watoto na jamii kwa ujumla.

C WAZAZI

1. Kuwa na vikao vya mara kwa mara na watoto ili kuweza kubaini kama wanaelewa juu ya masuala haya.

2. Kufatilia nyenendo za kitabia kwa watoto wetu.

3. Kuwafuatilia watoto wetu mashuleni na hata maeneo mengine ambayo wanakwenda.

D: SHULE , MADRASA & SUNDAY SCHOOL

1. Kusaidia katika kuongea na watoto juu ya madhara ya ulawiti katika jamii.

2. Kutoa elimu ya kiroho juu ya ubaya wa tatizo hili.

3. Kuripoti matukio ya ulawiti katika vyombo husika.

4. Kuwafichua waharibifu ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

5. Waalimu wajengewe uwezo ili waweze kusaidia kuibua kesi hizi mashuleni.

NB: TATIZO HILI NI KUBWA TUUNGANE PAMOJA KATIKA KULITOKOMEZA
 
Wenye watoto wakiume vichwa vinapata moto..miaka 30 haiwatishi...kwanini wasinyongwe tu mzizi wa fitina uishe?? Malezi ya mtoto yapo kwa ngazi ya family. Family mkishindwa basi ujue hakuna ataye kusaidia.

Walawiti wauawe.
 
Wenye watoto wakiume vichwa vinapata moto..miaka 30 haiwatishi...kwanini wasinyongwe tu mzizi wa fitina uishe?? Malezi ya mtoto yapo kwa ngazi ya family. Family mkishindwa basi ujue hakuna ataye kusaidia.

Walawiti wauawe.
Ahsante mkuu huu Uzi ni very important kwa wazazi wote but unfortunately hauna wachangiaji wengi sababu hauna habari za kimalaya
 
You have a big point. I think kuna lagging because of how the system is made. Maana huko polisi mzunguko n mrefu.

Wangeweka straight up kua mtu akikamatwa kwa ulawiti anakula kamba chap, Cases zingepungua.

N kama ilivoekwa adhabu ya kifo kwa wanaoua albino, cases zilipungua kbsa.

Hili suala shida n kwamba wengi wanataka kuyamaliza chini kwa chini.

Pia n muhm kuongeza awareness kwa wazazi maana in most cases watoto wanashindwa kuelezea yaliyowakuta due to parents behaviours
 
Tushauriane basi tufanyeje. Kila siku my boy kakienda shule tu nakuwa sina amani. Natamani nishinde nae mwenyewe. Siamini kabisa kama atakuwa salama huko. Daa sjui hata nifanyeje. Milawiti imekuwa mingi sana huko.
 
Sasaiv mtu wa karibu ndo anaemlawiti mtoto na vitisho vingi kama ingewezekana kampeni za kupinga hili suala ziendeshwe hasa mashuleni coz mtu ambae unategemea awe mlinzi wa mtoto yeye ndo anakua Jangili inaumiza
 
Ikiwa rais kaeakomalia mashoga wasitambuliwe hawa walawiti kwa nini ishindikane?
 
hali inatisha kiukweli mtoto wa kiume hayuko salama kabisa...........serikali ikiamua inaweza kwa kuweka adhabu kali na pia mlolongo wa kesi usiwe mrefu yaani sio mtu anazungushwa polisi hadi kero pia dhamana ingefutwa kwa walawiti na wabakaji.
 
Back
Top Bottom