Zawadi kubwa maishani ni hii

Zawadi kubwa maishani ni hii

charrote

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
1,987
Reaction score
4,409
Wapendwa mu wazima
Hivi karibuni kuna wimbi la watu ambao wana undugu sana na malaika limeibuka. Wao kucha kutwa ni kuwasimanga wanawake waliozaa bila kuolewa (singo mazas) na kuwaona hawastahili katika jamii .
Kwa kawaida binaadamu tuna tabia ya kujifunza kulingana na mazingira na nina uhakika kuna wanawake humu jf wanaogopa hiyo hali. Ndiyo unapaswa kuigopa na kuiepuka sana . Wanaogopa hasa kulingana na mabandiko yanayowekwa humu kila sekunde kuwakashifu wanawake hawa.Nawashauri wanawake wenzangu tujitunze tusiangukie katika hiyo hali lakini pia nikupe onyo

USITOE MIMBA
Nikupe siri hakuna mwanaume hataki kuitwa baba,mwanaume anapokuoa anataka mzae kwasababu WATOTO NI ZAWADI KUBWA MAISHANI.

SASA kama ulipata mimba ukaitoa kwa kuhofia kuitwa singo maza una hatari.Halafu bahati mbaya zaidi takwimu zinasema hali ya uzazi kwa sasa imedrop kutokana na lifestyle ,kazana kutoa sasa siku unataka huzipati hata ugegedwe kichwa chini miguu juu muulize madam.

Na hapo ndoa nayo inaota mbawa ,nani atakutaka umpotezee muda,Mwanamke akili kichwani ,nimekutana sana na wanawake wenye uhitaji wa watoto , ni wazuri, wameolewa,wana pesa lakini humo majumbani wanamoishi sio salama tena ni ulingo wa moto.Tujihadhar jamani lakini tusitoea mimba

Maisha ni zawadi .
Mtoto ni zawadi kubwa maishani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee umesema kweli tupu,kwanza hao wanaume wanaowasimanga wanawake singo mazas mbona wengi wao wamelelewa na hao hao singo mam mpaka wanakua?na kibaya zaid kisababishi cha huo usingo mam ni haohao wanaume maana wanawazalisha na kisha wanawaacha bila huduma.
 
Swadakta mkuu,umenielewa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoto sio zawadi sana katika maisha, the best gift ever ni uhai, Je usipokuwa hai anafaida ipi kwako? Ni sawa na gari.
nzuuuri lakini maeneo unayoishi hamna fundi wa kuitengeneza. Naam
hivyo hivyo uhai ndo zawadi kuu kwa
kiumbe chochoche Mali + watoto ni extra ili watu wafurahi uhai wao.
 
Sasa nawe ndo umeandika nini hapa!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina ndugu yangu mmoja wa karibu sana alicheza cheza sana enzi hizo nikawa namuona katoa sana mimba kutokana na michezo yake.

Mwaka 2010 kaolewa mpaka leo hana mtoto na naskia kaambiwa hawezi kuzaa tena.Saivi tunamuombbea dua tu Allah subhaanna wataala ampe miujiza kwani hakuna linaloshindikana kwake.

Ila usije ukanywa sumu makusudi ukasema Allah hasindwi kumponya mtu,utakufa na Allah anakuona hivi hivi.

Jirekebisheni enyi watoa mimba.
 
Wewe sio mzima .

Mkuu labda tuambie kwa ufupi huyo mtu anapitia hali gani ,kuna watu humu wanachukulia masihara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea vema,kama ni binti mdogo subiri na kama umepata kwa bahati mbaya zaa. Mimi ni mwanaume na nimeoa na naelewa maana ya kukosa mtoto hasa kama mama alicheza, familia bila mtoto nishida,sister yangu mkubwa alitoa akiwa shule hadi leo ajafanikiwa na nafeel anavyoumia japo hajakata tamaa anamwamini Mungu. PLEASE DON'T ABORT IT,WE LOVE THEM KIDS
. 32e059e227dc3ccd54a7047db4e59b3b.png
 
Mkuu labda tuambie kwa ufupi huyo mtu anapitia hali gani ,kuna watu humu wanachukulia masihara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiufupi anaonyesha hana wasiwasi lakini wanasaikolojia tunatambua kwamba hakuna ambae anapenda aonekane ana huzuni akiwa mbele zawatu.

Ukweli ni kwamba ana maumivu ya ndani kwa ndani yana mtesa sana kwa sababu anayaficha.
Mtu anayeficha maumivu anaumia sana kuliko mtu ambae anaonesha ana maumivu.

Ni sawa na mtu ambae amekanyaga kaa la moto alafu akaficha watu wasijue kama amekanyaga kaa la moto,hapapariki na wala hatoi mguu ili aendelee kuwathibitishia watu kwamba hana maumivu yotote,lakini wakati huo wote kaa linaendelea kumuumiza na kumchoma,mpaka akija kutoa mguu anajikuta ameshaumia saaaana,kaa limemuunguza vya kutosha.

Lakini mtu ambae amekanyaga kaa la moto mbele za watu na akatoa mguu haraka akajipuliza bila kujali kwamba atafedheheka,huyu ana nafasi kubwa ya kuyaepuka maumivu kwa sababu hakuchelewa kuyaitikia na kuyadhibiti.

Anapitia hali mbaya sana.na upendo kwetu sisi watoto wa ndugu yake unazidi sana kwa sababu anajua ndio watoto wake waliobakia na yeyr hawezi kupata mtoto tena,hivyo anatufanya kama watoto wake,ana mapenzi makubwa na watoto.

Nawashauri wote waliona huo mchezo waache mapema.
 
Umeongea vema,kama ni binti mdogo subiri na kama umepata kwa bahati mbaya zaa. Mimi ni mwanaume na nimeoa na naelewa maana ya kukosa mtoto hasa kama mama alicheza, familia bila mtoto nishida,sister yangu mkubwa alitoa akiwa shule hadi leo ajafanikiwa na nafeel anavyoumia japo hajakata tamaa anamwamini Mungu. PLEASE DON'T ABORT IT,WE LOVE THEM KIDS
.View attachment 1056693
Umenena mkuu, lengo ni kukumbushana kuwa sio vizuri kuzaa bila kuolewa lakini kama imetokea piga moyo konde kubali kuzaa, kuna leo na kesho watoto wanatafutwa sana mimi nimeshuhudia mpaka rafiki yangu akiniambia nahis nina mimba huwa nawapa jibu moja tu zaa .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnisamehe tu jamani kama nimehusika kwa namna moja ama nyingine katika kuwasimanga.

troublemaker 2019. all right reserved.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom