Zifahamu hatua 11 zinazofuatwa wakati wa kuchoma mwili wa marehemu

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,400
24,979
HATUA 11 ZINAZOTUMIKA

Kwa mujibu wa chanzo chetu chenye uzoefu wa maziko ya marehemu kwa njia ya kuchomamoto miili (cremation), kuna hatua kama 11 mpaka kumaliza zoezi la kuchoma mwili moto.

HATUA YA KWANZA; Mwili wa marehemu kuingizwa ndani ya jengo, ndugu wa karibuhuvunja nazi 3 katika kaburi lililokaribu kabisa na lango kuu.

HATUA YA PILI; Mwili hupelekwa kwenye tanuru ambapo mchomaji hupanga kuni juu ya tanuru hilo ambalo limeundwa kama kitanda cha chuma.

Kuni hupangwa kwa umahiri mkubwa katika mfano wa vyuma vya reli.

Magogo makubwa manne hupangwa kushoto, kulia magharibi na mashariki ya tanuru.

HATUA YA TATU; Kabla ya kuuweka mwili katika tanuru, ndugu wa marehemu huuzungusha mwili mara nne katika tanuru hilo.


HATUA YA NNE; Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya sanda nzuri huwekwa katikati ya kuni kichwa kikielekezwa upande wa magharibi.


HATUA YA TANO; Kabla ya uchomaji, ndugu huhakikisha kwa macho kuwa, mwili uliolazwa hapo ni kweli wamarehemu ndugu yao aliyefarikidunia.

HATUA YA SITA; Ndugu mmoja wa marehemu huchukua kipande kidogo cha kuni chembamba kilichoshika moto na kumchoma marehemu katika unyayo mara nne na kulizunguka tanuru.

HATUA YA SABA; Hatua inayofuata ni kuchukua moto kwa kutumia koleo maalum na kuuchanganya motona mafuta ya samli ili uweze kuwaka sana.

HATUA YA NANE; Ndugu wa marehemu huchota aina fulani za mbegu na kuzirushia juu ya mwili unaoendelea kuungua wakati huo huku ndugu wakilizunguka tanuru.

Kwa kawaida mwili wa marehemu huchomwa na kumalizika kabisa baada ya saa mbili au mbili na nusu na kinachotakiwa kubaki ni vipandevya mifupa.

HATUA YA TISA; Baada ya mwili kumalizika kwa kuungua, ndugu mmoja wa marehemu huchukua chungu maalum kilichojazwa maji na kukiweka katikati ya miguu, kisha hutazama upande akiyapakisogo mabaki ya mwili.

HATUA YA KUMI; Baada ya tukio hilo, ndugu na waombolezaji wengine wote hutakiwa kuondoka eneo la tukio bila kugeuka nyuma.

HATUA YA KUMI NA MOJA; Mabaki ya mwili ambayo kwa kawaida ni vipande vya mifupa ya mwili na fuvu, vilivyochanganyika na majivu namkaa huchukuliwa na ndugu kwenda kuyatupa baharini.


Chanzo: Maelezo kwa hisani ya mtandao.
 
Kuna nchi njia hii ndio ya bei ndogo sana kuliko kuzika mwili. Wanafamilia wengine wanamua wachomwe ndugu zao wasipoteze pesa kwa ajili yao.
 
Duh! aiseee hao ndugu wanaoshuhudia kuchomwa kwa mwili wana mioyo migumu! kama maiti huogopwa ingali na nyama zake, sipati picha pale anapo baki skeleton!!
 
Hakuelezea jinsi wanavyokabiliana na harufu, ya nyama ya maiti ya Binadamu, inayotoka pale kutokana kuchowa kwake. Huwa wanaiona inanuka, au inanukia.
 
Miye siwezi kubaki eneo la tukio nikishuhudia mpendwa wangu akiungua.
 
Back
Top Bottom