Zijue nguzo kuu 5 za Hip Hop

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
Katika maisha yangu kwa Bahati nzuri pia nimekulia Katika Familia na mtaa wa HIP HOP Tanzania.Huenda wengi wakashindwa kujua na kudhani Deadbody ni mbana pua.Ni kunivunjia heshima sana kunipeleka mimi kwenye shoo za wabana PUA na haitotokea kamwe.

Nikienda FIESTA huwa sina TIME na anaoimba(wanabana PUA) hata kidogo,yani kwa kifupi moyo wangu umejaa na hip hop.

Nimekulia HOTPOT FAMILY mtaa wetu fulani hivi unaitwa KARAKATA na hapo ndio ilikuwa sehemu yangu ya KWANZA kujifunza kidogo HIP HOP.Wakina SUMA G ,Soggy Dog walinipandikizia Mbegu ya HIP HOP ambayo imeota mpaka leo hii napoandika thread hii Deadbody nakukimbia Harufu ya HIP HOP.

Hakika kizazi cha HIP HOP Tanzania nimekishuhudia Kuanzia KU CREW wakina KIBACHA,CHIEF RAMSO,Y-THANK ,D ROB,K SINGLE na engine kibao wanangu wa UPANGA-EAST.
kwanza-unit-future.jpg

kwanza-unit2bc.jpg

Kwanza-Unit.jpg


(Hawa ndio KU CREW)

IDEA ya HIP HOP niliyopandikizwa na KU CREW nikiwa mdogo zaidi ndio imenifanya Deadbody leo niwe miongoni mwa wanafamilia ya TIP HOP fans Duniani.

Harakati zangu za kufuatilia muziki wa HIP HOP zilidumu zikizidi kuwa Imara kiasi kwamba nyimbo yoyote ya HIP HOP iliyokuwa inatoka maeneo ninayoishi ni lazima niijue kuiimba kwa ufasaha tena Ki HIP HOP zaidi.

Nimeshuhudia VIDEO ya DKNOB 2003 -Elimu mitaani ikiwa ina rekodiwa mitaa ya uwanja wa ndege mtaa ambao tulihamia hivyo nikawa mwana Familia "Mitaani Most wanted"

Hivyo napoandika Thread Hii Deadbody naiandika nikitokea UKONGA aka home of TAMADUNI muziki(Home of freestyle Tanzania).Hakuna mtu anayeweza kubisha ninaposema HIP HOP kwa TANZANIA imehamia UKONGA.Kwakifupi karibuni sana UKONGA

Ila maisha tuliyojijengea hapa duniani ni kuwa kila sehemu kunawekwa sheria kulingana na mahitaji ya jamii husika.Pia hata kwenye masomo pia kuna sheria zake ambazo unapaswa kuzifuata ili kumudu uhusika katika somo hilo.Hahahah hapa wanangu wa PCM,PGM,PCB na wengine huko mnanielewa vizuri kuwa kuna principles nyingi mno ili kuishi katika hayo masomo

Yah,kwa kifupi masomo yote yana principles zake ,hata wale wanaosomea kitandani wanasheria zao ikiwemo kulala saa 2 usiku(Hahahaha hapa sipo serious msije mkani-mind).Kwa kifupi pasipo sheria hakuna kitu kinachoweza kufanikiwa kwa ufasaha zaidikwenye jamii.

SASA LEO HII DEADBODY NAWALETEA UZI HUU KUKUFAHAMISHA KUWA HIP HOP INA NGUZO KUU 5 TU(5 PILLARS OF HIP HOP)

Nguzo hizi za Hip Hop ni hizi hapa:

  • Break dancing
  • Mceeing (Msanii wa Hip Hop)
  • Graffiti writing
  • Djing
  • Knowledge
1.GRAFFITI WRITING
upload_2018-1-15_10-4-45.png

Hapa tunapoongelea GRAFFITI WRITING(uchoraji) katika Hip Hop huwa tuna maanisha kuwa katika kufikisha Ujumbe wake kwa jamii HIP HOP pia huweza kutumia hata michoro katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii.

Nguzo hii ya HIP HOP usiseme kuwa hujawahi kufanya katika maisha yako,hii by default kila mmoja wetu humu JF kwa namna moja ama nyingine ameitumia katika kufikisha ujumbe wake kwa watu fulani .
SPLGHod.jpg


Mfano tulipokuwa shule za msingi na Secondary tuliitumia sana nguzo hii kufikisha ujumbe wetu kwa jamii.Nikiuliza humu JF ni nani hasa hakuwahi kuchora darasani Kuwa "Usiyempenda kaja" au msemo wa aina yoyote ule katika meza au kiti ulichokalia unaweza ukamkosa mtu huyo.

