Zijue sababu kuu za ajali za magari barabarani

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,423
13,935
Ajali za magari barabarani zinatutia hasara kubwa za aina mbalimbali kwa taifa, makazini, familia, matajiri wa magari na kwa ndugu na jamaa za wahanga wa ajali hizo.

Utafiti wangu nilioufanya kuhusiana na ajali hizi nimegundua kuwa sababu ya ajali hizi sio ubovu wa magari, barabara wala mwendo kasi wa magari. Bali kinachosababisha ajali nyingi ni usingizi na uchovu wa madereva wawapo barabarani.

Chanzo kikuu cha usingizi wa madereva ni kushiba kupita kiasi na kuendesha gari hapohapo. Kisayansi mtu akishiba inasababisha damu nyingi kuhamishwa kutoka sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kichwani/ubongo na kuelekezwa tumboni na kwenye ini ili kwenda kupokea na kusambaza chakula kutoka kwenye utumbo na ini kwenda sehemu nyingine za mwili.

Kitendo hiki kinasababisha upungufu wa sukari na hewa kichwani/ubongo hivyo kumfanya mtu ajisikie usingizi muda mfupi tu baada ya kula chakula kizito na kingi. Dereva anayesinzia atakosa umakini barabarani.

Siku hizi wafanyabiashara wa migahawa na hoteli zilizoko kandokando ya barabara kubwa (high ways) wamebuni mtindo wa kuwarubuni madereva hasa wa magari ya abiria wasimamishe mabasi yenye abiria wao kwenye hoteli zao kama sehemu ya kuwaletea wateja.

Madereva wanaokubali kuingiza magari yao huwa wao wanapewa chakula cha bure pamoja na posho ya fedha hivyo kuwafanya wale na kushiba na kusinzia sana njiani. Mbali na kuegesha magari na kupewa misosi ya bure hotelini pia wanapewa vyakula snacks za bure na wafanyabishara wanaopandia njiani kwaajili ya kuuza bidhaa zao ndani ya mabasi.

Hivyo ajali nyingi huwa zinatokea wakati dereva akiwa amelala.

Elimu kwa madereva itolewe kuhusu uhusiano wa mlo mzito na kulala.
 
Ajali nyingi
Uzembe wa dereva wa gari lililopata ajali au dereva mwenzake
Ubovu wa gari
Ubovu wa barabara
Kutokuwepo kwa alama za barabarani
 
Ajali nyingi
Uzembe wa dereva wa gari lililopata ajali au dereva mwenzake
Ubovu wa gari
Ubovu wa barabara
Kutokuwepo kwa alama za barabarani
Waswahili hawasomi alama hata kama zipo. Mlango umeandikwa PULL/VUTA yeye an PUSH/SUKUMA
 
Back
Top Bottom