Mhafidhina07
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 3,678
- 5,166
Katika maisha kuna vitu tofauti ambayo hufanywa ili kuleta furaha/chachu ya mapenzi katika uhusiano, mojawapo ni zawadi. Kusema kweli zawadi ni kitu kidogo lakini kina effect kubwa katika mahusiano.
Mpenzi wako akinuna unaweza kumfurahisha kwa kutumia zawadi. Mfano mimi mnamo mwaka juzi(2014) kuna msichana nilikuwa na uhusiano nae kwa muda mrefu takribani miaka 2 lakini tukaingia katika mgogoro mwaka huo mwezi wa saba. Kiukweli nilimpenda sana na sikuwa radhi kumuacha hivyo nilitumia mbinu nyingi kupitia wadogo zake na dada zake kuniombea msamaha ila nikafeli.
Lakini Mungu si Athumani ikanijia akili ya kumnunulia kadi ambayo ilikuwa na misamiati ya msamaha pia nikaongezea na yangu pamoja na kapete basi ndiyo ikawa chachu ya kumpata tena.
Hapa najaribu kuwaonesha jinsi gani zawadi ni nzuri katika mapenzi. Naomba kujua wewe kama mwanaume/mwanamke ni zawadi gani ambayo ushawahi kumpa mpenzi wako akaifurahia?