Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Aidha katika kesi hiyo iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama kuu ya Zanzibar, Abraham Mwampashi, imethibitika kuwa Nangoma aliwaua Polisi wenzake kwa kuwapiga risasi kwa makusudi
"Kutokana na mshtakiwa kubainika na kosa la kuua kwa makusudi, Mahakama haina haja ya kusikiliza kumbukumbu za makosa na haitasikiliza utetezi kutoka kwa wakili wake" alisema Mwampashi
Polisi huyo alishtakiwa kwa makosa mawili tofauti ambayo ni kutumia silaha kuwaua wenzake, kwa kukusudia Juni 20, 2003 saa 11 :58 katika kituo cha polisi Chake Chake.
Hata hivyo Jaji ameiambia Mahakama kuwa kosa hilo alilofanya ni kinyume na kifungu cha 180 na 181 cha sheria namba 13 sheria ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Chanzo: Dar24