Ziara ya Rais Kikwete Mkoa wa Mara

Ziara ya Rais Kikwete Mkoa wa Mara

Nyamemba

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
845
Reaction score
447
Zikiwa zimebaki wiki mbili kabla ya ziara ya Mkuu wa nchi,mh Jakaya Kikwete katika mkoa wa Mara,mapya yameibuka baada ya viongozi waandamizi Mkoani kuandaa kile kinachoitwa kukwamisha malengo ya ziara hiyo.

Kwanza kabisa kuna miradi kadhaa inatakiwa kufunguliwa ikiwemo ya maji na ukaguzi wa maabara katika shule za sekondari,lakini kutokana na miradi mingi ya maji kuchukuliwa na baadhi ya viongozi wa CCM hasa wajumbe wa NEC miradi hiyo imejengwa chini ya kiwango hali inayotia wasiwasi iwapo unaweza kumleta kiongozi wa nchi kuifungua.

Hayo ni maneno ya baadhi ya watalaam mjini Musoma wakionyesha wasiwasi wao iwapo kweli Mh Rais atafanya kilichokusudiwa,"unajua tender nyingi hasa wilayani zinachukuliwa na either makada wa CCM au marafiki zao,hali hii inapelekea miradi mingi kujengwa chini ya viwango"alisema kiongozi huyo.

Mfano timu yetu ilitembelea miradi ya maji wilayani Serengeti na kukuta MNEC wa pale ameijenga chini ya kiwango na Mh Rais ndo anatakiwa aizindue,sasa hapo inakuwa mtihani.

Kwa upande wa maabara hakuna kilichofanyika zaidi ya kuyageuza madarasa na kuyakarabati eti yawe maabara,kwa kweli tutaaibika iwapo mh Rais ataamua kuendelea na kile anachokuja kukifanya ndugu yangu,na wengine wetu (watendaji) hatujui hatma yetu iwapo hili litajulikana,alisema afisa mmoja wa ofisi ya RAIS.
 
Nchi hii bhana...eti wataaibika.....yani hawajali kabisa maslahi ya wananchi ambao ndio wadau muhimu wa huduma hizo.
 
Rais kwenda Mara ajiandae vizuri kisaikolojia maana anaweza akakutana na zomeazomea kama iliyomkuta Pinda 2011 wakati wa bei ya kuruka ya sukari.

Zikiwa zimebaki wiki mbili kabla ya ziara ya Mkuu wa nchi,mh Jakaya Kikwete katika mkoa wa Mara,mapya yameibuka baada ya viongozi waandamizi Mkoani kuandaa kile kinachoitwa kukwamisha malengo ya ziara hiyo.

Kwanza kabisa kuna miradi kadhaa inatakiwa kufunguliwa ikiwemo ya maji na ukaguzi wa maabara katika shule za sekondari,lakini kutokana na miradi mingi ya maji kuchukuliwa na baadhi ya viongozi wa CCM hasa wajumbe wa NEC miradi hiyo imejengwa chini ya kiwango hali inayotia wasiwasi iwapo unaweza kumleta kiongozi wa nchi kuifungua.

Hayo ni maneno ya baadhi ya watalaam mjini Musoma wakionyesha wasiwasi wao iwapo kweli Mh Rais atafanya kilichokusudiwa,"unajua tender nyingi hasa wilayani zinachukuliwa na either makada wa CCM au marafiki zao,hali hii inapelekea miradi mingi kujengwa chini ya viwango"alisema kiongozi huyo.

Mfano timu yetu ilitembelea miradi ya maji wilayani Serengeti na kukuta MNEC wa pale ameijenga chini ya kiwango na Mh Rais ndo anatakiwa aizindue,sasa hapo inakuwa mtihani.

Kwa upande wa maabara hakuna kilichofanyika zaidi ya kuyageuza madarasa na kuyakarabati eti yawe maabara,kwa kweli tutaaibika iwapo mh Rais ataamua kuendelea na kile anachokuja kukifanya ndugu yangu,na wengine wetu (watendaji) hatujui hatma yetu iwapo hili litajulikana,alisema afisa mmoja wa ofisi ya RAIS.
 
Lameck airo kahodhi jimbo la Rorya kama Mali ya familia yake, tenda zote za halamshauri ya Rorya ka chukua yeye, matokeo yake anadanganya wananchi kuwa anatengeneza kwa pesa yake ,wananchi wasubiri kuchinjiwa ng'ombe
 
Nchi hii bhana...eti wataaibika.....yani hawajali kabisa maslahi ya wananchi ambao ndio wadau muhimu wa huduma hizo.
Hao panya wanapeana tenda zote alafu wanasema - eti wataaibika - ----
 
Watumishi na makada mara nyingi ndo wanamuangusha JK
 
Lameck airo kahodhi jimbo la Rorya kama Mali ya familia yake, tenda zote za halamshauri ya Rorya ka chukua yeye, matokeo yake anadanganya wananchi kuwa anatengeneza kwa pesa yake ,wananchi wasubiri kuchinjiwa ng'ombe
na yule mama kibaka
 
Hivi JK alisha mteu mkuu mpya wa Mkoa wa Mara baada ya yule wa zamani kufariki ghafla kule Tarime?
 
Mkoa wa Mara hauna Mkuu wa Mkoa kwa muda mrefu sasa; na Wilaya ya Serengeti ndiyo kabisaaa! DC wake alifariki miaka kadhaa, lakini hadi leo kuna kaimu tu. Sijui JK kaiweka Mara katika kundi gani. Aende akaone miti ilivyomalizwa kwa sababu mkaa sasa ndiyo biashara kuu ya maskini. Hakuna samaki kwa sababu viwanda vinasindika minofu, wananchi wanaambulia mapanki. Mara ni shida kweli kweli.
 
Week 2 zijazo kweli JK atakuwa kapumzika,sababu now anakula bata kwa Obama sasa akianza tripu ya kurudi mpk aje afike wangebadilisha timetable tuu.Aende November.
 
Mkoa wa Mara hauna Mkuu wa Mkoa kwa muda mrefu sasa; na Wilaya ya Serengeti ndiyo kabisaaa! DC wake alifariki miaka kadhaa, lakini hadi leo kuna kaimu tu. Sijui JK kaiweka Mara katika kundi gani. Aende akaone miti ilivyomalizwa kwa sababu mkaa sasa ndiyo biashara kuu ya maskini. Hakuna samaki kwa sababu viwanda vinasindika minofu, wananchi wanaambulia mapanki. Mara ni shida kweli kweli.

mkoa wa mara ni kati ya mikoa yenye neema ya kuwa na hali ya hewa nzuri kwa kilimo, huwa wakazi wa huko wanasema , tunavuna mara mbili kwa mwaka, nadhani wakitumia nafasi hiyo watafanikiwa kwa kuwa na kilimo chenye tija
 
Namshangaa Mzee Wassira anapiga jalamba la Urais ilihali Wilaya yake ni miongoni mwa wilaya masikini zaidi Tanzania na yeye kama mbunge na Waziri aliye karibu na Mh Rais mda mwingi ameshindwa kuiongoza wilaya/jimbo lake kuondokana na lindi la umaskini.Jamani nani aliuroga Mkoa wa Mara?
 
Back
Top Bottom