Ziara ya Pinda Manyara yatoa matumaini Kiteto

JAMHURI

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
450
225
Ziara ya mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda, Mkoani Manyara, imeingia siku ya pili kwa kutoa matumaini kwa wananchi na Viongozi.

Mhe Pinda alipokelewa Kijiji cha Dosidosi Kiteto jana na kuongea na wananchi akiwataka kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Magufuli katika kuwatumikia wananchi.

Akiwa Kiteto alikutana na
viongozi wa CCM na kuongea nao huku akipokea kero na changamoto zinazowakabili na kuahidi kuzitatua

Baadaye alifika shule ya Sekondari Engusero kuzindua bweni la wasichana lililojengwa na halmadhauri ya Wilaya kwa shilingi mil 86.4

Bweni hilo linauwezo wa kuhifadhi wanafunzi 84 ambalo limetajwa kuwa msaada mkubwa baada ya uhitaji kuongezeka.

Mhe Pinda aliwataka wanafunzi hao kusoma Kwa bidii na kuheshimu walimu wao ambao kazi yao ni kuelimisha wanafunzi.

Baadaye Mhe Pinda alienda kata ya Matui ambapo hapo alikutana na viongozi wa CCM na kuongea na kuhusu changamoto zinazowakabili.

Akiwa Kibaya Mhe Pinda alielezwa mengi ikiwemo migogoro ya ardhi na namna ya kuitatua, kuwa na Mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Kwa ujumla wanachama hao walizungumza kwa ujumla juu ya sekta ya Afya, elimu na Barabara kuwa bado Serikali inatakiwa kumaliza kabisa

Katika hatua hiyo Mhe Pinda pamoja na kuelezwa changamoto hizo pia aliwataka wananchi kuwa makini katika maendeleo yako

Mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 

dansmith

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
2,309
2,000
Lugola kaenda zenji kuzuia watu wa act kujiumga na chama tuuu halfu mtu anasema maendeleo hayana vyama
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,245
2,000
Atakuwa hana kazi za kufanya ndiyo maana ameona bora atumie muda wake kupuyanga. Au labda msimu wa kulina asali bado haujawadia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom