Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi (BLW) wamemchagua kwa kura za kishindo Spika mpya Zubeir Ali Maulid kwa kura 75 kuwa Spika wa Nne wa Baraza hilo. Maulid amewataka wajumbe wa Baraza hilo kufanya kazi kwa uadilifu na kuhakikisha wanaisimamia Serikali kuona inawajibika kwa ajili ya kuleta maendeleo licha ya kwamba Baraza hilo linaundwa na wajumbe wote kutoka chama tawala, CCM.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Dk Yahya Khamis Hamad alitangaza matokeo hayo yaliyotokana na wajumbe wa BLW kupiga kura ambazo kura 75 zilimchagua Maulid huku kura moja ikisema hapana.
“Ndugu waheshimiwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi uchaguzi wa kumchagua Spika wa Baraza la Wawakilishi umekamilika ambapo kura zilizosema ndiyo kwa Spika ni 75 na kura moja iliharibika kwa hivyo namtangaza Zubeir Ali Maulid kuwa Spika wa Nne wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,” alisema Dk Hamad.
Maulid alikula kiapo cha utii na uaminifu kwa ajili ya kazi za Spika wa BLW na kuahidi kuleta mabadiliko makubwa katika chombo hicho ambacho kipo kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa Zanzibar na kuwatumikia.
Aliwataka wajumbe kufanya kazi kwa kuzingatia uadilifu bila ya kujali itikadi za kisiasa huku wakiweka mbele uzalendo wa kuleta maendeleo kwa wananchi wa Unguja na Pemba na kupambana na umasikini.
“Nawashukuru sana wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa kunipigia kura na kupata ushindi mkubwa ambapo naahidi kufanya kazi kwa ajili ya kuleta maendeleo ambapo mafanikio ya yote hayo ni mashirikiano kwenu ninyi,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Bunge la Tanzania.
Baada ya kula kiapo cha utii alikabidhiwa katiba zote mbili za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ile ya Muungano pamoja na kanuni zinazosimamia utekelezaji wa kuendesha Baraza la Wawakilishi kutoka kwa Katibu wa Baraza na baadaye kuchukua nafasi yake ya kiti kwa kuapisha wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi.
Maulid anakuwa Spika wa Nne wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, akitanguliwa na Idriss Abdul Wakil na Ali Khamis (wote marehemu) na baadaye Pandu Ameir Kificho ambaye hivi karibuni alishindwa na Maulid katika uteuzi wa ndani ya CCM baada ya kuishikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka 20.
Source: Habari Leo