Ile kwenye Hip Hop ndio tunaita Graffiti hivyo tunaposema Hipo Hop ni maisha tunamaanisha kuwa ulikuwa katika maadili ya Hip Hop pasipo kuja kuwa ile ni Hip.

Mara ngapi tukiwa darasani huko sec na primary tulimwandika vibaya mwalimu mnoko ubaoni ili akija asome ? Hiyo ndio ilikuwa nguzo hii ya Hip Hop

Ujumbe kama huu tuliweka ubaoni ili muhusika akija aone "Mwalimu TUMBALO ngoja tukifunga shule utanitambua " hahahaha wale wa shule ya Msingi Minazi mirefu kitambo hicho nadhani sentensi kama hii sio ngeni kwako .
13_meitu_1.jpg


Lengo la Ujumbe huu ni kufikisha ujumbe tu kwa muhusika.Na hiyo ni HIP HOP na ilifanywa na watoto tu wadogo ambao hawakujua kuwa ile ilikuwa na Nguzo ya Hip Hop.

Wale wanaume wenzangu wa DAR nadhani ile misemo ya pale njia panda ya shang'ombe kuelekea KARUME machinga COMPLEX mnaijua vizuri sana.Ile iliandikwa tu na wahuni ikiwa na lengo la Kufika ujumbe kwa jamii husika (Sisi wanaume wa Dar)...

Moja ya msemo uliopo pale ni huu "Imagination is better than Knowledge "

Hizi ndio tunaita GRAFFITI katika HIP HOP
9yNgXgt.jpg


Pia ni mara ngapi tumeshuhudia kwenye vioo vya nyuma vya magari mashafu yameandikwa maneno haya "Nioshe " au bonge la tusi hahahah ile ndio hip hop na naposema FRAFFITI nakuwa namaanisha hata hiyo


wVSbPGA.jpg


Siku nikienda kutembelea ofisi za JF nitatafuta mkaa nyuma ya jengo nitaandika "DEADBODY CAME HERE" hahah Ndio HIP HOP hiyo

2.DJing (Hapa namuongelea DJ)

Hii pia ni nguzo ya Hip Hop imara sana na ndio husimamia ubora wa Muziki wa Hip Hop.Sisi watu wa Ukonga Tunamwelewa sana DJ Manywele..

Vionjo vyote vitamu vya muziki anakabidhiwa huyu DJ.

Sasa ndio umkute DJ mzuri anakupa beat zuri kama hili utambae nalo ndio utazidi kuiona radha ya Hip Hop



Shule ya msingi kuna wale wapiga Ngoma wa shule(band) na ndio maDJ wetu wale..Hahahaha walikuwa kwenye hii nguzo bila kujua.Yani kwa kifupi hata serikali inaspoti sana HIP HOP.

Watoto wale wamekuwa na nguzo hii ya HIP HOP pasipokujua .

Hivyo tunaposema HIP HOP ni maisha muwe mnaelewa basi

coversteevcooldj.jpg


Huyu sasa DJ ndio mtengenezaji wa Muziki wa HIP HOP.Hii ndio sanaa ya kutengeneza Hip Hop Music
DJ-Huarache.jpg


Mfano wa Dj pia huyu:
dj-promote-hip-hop-interview.jpg


Nadhani wanaJF naoandika DJ mnanielewa sana maana hakuna mtu humu hajawahi kusikia au kuona hata picha ya DJ au kujua kinachofanyika kwa DJ.

3.MC (Msanii wa HIP HOP)

Huyu ndio anayeimba Hip Hop sasa..
Kunatofauti kati ya MC na rapa ila sasa hapa sio mahali pake kuijadili hii(Ukiihitaji nitaifungulia uzi wake)

Mfano wa Hip Hop MC ni kama FID Q,Deadbody,JCB,JAY Z,YOUNG JEEZY,NAS na wengine kibao aiseeeee(Wengine wa JF wapo kwenye ileee thread )

Hii ni picha MC akiwa stejini

underpressure7-1000x600.jpg


Hata tulipokuwa watoto tulichana sana mistari japo hatukufahau kuwa ile ilikuwa HIP HOP

HOT-articleLarge.jpg


Wale kizazi changu ngoja niwakumbushe kidogo
(Moja mbili tatu ,akili zako fyatu kama soli ya kiatu)

Dah noma,ilikuwa Hip Hop hiyo na tuliifanya tukiwa wadogo tena bila kujua kuwa ilikuwa ni Hip Hop.

WCPO_cover_0703Jam36_1467632643951_41688122_ver1.0_640_480.jpg




Hivyo tunaposema Hip Hop ni maisha tunakuwa tunamaanisha ulizaliwa ukiwa MC na utakufa Ukiwa MC,yani kwa kifupi umekluliwa katika Hip Hop.

4.DANCE

1tNk8Ll.jpg


Hii ni nguzo ya Hip Hop,kwenye Hip Hop tunaimba na pia tunacheza .Hip Hop ni kinyume cha wasabato ambao wakiimba nyimbo zao za dini hawaruhusiwa kucheza ila kwenye hip hop cheza hata ukivua hadi nguo ni fresh.Wanangu wa Chuga mpooooo(Ukitoa UKONGA kwa hip hop wanafuata CHUGA)

Hip-Hop-Dance-hip-hop-dance-25416681-450-577.png


Wee ruka utakavyo kwenye hip hop ila uagane na nyonga kwanza.Hii ndio HIP HOP.Kucheza kwenye Hip Hop unaruhusiwa kucheza kwa style yoyote ile hata kutikisa tu kichwa nayo ni support kubwa sana kwetu wana HIP HOP .

Wale watoto waliocheza namimi zamani hizo huko karakata wanakumbuka kuwa tulicheza sana Aidama yoyoyooo tena mmoja anatoka mbele anacheza huku wengine tumekaa tunamuangalia na kimaliza anafuata mwingine.Hiyo ndio Hip Hop na tunakushukuru wewe mwanaJF ambaye ulisapoti HIP HOP kwa namna hii pia.
harlem-shake-hip-hop-dance-moves.jpg

Kama uliweza kucheza bilinge bayoyo kipindi kila na sasa unasoma uzi huu inaashiria kuwa umeishi katika HIP HOP muda wote huu mpaka dakika hii.

Vijana wa Arusha Aka A-TOWN napoongelea Ngareloooo wananipata vizuri kabisa.Kama hujawahi kujimix A-town hapa lazima utoke KAPA
upload_2018-1-15_7-34-23.png

upload_2018-1-15_7-35-39.png



Pia nisije kusahau kuwa kwenye Hip Hop hata ukitikisa mikono ni sapoti kubwa sana katika Hip Hop.
upload_2018-1-15_7-37-26.png


5.Knowledge (Ujumbe)

Kama ilivyodhana ya Fasihi ni kufikisha ujumbe kwa jamii hivyo Hip Hop kwa kutumia Nguzo hii nilizokwisha zielezea ni katika kufikisha Ujumbe wake kwa jamii.

Uzuri wa Hip Hop huwa hatuna muda wa kupoteza kama wale wengine,yani kwenye Hip Hop kila neno ni ujumbe tosha na unapaswa kulegeza akili ili kulielewa ipasavyo kama ilivyokusudiwa na MC.

MC anaweza kufika ujumbe unaohusu UKIMWI nk katika jamii anayoizunguka.Hivyo tunasema Hip Hop inaishi mileleeee



SENGWILE MAKAMANDA
DEADBODY
JAMIIFORUMS
 
5.Knowledge (Ujumbe)

Kama ilivyodhana ya Fasihi ni kufikisha ujumbe kwa jamii hivyo Hip Hop kwa kutumia Nguzo hii nilizokwisha zielezea ni katika kufikisha Ujumbe wake kwa jamii.

Uzuri wa Hip Hop huwa hatuna muda wa kupoteza kama wale wengine,yani kwenye Hip Hop kila neno ni ujumbe tosha na unapaswa kulegeza akili ili kulielewa ipasavyo kama ilivyokusudiwa na MC.

MC anaweza kufika ujumbe unaohusu UKIMWI nk katika jamii anayoizunguka.Hivyo tunasema Hip Hop inaishi mileleeee



SENGWILE MAKAMANDA
DEADBODY
JAMIIFORUMS

Mkuu nimekuelewa vilivyo, hapo kwenye "Knowledge" umenikumbisha mstari mmoja alichana Lord Eyez wa Nako 2 Nako, anasema:-

Hip hop ni Knowledge, Nako 2 Nako ni College...!
 
Hahahaha!....niga! .niliumia sana pale nas alipotoa hip hop is dead!!!.....yaani hip hop ilitutawala mpka sasa nikihtaji msaada kwa mtu bas lazma nimalizie okoa hip hop ....!... Mpka bi mkubwa anajua huwa na maanisha nn .....hata washkji zangu waktaka msaada yaani akinambia mwanangu kwahyo unaacha hip hop izame? ....yaani ntahangaika mpka nimsaidie kisa nisionekane nazamisha hiphop
 
Hahahaha!....niga! .niliumia sana pale nas alipotoa hip hop is dead!!!.....yaani hip hop ilitutawala mpka sasa nikihtaji msaada kwa mtu bas lazma nimalizie okoa hip hop ....!... Mpka bi mkubwa anajua huwa na maanisha nn .....hata washkji zangu waktaka msaada yaani akinambia mwanangu kwahyo unaacha hip hop izame? ....yaani ntahangaika mpka nimsaidie kisa nisionekane nazamisha hiphop
Mkuu HOKOA HIP HOP

Bila shaka wewe Chalii wa CHUGA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom