Zile fedha za wauza bangi, pengine zipo kazini hivi sasa

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Mwalimu Julius Nyerere atabakia kuwa shujaa wangu mpaka siku ya mwisho kabisa ya uhai wangu.

Naikumbuka hotuba yake ya 1995 siku ya Mei Mosi, ilijaa maskhara na ujumbe mwanana kwa Watanzania.

Inakaribia kufikia miaka 22 tangu mwasisi wa Taifa amwage busara zake pale Sokoine Stadium lakini neno lenye hekima na uhai hata siku moja haliwezi kupitwa na wakati.

Katika kuliasa Taifa mwalimu alisema tuwe waangalifu na watu wanaoitafuta Ikulu kwa udi na uvumba mpaka kufikia hatua ya kuweza kutumia fedha za wauza bangi (madawa ya kulevya).

Mwalimu alikuwa akitabiri juu ya Tanzania ambayo imekuja kuukumbatia udhalimu wa wenye mali, ambao wanafikia kiasi cha kutaka maamuzi ya juu kabisa yafanyike kwa faida ya maisha yao.

Hizi pilikapilika zinazoanzishwa na wauza bangi wa karne hii ni matunda ya mchakato wa udhalimu kutaka kubakia kwenye nchi, kwa madhara ya mateso na umasikini wa walio wengi.

Ikiwa wauza bangi wanakuwa na nguvu mpaka za kuhakikisha hukumu za mahakama zetu zinawapendelea wao, wanashindwa vipi kuhakikisha magazeti yetu yakaweka msisitizo katika kuwatetea?.

Ikiwa wauza bangi wanao uwezo wa kupanga nani awe mtu muhimu katika idara gani nyeti ili biashara zao zisidhurike, wanashindwa vipi kuendeleza mapambano na malengo pamoja na mipango ya awamu ya tano?.

Mwezi Mei mwaka huu hotuba ya Baba wa Taifa ya pale Sokoine Stadium inafikisha miaka 22, ni umri wa mtu mzima mwenye kujielewa, lakini onyo lake kuhusu kuepuka fedha za wauza bangi lina umuhimu mwaka huu wa 2017 kuliko wakati wowote ule kabla.
 
Back
Top Bottom