Kwa kweli nilikuwa unguja kwa week moja ,na kabla ya hapo nilishawahi kuishi unguja miaka 5 hadi 2002.Zanzibar ya sasa imebadilika sana mazingira masafi sana!
Na kilichonivutia ni wao kutumia mifuko ya karatasi madukani na sokoni badala ya hii mweusi ya nailoni tunayotumia huku kwetu bara .
Yaani Zanzibar hadi Pemba hutaona mfuko wa plastic na hata kama unanunua bidhaa nyingi kuna mifuko mikubwa maalumu na rafiki kwa mazingira .
Mbona huku bara tulipiga marufuku hii mifuko ni kitu gani kiliirejesha kutengenezwa? Hii mifuko kipindi cha mafuriko ndio inaziba mitaro kwani haiozi .
Mboni ni rahisi tu kupiga marufuku tena kwa utawala huu hiyo ni amri moja tu kama ilivyokuwa viroba!