Zijue hatua 5 za usingizi

hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
2,811
5,599
Wana jamii habari zenu,

Nimeanzisha uzi huu kwa sababu ya mwanajamii mwenzetu aliyeniuliza kuhusu rapid eye movement(REM) nami nikaona ni vema kumjibu kupitia uzi huu kwa sababu REM ni moja kati ya hatua 5 za usingizi.

Usingizi ni kitendo cha asili cha kulala ama kupumzika kinachoambatana na ufumbaji wa macho kutokufanya kazi mwa misuli ya hiyari na kupungua hisia za mwili dhidi ya mabadiliko ya nje na ndani kwa mda usio wa kudumu.

usingizi husababishwa na kemikali maalumu zinazopatikna katika ubongo(sitaongelea zinasababishaje usingizi).

wakati mtu amelala ubongo unakuwa active na mifumo ya mwili pia inakuwa katika anabolic state.

wakati mtu amelala hupitia hatua tano za usingizi zinazojirudia rudia,hatua hizo ni kama ifuatavyo;

-hatua ya kwanza(1) ya usingizi;
hatua ya kwanza ni ile hatua ya usingizi mwepesi(light sleep) na ni kati ya unaponza kulala na kuwa macho katika hatua hii macho yanamove kidogokidogo na shughuli za misuli hupungua kidogo kidogo pia mtu usikia kwa mbali akiitwa.

-hatua ya pili ya usingizi(2);
ni hatua ya pili ya usingizi inayoambatana na kufumbwa kabisa kwa macho na misuli ya macho huacha kujivuta.

hii husababishwa na mawimbi ya ubongo(brain wave) yanayotokana na kubadilika umeme kwa kupungua na kuzalisha spindle waves.

-hatua ya tatu ya usingizi.
katika hatua hii mawimbi ya polepole ya delta wave huzalishwa na ubongo.

-hatua ya nne ya usingizi.
katika hatua hii ubongo uzalisha mawimbi ya delta mfululizo na kupelekea usingizi mzito (deep sleep)
hakuna kuyumba kwa macho na misuli ya mwili huwa relaxed pia ni ngumu mno kumwamsha mtu aliye stage ya 3 na 4 kwani usingizi huwa mzito sana.
pia ndio hatua ambayo watu ujikojolea hasa watoto.

-hatua ya tano na mwisho ni ni hatua ya rapid eye movement(REM) na ni kile kitendo kinachoambatana na kuchezesha misuli ya macho kwa haraka na kuduwaa kwa misuli(paralysis of muscle).
-chanzo cha kuduwaa kwa misuli(paralysis of muscle) ni kutokana na baadhi ya nerve cells zinazopatikana katika brain stem kuzuia huzalishwaji wa mono amine neuro transimitters kama vile histamine,serotonin na norepinephrine zinaso sisimua ufanyaji kazi wa motor neurone inayoamrisha ku kurelax na ku contract kwa misuli hivyo zisipozalishwa misuli huduwaa na kutulia (paralysis)

wakati huu wa REM;
-kasi ya upumuaji uongezeka
-misuli ya macho u move uku na huko

-misuli yote ya mwili huzubaa(paralysis)
-mapigo ya moyo huongezeka na damu husambazwa mwilini kote na kupeleka mpaka uume kupata damu na kusimama(kudinda) hii kumbuka ndo hatua ya mwisho ndio maana mwanamme anapoamka akiwa steji hii lazima uume wake usimame.
-mtu huanza kuota ndoto na ndoto zote huotwa katika hatua hii ya tano.
 
Ayaaaa!!! Mkuu umenionyesha embe mbichi alafu hukunipa. Weka nondo mistari iwe kama buku ivi.
 
Nimeipenda Elimu hii asante Doctor ongeza tena ujuzi, tongo tongo za kwenye macho zinatokana na nini doctor?
 
SWALI:Je ukipewa dawa za nusu kaputi zile wanazopewa wagonjwa ili kufanyiwa upasuaji unalala usingizi hatua ya ngapi?Tafadhali naomba jibu mtoa uzi!!!
 
Back
Top Bottom