Bedui la bongo
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 297
- 306
Umenena mkuuHabari wadau wa JamiiForums
Binafsi napenda kuchukua fursa hii kutoa rai juu ya muungano wa Zanzibar kama ifuatavyo.
Zanzibar haistahili kuwepo na serikali inayojiendeshe yenyewe ya ndani sababu ni moja ya vikwazo vya maendeleo Zanzibar kuwafanya wananchi kutawaliwa na serikali mbili kitu ambacho hakiko kokote duniani.
Lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa Zanzibar ambae anamapenzi na Zanzibar na mzalendo wa kweli zaidi ya kuwepo viongozi wanaon'ang'ania madaraka na kulisha matumbo yao
Pia wanachi wa Zanzibar tunahitaji kupewa budget za kimikoa kama inavyofanyika huko bara na kusimamiwa kwa ukamilifu utumiaji wa fedha mana Zanzibar haibadiliki wanakula wao viongozi na kila siku wanakula kwa style mpya
Lakini la mwisho ni kwamba tushagundua kua Zanzibar na Tanzania bara tunaweza kuishi pamoja na kufanya mambo yetu kwa pamoja na tumeona na tunaaminiaana na tupo huru hasa wazanzibari tupo huru sanna bara mana tunaenda kukaa mikoani huko na tunakaribishwa na kuheshimiwa sanna
Hivyo nadhani ni wakati sasa kwa wazanzibari kudai muungano wa serikali moja tu
Zajua wasakatonge wa kisiasa wa chama tawala Zanzibar na upinzanj watagoma sababu ya maslahi yao binafsi ila tu waoumia ni wazanzibari hivyo serikali ya bara tunaomba mutusaidie kuiondosha serikali ya zanzibar hatuitaki inatukandamiza
Dr mwinyi anajitahidi sanna ila haiwezekani mana mafisi ni wengi na wanatumia style mpya zanzibar haiwezekani
Najisikia aibu kabla ya muungano zanzibar uchumi wake ulikua juu kuliko bara ila leo bara ipo juu kiuchumi kuliko zanzibar na nakataa kusema ni bara ndio inayodumiza maendeleo yetu Zanzibar bali ni viongozi wa zanzibar ndio sababu kuu
Nakuhakikishieni kua Wazanzibari ambao sio washabiki wa siasa wanahitaji serikali moja ili pia kuwepo na upendo na amani hasa katika kipindi cha uchaguzi, tuondeleeni serikali ya Zanzibar tuendelee kupendana na kuzikana serikali ya zanzibar imetufikisha pabaya hata leo kuna wengine hatuzikani