Zijue sifa za mke mwema

Andie

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
712
Reaction score
1,643
Umuofia kwinu !!

Nina hakika kila mmoja hapa amepata kusikia "MKE MWEMA HUTOKA KWA MUNGU" na pasina shaka wengi wana ushuhuda kwa jambo hili. Na kwa muendelezo wa mantiki hii MUNGU wa mbinguni akatupatia utashi wa kutambua mke atokae kwake na wafuatao kuja kwako HAWAJATOKA KWA MUNGU. HAKUNA MKE MWEMA HAPA:

1. MDOLI GIRL.
Mwenye bandia, kope bandia, kucha bandia, ngozi kajichubua. Mungu hawezi kukupa mke fake huyo hajatoka kwa Mungu na madhara ya kua na mke wa namna hii ni kubwa mno
(a). Hana nidhamu, kama Mungu kampa kope ila ananyoa na kuchora mstari kwa penseli wewe unadhani kipi utampa atakithamini ?

(b). Maisha fake, hakuna uhalisia ni mtu wa kuiga na kujikweza na kwa hakika maisha yako yatagubikwa na matata lukuki.

(c) Hawezi kuridhika kwa jambo lolote na wanawake hawa hupenda kufanya mambo ya kijinga. Huyu hajatoka kwa Mungu. mke toka kwa Mungu ni mrembo ila alisi. (Beautful and natural)

2. DEGREE GIRL.
"Mimi ninajielewa" (Japo sio wote) ila asilimia kubwa ya wanawake wenye vijielimu ni wajeuri na wajuaji kupita maelezo. Na hao walijipatia degree kwa kupanua mapaja na kupewa marks tuite "mapaja wazi warks" Mungu hawezi kukuletea mwanamke mjuaji kwa sababu amekutaka uwe kichwa cha familia mwanamke mjuaji atataka mwende sambamba na ikiwezekana usukani ashike yeye. Mke toka kwa Mungu ni msikivu kwa mumewe.

3. DADY'S GIRL.
Ushakutana na mwanamke maneno mawili "dady hua ananiletea bla bla bla .... " "dady hua ananipeleka bla bla bla .... " mdogo angu kimbia hakuna mke hapo hawa huwa ni maqueen wa drama. Atakuletea huzuni kila kitu utachofanya kwake kina mapungufu na hawana shukrani kabisaa Mungu hawezi kukuletea mke wa namna hii labda Mungu wa Kalumanzila. Duniani tunajulishwa kuna wana wa Mungu bila shaka kuna wana wa shetani pia.

4. LAZY GIRL.
Umeshaona pembezoni mwa barabara kuna vibanda wanawake wanaoshwa miguu na wanaume ?! Usioe hiyo mbuzi, kama mwanamke hawezi kuosha mwili wake mwenyewe itakuaje kwa malezi ya watoto ?! Aina hii ya wanawake ndio siku hizi hata kuzaa hawataki kupitia uchungu wanalipa pesa wafanyiwe upasuaji, hawanyonyesi wanampa mtoto maziwa ya kopo, mtoto akijisaidia wanaruka kando wanamuita "dada wa kazi" aje kumsafisha mtoto wao hawawezi kushika uchafu. Mke toka kwa Mungu ni hodari wa majukumu yake.

5. SODOMA GIRL.
Mwanamke anayependa kupiga picha kama wanasiasa wanavyopenda kusema uongo na kila picha kabinua makalio juu sura inaonekana nusu upande ila kalio lazima lionekane katikat kila pose kila picha hapo hajavaa chupi ila kavaa kikuku, katoboa pua na akitembea lazima achezeshe makalio yani kiufupi cha muhimu kwake ni makalio. Kwake makalio yana thamani kuliko ubongo, Hapana huyo mke katumwa na utawala wa Shetani, shetani wa mguu mmoja sio Mungu. Mungu anaekutakia mema daima hakika hawezi kukupatia balaa. Mke toka kwa Mungu atajisitiri maungo yake kwa adabu.

6. COMANDO GIRL.
Unaweza kuwaita feminists "Whatever a man can do a woman can do it better" hebu subiri like seriously ?! Kuna mwanamke anaweza kwenda vitani ?? Hawa wanawake wanaojifanya wao ni hodari na hata kukashifu wanaume kaa nao mbali ukioa mwanamke wa hivi umejitafutia vita. Hautapata amani ni mashindano ngebe kucha kutwa, siku, wiki, miaka. Kuna jamaa staff mwenzetu alipelekwa mahakamani na mkewe kwa sababu za kijinga hao ndio macomando girl wao furaha yao ni kupambana na wanaume hakuna jinsi Mungu atakupatia balaa hili mke toka kwa Mungu ni mtiifu.

7. PUBLICITY GIRL
Anafahamiamda na wanaume kila mtaa. "Mimi sipendi urafiki na wanawake, marafiki zangu ni wanaume" ooh kaa mbali na hii laana mwanamke asiyependa kukaa na wanawake wenzake anakipi hasa cha kujiusisha na wanaume kila mtaa ?! Oya acha ujinga achana na hiyo malaya utakuja kujuta.

8. MONEY MONEY GIRL.
Ushawahi kukutana na mwanamke mda wote anawaza atapata wapi pesa, tena pesa nyingi ?! Furaha yake siku zote inategemea kama ana fedha au laah, akiahidia fedha atajichekesha wewee, hakomi kuomba omba watu pesa hata kama hana uhitaji wa pesa ulafi wa fedha umejaa kila chemba ya mamazo yake. Mdogo angu ukishupaza shingo ukaoa mke wa namna hii tutakuzika baada ya kupitia maisha ya ajabu. Mwanamke wa namna hii hatosheki na fedha hata umpe kiasi gani, atafanya lolote kupata pesa ataweza hata ikibidi kuwadhuru wengine ikiwemo wewe ili apate pesa. Mungu wa Mbinguni hawezi kukuletea mke wa namna hii, Mungu atakupa mke mwenye kiasi.
 
aaaah jiumbie wako😏😏😏 tukose kupitia njia hata moja wapo hapo kisa mwanaume wa kukuoa ambae anaewajaza kwenye behewa moja kutwa kubadirisha atakavyo mxiiiiiuuu😣😏
 
👏🏻👏🏻👏🏻👏🏻✍🏻✍🏻✍🏻 hawautaki ukweli.
 
Mithali 31:10-31
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁰ Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
¹¹ Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
¹² Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
¹³ Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
¹⁴ Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
¹⁵ Tena huamka, kabla haujaisha usiku; Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao.
¹⁶ Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
¹⁷ Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
¹⁸ Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
¹⁹ Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
²⁰ Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
²¹ Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
²² Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
²³ Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
²⁴ Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
²⁵ Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
²⁶ Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
²⁷ Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
²⁸ Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
²⁹ Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
³⁰ Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.
³¹ Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…