Ziara ya mama Samiah Suluhu mkoa wa Mara

Ziara ya mama Samiah Suluhu mkoa wa Mara

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024
Wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mugumu jimbo la Serengeti mkoani Mara
Mgombea Ubunge jimbo Dk. Kebwe Stephen Kebwe, Serengeti mkoani Mara, akiomba kura katika mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika katika jimbo hilo, jana, Oktoba 1, 2015. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, Christopher Sanya.
Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mugumu, jimbo la Serengeti mkoani Mara, Oktoba 1, 2015
Mama Samia akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Mugumu katika jimbo la Serengeti mkoani Mara
Kijana akifuatilia hotuba ya Mama Samia kwenye mkutano wa kampeni wa jimbo la Serengeti mkoani Mara
Ukarimu wa Serengeti
Mwananchi akimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mugumu, jimbo la Serengeti mkoani Mara, jana Oktoba 1, 2015.
Mwananchi mwenye ulemavu, akimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, aliposimama kwa muda kusalimia wananchi katika eneo la Mugeta, jimbo la Bunda Vijijini mkoani Mara, Oktoba 1, 2015
Wananchi akiwa wamezuia msafara wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan, katika eneo la Natta, ukitoka Mugumu kwenda Kisorya, Bunda mkoani Mara.
Mgomea Ubunge jimbo la Bunda Vijijini mkoani Mara, Boniface Mwita Getere akiomba kura, wakati msafara wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto), uiposimamishwa na wananchi katika eneo la Mugeta, katika jimbo hilo, jana, Oktoba 1, 2015.



Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia Mgombea Ubunge Jimbo la Mwibara, Kangi Ligora, alipowasili kufanya mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya mnadani, katika jimbo hilo, jana, Oktoba 1, 2015. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bunda mkoani Mara, Joshua Mirume.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi alipowasili katika viwanja vya Mnadani wa Kisorya, kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Mwibara, wilaya ya Bunda mkoani Mara, jana, Oktoba 1, 2015.



 
hao sio wakazi wa mara bwana au huijui mara mura tutakugecha na magufuli wako
 
Tutawaamulia tarehe 25,

nachofahamu ni kuwa Lowassa hakuuza nyumba za serikali, hakusimamia barabara zinazobomoka mwezi mmoja baada ya matengenezo, hakubomoa nyumba za wananchi maskini

Lowassa ni rais ajaye pamoja na kuitwa majina mengi ushindi kama kawa (Rejea Kenya - Uhuru, SA - Jacob Zuma, Italy - Baliskoni, Urusi - Putin, Nigeria - Buhari, wote hawa waliitwa mafisadi ila wananchi wao wakawachagua)

TL
 
Wananchi wakiwa na bango wakati wa mkutano wa kampeni za CCM wa Mama Samia, uliofanyika Oktoba 1, 2015, katika Viwanja vya Mugumu, Serengeti mkoani Mara.

Wanaonekana kabisa hawana amani,
kwasababu ya pesa tuu. So sad


Yani mi nashangaa sana kuona binadamu anaitetea ccm, kwa yapi iliyofanya?


We Mr chin ni lini utakua huru?? Unasupport kitu bila kuwa na sababu ya msingi.
Yaani nchi nyingine wanatushangaa kwa rasilimali zote tulizo nazo ila bado uchumi wetu upo chini,

Viongozi wa ccm kujilimbikizia mali ndo mnachoona sahihi
We kenua lakini kuna watu wana suffer kwasababu ya uongozi mbovu wa ccm.


Poor Mr Chin wake up men. Haya siyo maigizo just for the sake of our country.
Kama unaipenda Tanzania huwezi kuisupport ccm.
 
Mbona kama wamelazimishwa?

Watulivu ndo uchuja hoja ila wapayukaji hawanaga hoja, ukimuuliza nini kimesemwa wala hatakwambia kwasababu mda wote yeye alikuwa anapayuka tu
 
Hivi ccm wamewaroga watanzania au???
Mbona hamjitambui??
Kwa,hali ilivyo sitarajii kuona mtu yeyote anaitetea ccm. Sijui mtaamka lini.
Embu acheni uvivu wa kufikiria, amkemi bhanna.

Mnashindwa kuelewa serikali ya ccm imeipa hasara kiasi gani nchi yetu kwa maslahi binafsi.
 
Mbona wananyoosha kwa unyonge mtanyooka tu mwaka huu kizazi kipya kimejiandikisha na kinapanga kuwatia adabu.
 
Back
Top Bottom