Zijue faida za kuoga maji ya moto

Feld Marshal Tantawi

JF-Expert Member
Dec 24, 2014
609
1,007
Watu wengi hupendelea kutumia maji ya moto kuoga pale hali ya hewa inapobadilika na kuwa ya baridi au wakati mwingine mtu anaumwa hivyo anatumia maji ya moto.

Sehemu kama Dar es Salaam ni mara cheche utakuta wakazi wake wanaogea maji ya moto kutokana na hali ya joto katika jiji hilo.

Lakini kwa ajili ya urembo na afya ya ngozi, maji ya moto yanatajwa kuwa ni kitu muhimu sana kama vilivyo vipodozi vingine vinavyoisaida ngozi yako kuwa nyororo.

Hizi hapa ni baadhi ya faida zitokanazo na matumizi ya maji ya moto angalau mara tatu kwa wiki

Kulainisha na kutunza ngozi
Maji ya moto husaidia kulainisha ngozi yako tofauti na ukitumia maji ya baridi. Maji ya moto hasa yaliyo katika jakuzi ambapo utatumia muda mrefu kidogo ngozi yako ikiwa kwenye maji, husaidia kuilainisha ngozi yako na kuiweka katika hali nzuri.

Usingizi
Kama huwa unapata matatizo kupata usingizi usiku, amka oga kwa kutumia maji ya moto kwani husaidia kulainisha misuli ya mwili wako na itakaa sawa na utaweza kupata usinngizi.

Kukuweka katika hali nzuri
Kuna wakati mwingine mtu hujisikia uchovu wa mwili na kutotaka kufanya chochote (Off mood). Ukioga kwa maji ya moto yatakusaida kukuondolea uchovu na utajisikia mwenye nguvu na upo tayari kukabiliana na changamoto za siku.

Kuchangamsha ubongo
Unapooga kwa kutumia maji ya moto husaidia kuchangamsha ubongo na kuufanya uweze kufanyakazi kwa ufanisi na kwa haraka zaidi.

Kushusha shinikizo la damu
Ukiachanna na masuala ya urembo, kuoga maji ya moto kunatajwa kuwa ni njia ya haraka ya kusaidia kushusha shinikizo la damu. Tafiti zinaonyesha kuwa mtu mwenye shinikizo la damu la kupanda, akioga kwa maji ya moto husaidia kushusha.

Kusaidia mzunguko wa damu
Ukioga kwa kutumia maji ya moto husaidia kusisimu na kuitanua mishipa ya damu hivyo kuwezesha damu kuwa na mzunguko mzuri mwilini.

Licha ya kuwa maji ya moto ni mazuri kiafya, unashauriwa kuto oga kwa maji ya moto sana kwani huathiri ngozi.
 
Nasikia maji ya moto sio mazuri kuoga mara kwa mara kwa mtoto wa kiume.

Kwani cell za uzazi (sperm cells) zinahitaji joto la kadri ambalo hua ni chini ya lile ambalo maji unayooga yanakuwa nalo.

Kwahiyo mazoea ya kuoga mara kwa mara maji ya moto huleta athari za kiafya ikiwa ni mojawapo na kutokua vizuri kunako sita kwa sita. (Eti inasababisha ule ugonjwa wetu wa dakika mbili chali).

Sina hakika. Nilizipata tu somewhere

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mawazo tu ya watu ambayo sidhan km yana uthibitisho kisayansi lakni hata maji ya moto yenyewe yasiwe ya moto sn bali yawe ya kawaida sn
 
Nasikia maji ya moto sio mazuri kuoga mara kwa mara kwa mtoto wa kiume.

Kwani cell za uzazi (sperm cells) zinahitaji joto la kadri ambalo hua ni chini ya lile ambalo maji unayooga yanakuwa nalo...
Funika na kilambo! then oga huku kwingine
 
Back
Top Bottom