Zika mwenyewe mwanao

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,850
Reaction score
9,423
Kuna binti wa miaka 24 amekuwa mjeuri sana. Mpaka siku moja mama yake akaniita kuongea naye. Huyo Binti akaniambia "YA KWAKO YAMEKUSHINDA ACHANA NA MIMI SITAKI MAMBO YA KISE......,
Akanipasha hasa. Nikamsihi sana.
Akaniambia nimkome. Mpaka akaniambia kama unataka nikuonyeshe mimi ni nani Nitamchukua mumeo ndo unijue unifuate vizuri.
Mama yake akasikitika sana.
Nikamwambia Muombee tuu.
Mama wa huyo Binti anafanya kazi za kuuza sokoni. Na hapo mama yake kamsomesha mpaka form 4. Akafeli. Akampeleka chuo cha Secretary akafeli ndo akaanza huo upuuzi.
Hamjali mama yake wala hasaidii kazi za ndani.
Yani ataamka mama atapika chai atakunywa na hataosha hata kikombe.
Na atajipodoa ataondoka. Hataosha hata kikombe wala kufagia. Mume wa huyo mama naye ni mlevi hatarii. Akipata pesa anampa mtoto huyo mpuuzi anunue vyakula ndani. Akipewa elfu hamsini anatumia 45. 5 ndo ananunua vitu ndani.
Sasa akapewa laki mbili na baba yake. Alipe ada ya mdogo wake.
Akasepa na hizo pesa tangu mwaka jana january.
Hapigi simu kwa mama. Ila kwa baba anapiga simu.
Akapata mimba.
Akajifungua. Maisha yakampiga hasaaa. Alikuwa dodoma. Yani maisha yamempiga vizuri.
Sasa huyo mtoto anaumwa nafikiri kukosa matunzo ya uzazi. Na mtoto wake akaumwa sana. Mtoto amefariki.
Yuko Dodoma.
Akatuma ujumbe anaumwa hakuna aliyeenda. Maana haongei na mama yake. Ni baba tu.
Sasa katuma taarifa mtoto wake kafariki.
Mama akamwambia Zika tuu mwanangu. Pole na msiba mwanangu. Pole sana. ZIKA TU MAMA.
Huyo Binti akanipigia Simu kunililia nimsaidie.
Nikamwambia hali ya mama yako naifahamu kiuchumi.
Kusafirisha huo mwili mpaka Arusha sidhani kama ataweza. Nikusihi Uzike. Kisha nitakupa Nauli.
Urudi nyumbani baada ya Mazishi. Upeleke msiba nyumbani.
NIMEKOSEA AMA NIMEPATIA?
Binti analia anasema mama yake hana uchungu naye eti kwa nini aseme
"Pole Mwanangu zika tuu."
Najua Binti ana makosa.
Ila nimeona sasa hivi sio muda wa kumgombeza maana ana Uchungu huo na haitasaidia.
Ila baada ya msiba huo ndo unaweza kujua
Anafaa kugombeza ama anafaa Kushauri ama Kuonya.
Mama nimempigia simu yuko sokoni. Namwambia msiba ananiambia MUACHE AZIKE TU IRENE.
Hembu sema lolote.
Litanisaidia baada ya Matanga.
Maana nitapata nafasi ya Kuongea nao wote
irene Mbowe
 
Irene mbowe..mbona nalijua hili jina..

Umeshauri vizuri hujakosea..wanakwambia "usipofunzwa na mama yako utafunzwa na ulimwengu'
 
Azike tu kwani yeye anataka nn?!
 
bimecheka aliposema atamchukua mme wako. Kuna binadamu wanamajibu ya hovyoo mpe pole mwambia asijali ni sehemu ya maisha kuanguka then unasimama maisha yanaendelea

r.i.p mtoto
 
Usijihusishe kabisa na huyo binti achana naye hana adabu, ukimtumia pesa alete msiba nyumbani atakuja msumbua sana mama yake maana hadi sasa hajaona kosa alilomfanyia mama yake hivyo akifika huko ni kulipiza kisadi kwa like jibu la mama "zika tu" kaa mbali tafadhali yule Mtoto ana laana ya mama yake sio bure. Halafu Dodoma kuna mdudu anatembea ni ajabu, "RAV 4" imewapenda hakuna mwembamba hivyo sio rahisi kutofautisha akacheki afya yake tu huo ndio ushauri unaotakiwa kumpa na si kumtumia nauli
 
Duh hapo kwenye Irene na Arusha nikajua ni Irene yule demu wangu wa Mbauda wa enzi hizo tupo skuli. Ila ulipomalizia Irene Mbowe nikasema ehuuuu kumbe siye.
 
msiba ukimalizika, usimshauri chochote mpaka atakapoanzisha mazungumzo yeye mwenyewe ili ujue akili yake iko positioned vipi kuhusu aliyokuwa anafanya na outcomes zake amejifunza nini, then from there you will orient her mind towards it. lakin ukianza kuyaongelea wewe utakuwa umevaa U-yeye which wont help that much
 
Hivi watu wanapata wapi nafasi ya kubishana na mama...wazazi ni Jannah
 
Asante kwa Ushauri muruwa
 
Duh hapo kwenye Irene na Arusha nikajua ni Irene yule demu wangu wa Mbauda wa enzi hizo tupo skuli. Ila ulipomalizia Irene Mbowe nikasema ehuuuu kumbe siye.
Nimekuzuga tu na jina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…