Zanzibar: Meli mpya yawasili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar: Meli mpya yawasili!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by n00b, Oct 1, 2012.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 950
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

  [​IMG]

  Kampuni ya Azam Marine inayomiliki boti ziendazo kasi hapa nchini, leo imeingiza meli mpya na ya kisasa itakayochukua zaiidi ya abiria 1500 na magari 200. Meneja Mkuu wa Kamuni ya Azam Marine, Bw. Hussein Mohammed Saidi, amesema leo mjini Zanzibar kuwa meli hiyo ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es Salaam, zanzibar na Pemba itatoza nauli nafuu kwa abiria wake.

  Amesema meli hiyo ambayo inatarajiwa kuanza safari zake mara baada ya kukamilisha taratizo za mamlaka mbalimbali. Meli hiyo inayoitwa AZAM SEALINKI ni ya kisasa katika ukanda huu wa Mwambao wa nchi za Kusini na Pembe ya Afrika.

  Bw. Hussein amesema Meli hiyo ambayo imetengenezwa nchini Ugiriki na inatayarishiwa eneo maalumu litakalotumika kwa kupakia na kushusha abiria na mizigo yakiwemo magari. Amesema meli hiyo itasafiri kwa muda wa saa tatu kutoka Dar es salaam na Zanzibar na saa 4 kutoka Zanzibar na Pemba ama saa 7 kutoka dar es salaam na Pemba.

  Amesema pamoja na kuwasili kwa Meli hiyo, Kampuni ya Azam pia inatarajia kuleta meli nyingine ya abiiria inayojulikana kama Kilimanjaro namba 4.

  Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Visiwa vya zanzibar wamepongeza ujio wa meli hiyo lakini wakaitaka serikali kuendelea kudhibiti uingizwaji wa meli chakavu na kukuu ili kuepuka uwezekano wa kutokea ajali za mara kwa mara.

  Bwana Rajabu Khamisi mkazi wa Pemba na Bi. Rehema Omari wa mjini Zanzibar, wamesema kuna haja ya Serikali kusimamia ukomo wa nauli ili kila mwananchi aweze kusafiri kutoka sehemu moja na nyingine kwani wamesema vipato havilingani.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  picha ???
   
 3. k

  kazidi Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 7, 2008
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  meli4.jpg meli1.jpg meli2.jpg meli3.jpg

  picha hizo za meli
   
 4. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mtukumbukage na sisi wa ziwa nyasa, au ndo tushakuwa wamalawi?
   
 5. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,498
  Likes Received: 5,408
  Trophy Points: 280
  wow!!. afadhali nimeiona. ina rangi ya chama kubwa chadema. mia
   
 6. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Monday, October 1, 2012


  [​IMG]

  Meli ya Azam Marine inayoitwa Azam SeaLink 1 ikiwasili katika bandari ya Visawani Zanzibar kwa mara kwanza.
  [​IMG]
  Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wakipiga picha Meli hiyo iliyowasili Visiwani Zanzibar leo.
  [​IMG]
  Mzee Said Bakheresa (mwenye nguo nyeusi) akikagua mazingira ya Meli hiyo baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo.
  [​IMG]
  Sehemu ya Parking yenye uwezo wa kuingiza magari 200.
  [​IMG]
  Muonekano wa ndani wa Lounge ya kumpzikia wasafiri.
  [​IMG]
  Muonekano wa nje. (Picha na Omar Said wa Kampuni ya Bakheresa).
  [​IMG]

   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Fantastic... Sasa itakuwaje MUUNGANO UKIVUNJIKA ? HIYO MELI ITAKUWA INAFANYA

  ZIARA kati ya PEMBA na
  ZANZIBAR ?
   
 8. b

  busar JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Asante Azam,, nitaendelea kunywa juice za AZAM
   
 9. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,069
  Likes Received: 6,001
  Trophy Points: 280
  Azam ana uwezo mkubwa wa kifedha kuliko serikali ya dhaifu
   
 10. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,420
  Likes Received: 1,586
  Trophy Points: 280
  Hii ni boti sio meli
   
 11. N

  Nyakipambo JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 435
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jiulize Muungano ukivunjika Alhaji Mwinyi atabaki Msasani au atahamia mji mkongwe?
   
 12. Root

  Root JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 23,752
  Likes Received: 9,758
  Trophy Points: 280
  Surely he does good for zanzibar

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 13. T

  Turbulence Senior Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mzee ni true businessman.
   
 14. madibira1

  madibira1 Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ni nzuri lakin HII SIO HABARI YA KISIASA kumbuka hapa ni jukwaa la siasa
   
 15. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,610
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Sasa wachome tena na kanisa jingine alafu ndipo wataona nini atawafinyia huyu Mungu mkuu wa Israel kama ktk zile meli 2 zilizopita.

  Enewei, God is good all the time and all the time God is good.
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  IKIWEKWA MNADA nitaigombea Sababu pia ina SELF CONTAINED BASEMENT !!!

  Ataenda MJI MWEMA LOL...
   
 17. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,600
  Likes Received: 9,675
  Trophy Points: 280
  lazima abaki MSASANI............ chezea daslam weye...........
   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,874
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145

  Kumbuka Issue ilikuwa ya KISIASA haukumbuki MBUNGE WAZIRI WA CUF alijiuzulu na WAZANZIBARI walitaka

  Waziri WA NDANI wa TANGANYIKA pia ajiuzulu ? Haukumbuki WABUNGE, Bungeni wote waliondoka wa CHADEMA na

  CUF na WA CCM WAISLAMU isipokuwa BIG BOSS ZITTO KABWE ???
   
 19. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,749
  Likes Received: 4,618
  Trophy Points: 280
  Muungano ukivunjika...biashara itayumba sana!!
   
 20. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 13,387
  Likes Received: 836
  Trophy Points: 280
  Hii ni dalili ya serekali iliyokolea kwa rushwa haingii akilini kampuni kubw akama VODA, TIGO NA AZAM, zina zidiwa kulipa kodi na CHIBUKU.
   
Loading...