Bernard bakari
JF-Expert Member
- Mar 30, 2016
- 407
- 781
Mwanaume na mwanamke inafika mahali wanaacha wazazi wao na kujenga familia yao kama mke na mume ndivyo tulivyoagizwa na kwenye vitabu takatifu vya mungu. Ya kuwa Tazama mke utaacha wazazi wako na kuambatana mmeo. Napata shida wale wanaooa au kuolewa lakini bado hawajaacha wazazi wao either mme anaishi ukweni au mke anaishi na mwanaume ambaye bado anaishi na wazazi wake vitabu vyetu havijasema kitu kuhusu hilo wenda tuhitimishe kuwa wanakosea.
Lengo la mada hii ni kueleza kwa ufupi nini kazi ya mwanaume kwa mkewe katika maisha ya ndoa. Mme anazo kazi nyingi sana za kufanya kwake wake lakini leo tuangazie kazi tatu muhimu ambazo mme anapaswa kumfanyia mkewe.
Mme anatakiwa kuwa kiongozi kwa mkewe (Leader) wanaume tumeagizwa kuwaongoza wake zetu katika kila jambo ili kuhakikisha wanafikia matakwa na malengo yao. Katika kitabu kitakatifu cha mungu 1 Wakoritho 11:3 kinasema " Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanaume ni kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanaume..." . Hapa tunaaswa wanaume kujua kuwa sisi ndiyo vichwa vya wanawake yaan viongozi wa wanawake, tunatakiwa kuwaongoza katika misingi mizuri kumbuka kiongozi mbaya hufanya watu anaowaongoza waharibike nasi kama wanaume tumepewa dhamana hiyo hatuna budi kuitendea haki.
Kazi ya pili ambayo wanaume tunatakiwa kuwafanyia wanawake ni Kuwapenda. Maagizo hayo tumepewa toka katika kitabu cha mungu cha Waefeso 5:25 imeandikwa " Enyi Waume, Wapendeni wake zenu, kama Kristo naye akivyolipenda kanisa, Akajitoa kwa ajiri yake." Hiyo ndiyo kazi ya pili wanaume tumepewa kazi hiyo ya kuhakikisha tunawapenda wake zetu kwa upendo wa hali ya juu mwanaume ambaye hampendi mke wake si tu amethariti wajibu wake bali anamkosea hata mwenyezi mungu.
Kazi ya tatu ambayo tumepewa wanaume ni Kuwahudumia wake zetu. Mwanaume unatakiwa uhakikishe unamhudumia mkeo katika raha na taabu. Ikumbukwe mwanaume ni kiongozi wa mwanamke hivyo anatakiwa amhudumie kama ambavyo kiongozi yeyote anawajibika kuhudumia wale ambao anawaongoza.
Mungu tubariki sisi wanaume tutimize wajibu wetu kwa wake zetu kama vile ulivyotuagiza. Maana umesema mwanaume asiyempenda mke wake ni mchaafu maana umetuasa kuwapenda wake zetu kama tupendavyo miili yetu anayechukia mwanamke maana yake anachukia mwili wake pia. Katika wewe tutatimiza wajibu wetu kwa wake zetu mungu awabariki wote.