singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
BAADA ya kuapishwa kuongoza tena Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, juzi alimwapisha Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Hatua hii inaonesha kwamba baada ya kumalizika kwa uchaguzi, Dk Shein ameanza kuunda timu yake itakayowaongoza Wazanzibari katika kipindi kingine cha miaka mitano ambacho kikatiba ni cha mwisho cha uongozi wake.
Matumaini ya wengi ni kwamba Dk Shein ataunda serikali ya Umoja wa Kitaifa, kwani hilo alilizungumza mara kadhaa wakati wa kampeni mwaka jana. Ingawa katika uchaguzi wa marudio hakuna chama cha upinzani kilichofikisha asilimia 10 au kupata angalau mwakilishi ili kukidhi matakwa ya kikatiba, bado Shein anaweza kutumia madaraka yake ya kuchagua wawakilishi kutoka upinzani na hivyo kuweza kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Katiba inamruhusu Rais Shein kuchagua wawakilishi 10. Hata hivyo, la muhimu zaidi ni Wazanzibari kumuunga mkono katika harakati zake za kuijenga Zanzibar ikiwa ni pamoja na kudumisha amani huku wakizingatia kwamba ni yeye Shein aliyeridhia na kutekeleza uundaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, baada ya asilimia 66 ya Wazanzibari kutaka uwepo wa serikali hiyo.
Wazanzibari wakumbuke pia kwamba amani ya Taifa lolote lile ni nyenzo muhimu ya maendeleo na ni hatari kuruhusu amani iliyopo iharibike. Kwa vile chama chochote cha siasa kinaanzishwa lengo kuu likiwa ni kuwatumikia wananchi kwa kutatua changamoto za maisha yao, ni vyema vyama vya siasa vikiwemo vilivyosusia uchaguzi wa marudio vikajikita katika kusaidia utatuzi wa hali ngumu ya maisha ya Wazanzibari kwa kujenga hoja na kutoa njia mbadala na sio kuwagawa watu kwa kuwapandikiza chuki.
Baada ya Wazanzibari kuondoka katika siasa za chuki pale ilipoundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010, bado tunaamini kwamba mwanasiasa halisi ni yule anayewahurumia watu wake na si yule anayejinasibu kuivuruga amani na kupania kuifanya serikali iliyoko madarakani ishindwe kutekeleza majukumu yake.
Chama chochote makini cha siasa sharti kitambue kuwa amani hii iliyopo ndio kinafanya siasa na si vinginevyo. Zanzibar kwa muda mrefu imekuwa ikijulikana duniani kote kwa ukarimu, kuvumiliana na upendo wa watu wake. Tunu hii inapaswa kutunzwa na kila mwenye akili timamu.
Ni vyema sasa Wazanzibari wakasema yaliyopita si ndwele na hivyo wakaanza kuganga yaliyopo na yajayo kwa kuhakikisha hawarudi kwenye chuki za kisiasa. Ni kwa mantiki hiyo, tunaviasa vyama vilivyosusa uchaguzi sasa kuona namna vinavyoweza kushirikiana na Dk Shein katika kuijenga Zanzibar na siyo kuibomoa.
Ni vyema kila Mzanzibari akakataa kutumiwa, akaweka mbele maslahi mapana ya taifa lake, mintarafu suala zima la amani, upendo na utulivu. Iwe ni Zanzibar kwanza, siasa za vyama baadaye.