Zile ahadi za kuoana mnazowekeana na first love, ni wangapi walizitimiza?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,732
215,909
Habari za leo wapendwa,

Wengi wetu mpaka tumefika form six ndiyo unapata first boyfriend na ahadi kibao, wakati huo hujajua chuoni utapangiwa wapi, mawasiliano Enzi zile hayakuwa kama yalivyo sasa hivi, barua unasubiri wiki mbili, mobile zilipoingia kupiga simu ilikuwa gharama sana tuliishia mwendo wa kutext, whats up ilikuwa ni ndoto ya mchana.

Nilikutana na dada mmoja yeye na mume wake walifanikiwa kutimiza ahadi waliyopeana shule, jamaa alianza kubangaiza alipowin maisha tu alilipa mahari na walianza kushi pamoja na sasa wana watoto, ndoa ya kanisani walifunga baadae sana.

Kwa wengi ahadi zile hazitimii kutokana na hali ya uchumi, wakati huo kijana bado anatafuta na mdada anakutana na mtu ambae ni already made, ukiangalia yule aliyekuahidi bado anaishi kwenye chumba, hajui hata kesho itakwenda vipi, mkaka anakutokiea ana ka usafiri, amepangisha nyumba nzima Sinza, unafikiria maisha. Ni wachache wanaokuwa na subira kwa kweli.
 
Wanaokua na subira ni wachache mno,na ukimpata wa hivo aliekuvumilia hivo ni mke huyo si wakuacha
 
Habari za leo wapendwa,

Kwa wengi ahadi zile hazitimii kutokana na hali ya uchumi, wakati huo kijana bado anatafuta na mdada anakutana na mtu ambae ni already made, ukiangalia yule aliyekuahidi bado anaishi kwenye chumba, hajui hata kesho itakwenda vipi, mkaka anakutokiea ana ka usafiri, amepangisha nyumba nzima Sinza, unafikiria maisha. Ni wachache wanaokuwa na subira kwa kweli.

Ni kweli kabisa mkuu, hapo huwa ni changamoto sana. Mdada akifkiria maisha ni rahisi sana kushawishika hapo
 
Hiyo ni kweli kabisa mkuu, hata mpenzi wangu wa kwanza ilikua ni case exactly kama hii
Kesi kama hii inabidi muweke mapenzi kwanza, hamjali maisha mtakayoishi, kuna best yangu mmoja, jamaa ametuma mshenga kwao anataka kulipa mahari, baba mkwe kwa dharau sana akasema "hivi yule ndiyo anataka kuoa mtoto wangu". Demu aliposikia maneno hayo alibeba mimba ya jamaa.
 
Ahadi za ndoa tena? Changamoto iliyopo ni kukosekana kwa links. Unaweza kuwa ulimpenda mtu baada ya form six ukaenda chuo ukampata mwingine si kwa sababu hukumpenda wa nyuma bali nyakati hulazimisha uanze mwanzo mpya.

Una maliza chuo unapatwa na majanga ya kutafuta kazi na mengine. Uliyedate nae chuo akikutangulia kuwa na account inayosoma unalazimika kuachia ngazi. Sio kwa sababu humpendi bali unajikuta umelose balance of power and ghafla you don't fit her cycle.

Mwisho wa siku unapopata ramani na kuwa tayari hawa wa nyuma huwa wanakuwa si type yako tena aidha wana higher limits au very low limits kuliko unavyoona inafaa.

It just ends that way. Binafsi hizi ahadi zimenishinda toka form six hadi chuo. Ndio nipo mtaani nataka kuona kama ntaweka ahadi mpya.
 
Kesi kama hii inabidi muweke mapenzi kwanza, hamjali maisha mtakayoishi, kuna best yangu mmoja, jamaa ametuma mshenga kwao anataka kulipa mahari, baba mkwe kwa dhara sana akasema "hivi yule ndiyo anataka kuoa mtoto wangu". Demu aliposikia maneno hayo alibeba mimba ya jamaa.
Hahahahaa, ni wachache sana wanaweza fanya kitu cha kishujaa kama alichofanya huyo demu. Ila wanaume wengine huwa wanakuja kuzingua baadae, unakuta demu anamvumilia jamaa tangu chini akiwa hana chochote, ila akija kushika pesa anabadilika
 
Ahadi za ndoa tena? Changamoto iliyopo ni kukosekana kwa links. Unaweza kuwa ulimpenda mtu baada ya form six ukaenda chuo ukampata mwingine si kwa sababu hukumpenda wa nyuma bali nyakati hulazimisha uanze mwanzo mpya.

Una maliza chuo unapatwa na majanga ya kutafuta kazi na mengine. Uliyedate nae chuo akikutangulia kuwa na account inayosoma unalazimika kuachia ngazi. Sio kwa sababu humpendi bali unajikuta umelose balance of power and ghafla you don't fit her cycle.

Mwisho wa siku unapopata ramani na kuwa tayari hawa wa nyuma huwa wanakuwa si type yako tena aidha wana higher limits au very low limits kuliko unavyoona inafaa.

It just ends that way. Binafsi hizi ahadi zimenishinda toka form six hadi chuo. Ndio nipo mtaani nataka kuona kama ntaweka ahadi mpya.
Mkuu haya unayosema ni kweli kabisa, mkiachana baada ya muda kutokana na circumstances za maisha mnajikuta hamfit in tena wanasema you are no longer compatible. Maisha yaacheni yaitwe maisha.
 
Back
Top Bottom